Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 24 September 2012

Wanaume na Mitindo;-Burudani-P-Square ft. Akon & May D - Chop My Money!!!!







Waungwana;"Wanaume na Mitindo"Mambo hayo!!Vipi wewe Baba/Kaka Vivazi hivi vinakugusa/vipenda? Jee unapenda kuvaa Saresare na Mke/Mchumba,Dada...wako?
Na kina Mama/Dada jee ungependa Mumeo/Mchumba,Kaka na.. wakitinga/kuvaa hivi? jee Saresare vipi?

Jee Wanawake mnakawaida ya kuwanunulia Waume zenu Zawadi au mmezoea kupokea tuu?.

Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.Mambo haya kutoka kwa Rafiki wa Mswahili;
Thanks my love Tarou:http://www.tarou.sn "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima........


Sunday 23 September 2012

Nawatakia J'Pili yenye furaha;Burudani-Yu mwema Mungu yu mwema,karen men's Chorate na Gael!!!!


Wapendwa nawatakia J'Pili yenye furaha,Kusifu,kuabudu,kusamehe na kusahau.....Je! waweza wewe kumvua mamba kwa ndoano? Au,kuufunga ulimi wake kwa kamba?
Neno La Leo;kitabu cha Ayubu;41:1-34........Yeye hutazama kila kilicho juu;Ni mfalme juu ya wote wenye Kiburi!!!

"Swahili NA Waswahili"MUNGU NA ATUBARIKI SOOOTE.

Friday 21 September 2012

Waswahili Wetu Leo-Ilava,Wanawake na Mitindo!!Unapenda Shanga??Jimwage!!!!!!!!!












Waungwana,"Wanawake na Mitindo" Leo Tupo Kinyumbani nyumbani,Si wengine ni Wswahili hawa  Waishio Nje lakini hawasahau ya Kwao.ni Ilava............

Ilava: It Can Be Done


Nisimalize Uhondo wooote, unaswali,Unataka Utoke Ki-

Afrika?Usisite kuwasiliana nao kupitia
Shopping & retail
Chicago, Illinois 60653



+1 773-805-0704
 
 Pia unawezakuwapata Facebook.
Mwanamke mwenzio/Mswahili mwenzio akifanya kitu kizuriri lazima umpe sifa yake!!!!
Wanawake wa Swahili na Mitindo/Majukumu.
Unalolote la kuongezea hapo?
Karibu sana Tunasubiri Maoni,


Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.


"Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima.

Wednesday 19 September 2012

Wanawake na Mitindo,Leo Tupo Senegal;Burudani-2face - African Queen!!!!!!!!






Waungwana;"Wanawake na Mitindo".leo Ki-dada/mama-Ki Afrikaaaa!!!!!
kwakweli mavazi haya hayamchukii mtu kwa Mtazamo wangu,kila Anayevaa anapendeza,tena Vazi hili linaupa mwili Nafasi na Kujiamini, Au.. weweee unaonaje?
Vipi wewe Dada/Mama ni Mpenzi wa Mavazi haya? wewe Kaka/Baba ungependa Dada/Mkeo au Rafiki yako Atinge hivi?
kwanini Unapenda na kwanini Huyapendi?

Funguka/Tuambiazane..........Mmmmhhh nisimalize Uhondo ngoja nisikilize na wengine...........
Picha hizi nimetumiwa na Rafiki yangu Tarou,yeye si Mswahili bali ni Rafiki wa "Mswahili" kina kaka/baba nanyi nitawarushia Msikonde wala nini.
Thanks so  Much lovely Tarou.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Monday 17 September 2012

Wanawake na Urembo;Ya Kale ni Dhahabu,Burudani-LES WANYIKA BARUA YAKO!!!!!!


 Waungwana; "Ya Kale ni Dhahabu" Alikuwa kabin'ti Enzi hiizo, sasa ni mama .
 Kuna kitu chochote unakumbuka katika picha hizi? Hizi nguo sijui zilikuwa zinaitwa Bahama au.......?

Karibuni sana Waungwana katika Yoote.kama Unapicha  za  Zamani unataka tuzirushe hapa, Usikonde Tuma;rasca@hotmail.co.uk. 

"Swahili  Na Waswahili" Pamoja Daima.

Sunday 16 September 2012

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani-Mamajusi Choir !!!!!!!!!!

Wapendwa nawatakia J'Pili yenye Amani,Baraka,Shukrani na Upendo.
Ondoka,Uangaze;kwa kuwa nuru yako imekuja,Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
Neno La Leo;ISAYA:60;1-6.

"Swahili NA Waswhili" MUNGU ATUBARIKI SANA.

Saturday 15 September 2012

Chaguo La Mswahili Leo;Dully Sykes : Lady Jaydee,Banana Zoro na Papii Kocha!!!!!!


Mabibi wa [doti com] Kileo na Mambo Yao!!!!!!Mama Erik/Kadala.Ndugu wa mimi na Waungwana woote, hapo vipi? bibi katupiaaa.........Mabibi wa leo hawataki,Sangula,Vanga,Mganda,Lizombe,Mbeta, Mdumange. Nao wanaungana na mangoma ya sasa. Vipi ndiyo maendeleo au?
Waungwana; "Chaguo La Mswahili Leo"ni mambo Mchanganyiko.
Hunifahamu sikufahamu iweje leo unipakazie!!!........mambo ya Dully....Banana nae na mambo ya oohh oohh Nzela mwanamama!!!
mmhh ngoja nikanywe Maziwa kwanza...

Waungwana  sina Meengi Twende sotee sasa, kuna lolote unalo lakuongezea,kukumbuka katika nyimbo za Leo?Tuhabarishe/tuelezee!!!!!

"Swahili NA Waswahili" PamojaDaima.