Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana? Tunamshukuru sana Mungu wetu kwa Neema/Rehema hii ya kutuchagua tena kuendelea kuiona siku/wiki/mwezi huu..si kwa uwezo wetu bali ni kwa mapenzi yake.. Tunaomba Baba wa Mbinguni ukatubariki,Tazama mwezi/wiki/siku mwingine/nyingine tena Baba tukakuja mbele zako tukishukuru kwa mema yote uliyotutendea na unayoendelea kututendea..Asante kwa pumzi na afya,Asante kwa ridhiki zako ,wema na fadhili zako,Asante kwa yote na tunaanza nawe Baba wa mbinguni kwa kila jambo, maisha yetu yapo mikononi mwako,Tunaomba ukatubariki na kututendea sawasawa na mapenzi yako..Tunaomba utuokoe na mwovu na kazi zake zote..Tunaomba utubariki tuingiapo/tutokapo,vyombo vya usafiri na tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Baba, kazi zetu,Biashara,Masomo,vilaji/vinywaji na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia ukavitakase kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo yeye aliteseka ili sisi tupate kupona...Baba ukatutakase Akili na Miili yetu pia.. Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda,kutambua/kujitambua na tukawe na kiasi... Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mfalme wa Amani kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua.. Tunaomba na sisi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea na tuwe na kiasi ili tusikwazane tena.. Tunawaweka mikononi mwako wote wanaopitia magumu/majaribu..Baba tazama wenye Shida/Tabu, wagonjwa,Wafiwa ukawe mfariji wao,waliokatika vifungo mbalimbali, waliokataliwa,waliokata tamaa,wenye mashaka/hofu,waliomizwa moyoni,Baba wa mbinguni ukawaguse na kuwaponya.. Tazama Yatima na wajane,wanaotafuta watoto Mfalme wa Amani,wanaotafuta wenza mke/mume ukawapatie walio wao na kuwabariki katika mahitaji yao.. Baba tunaomba ukabariki Ridhiki zetu ziingiazo na zitokazo ukazifanye baraka na kuweza kusaidia wengine.. Yesu Anakataliwa na Wayahudi...!!
Huko Yerusalemu kulikuwa na sikukuu ya kutabaruku. Wakati huo ulikuwa wa baridi. Naye Yesu akawa anatembea hekaluni katika ukumbi wa Solomoni. Basi, Wayahudi wakamzunguka, wakamwuliza, “Utatuacha katika mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, basi, tuambie wazi.” Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia. Lakini nyinyi hamsadiki kwa sababu nyinyi si kondoo wangu. Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata. Mimi nawapa uhai wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu. Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wala hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba. Mimi na Baba, tu mmoja.” Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie. Yesu akawaambia, “Nimewaonesheni kazi nyingi kutoka kwa Baba. Ni ipi kati ya hizo inayowafanya mnipige mawe?” Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa ajili ya kazi njema, ila kwa sababu ya kumkufuru Mungu! Maana wajifanya kuwa Mungu hali wewe ni binadamu tu.” Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika sheria yenu: ‘Mimi nimesema, nyinyi ni miungu?’ Mungu aliwaita miungu wale waliopewa ujumbe wake; nasi twajua kwamba Maandiko Matakatifu yasema ukweli daima. Je, yeye ambaye Baba alimweka wakfu na kumtuma ulimwenguni, mnamwambia: ‘Unakufuru,’ eti kwa sababu nilisema: ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’ Kama sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini. Lakini ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, walau ziaminini hizo kazi, mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake.” Wakajaribu tena kumkamata lakini akachopoka mikononi mwao. Yesu akaenda tena ngambo ya mto Yordani, mahali Yohane alipokuwa akibatiza, akakaa huko. Watu wengi walimwendea wakasema, “Yohane hakufanya ishara yoyote. Lakini yale yote Yohane aliyosema juu ya mtu huyu ni kweli kabisa.” Watu wengi mahali hapo wakamwamini.
Mwamini Mungu ndugu yangu..katika shida zako mwite yeye,katika Raha,Furaha mshukuru yeye...Yeye asiye lala wala kusinzia hatokuacha daima, binadamu hubadirika lakini Mungu yeye habadiriki kamwe ukimtumainia yeye na kufuata njia zake kamwe hutojuta.... Sifa na utukufu ni wako Mungu wetu, tunayaweka yote mikononi mwako,tukishukuru na kuamini wewe ni Mungu wetu.. Amina..!! Asanteni sana kwa wote mliopita hapa Mungu Baba muweza wa yote aendelee kuonekana katika mahitaji yenu na aendelee kuwabariki.. Nawapenda. |