Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 3 February 2013

Muwe na J'Pili ya Matumaini na Amani;Burudani-Suma Mwakalibule - Indumbula na Nyingine nyingii!!!!!!!!



Wapendwa;Nawatakia J'Pili ya Matumaini,Amani,Haki na Upendo...Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,Ambao hautatikisika,wakaa milele...Neno La Leo:Zaburi 125:1-5:Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,Ndivyo BWANA anavyozunguka watu wake,Tangu sasa na hata milele.........Endelea.

"Swahili NA Waswahili"
Amani ikae na Nanyi.

Saturday 2 February 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Mchanganyiko-BOZI BOZIANA,Franco&Sam Mangwana,Madilu...Mmmhh..Mooto!!!!!




Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo..Mhhhhh...motoo.mambo mchanganyiko.ya Kitambo kidogo....

Vipi hizi zinakukumbusha nini/wapi?.Zina kubamba/kuzipenda? Au hukupata kuzisikia?...

Twende sote sasaa.....Balobakiee..na Imalobato lembiyeeeh........kusemasema walisema tumechokaaa..Muongo na mulozi ni watu wa kuchomaaaah.......
Kujulikana kumbetabu mwana mbokaaa... Ukiwa shantii  kama Mushedo wanashangaaaa....ukitembea peke yako wanasema wewe ndiyo mbayaaaa....Kujulikana kuna mamboooo....Lwambo wetu Franco wandugu eeehhhh.......

Rafiki yake ananiaeeehh...wewe Mangwana ee...usiwafuate endelea jamani eehh...Ukipata Tabu omba kwa MUNGU eeeehhh Alafu MUNGU pekee  yeye Milele na Milele eeehhh........

Wewe na mimi kisa gani ayaahh Ndugu nimekosea nini Angalia  Makambooo eee....kama kuna mambo unielezee Taratibuuu eeehh kukorofisha mbele ya watu sitakieeeeehh sikia eeeeehhh.........

"Swahili NA Waswahili"Pamoja sana.

Thursday 31 January 2013

Jikoni Leo,Shaba,Soda Mtungini na.....!!!!!!


    Kitu cha Shaba..Pilau..haswaa hii la Shughulini.....


Soda za kwenye Mtungi...nimezipata hukooo Ruhuwiko....

  Kitu Chipsi na Nyama Choma/kuku..... hapa Diet hakuna...

Waungwana;Jikoni Leo..Mambo kama hayo....
mimi sina meengi..zaidi  nasubiri kutoka kwako ..

Umeshawahi  Kula shaba/Pilau.Chakula cha Shughulini?...Nini ubaya wake na Nini Uzuri wake?

Karibuni sana kwa Maoni/Ushauli na Kuelimishana kwa upendo.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaana.

Wednesday 30 January 2013

Watoto Na Mitindo;Pata na Video Hairstyle Slideshow!!!!


Aliye msuka huyu  ndiyo aliyekuwa akiwasuka watoto wangu..Nimefurahi kusikia bado yupo na anaendelea vyema na kazi zake kwa watoto...tena anawezana nao haswa...

Waungwana; Mimi naamini watoto wana Mitindo yao..pia wakipendeza wao wenyewe na wazazi tunakuwa na furaha sana..

Si Lazima au si wote wanapenda  watoto wasukwe..basi hata kama ana Nywele fupi..kuna Vibanio vyao pia wanapendeza sana......

Nao Watoto  kuna Umri wewe mzazi utamchagulia Mitindo ya Nywele lakini kuna Umri mwingine Mmmhh !!...inakuwa kazi ya ziada, Yeye/Wao hutaka hivi nawe unataka hivi..basi ni mabishano tuu..kama wapo wawili huwa wanaangaliana wao na kucheka au kuguna....hahahhaahhah imeshakukuta hii?

Karibuni sana kwa Maoni/Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.....

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.





Sunday 27 January 2013

Natumai mlikuwa na J'Pili yenye Kupendeza;Burudani-Bahati Bukuku-Dunia,Samehe!!!!!!!!!




Wapendwa natumaini mlikuwa na J'Pili yenye kupendeza.....

Tumalize J'Pili hii kwa.....Neno La Leo;Wakolosai;3:18-25;

[18]Ninyi wake,watiini waume zenu,kama ipendezavyo katika BWANA.

[19]Ninyi waume,wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.

[20]Ninyi watoto,watiini wazazi wenu katika mambo yote;Maana jambo hili lapendeza katika BWANA

[21]Ninyi akina baba msiwachokoze watoto wenu,wasije wakakata tamaa......Endelea....


"Swahili NA Waswahili" MUNGU awabariki Saana.

Monday 21 January 2013

Jikoni Leo;Ugandan foods & Cuisines!!!!!!!



Waungwana;Jikoni Leo Tupo Uganda...Pata kujua Mapishi yao na Maandalizi yoote.
Mengi sina ukitaka kujua Uhondo wa Ngomaaa..Ingia Ucheze..

   "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Sunday 20 January 2013

Wapendwa Nawatakia J'Pili Yenye Ushindi;Burudani-Geraldine Oduor - Wewe ni Mungu na Nyingine Nyingii!!!


Wapendwa Poleni na Snow natumaini hamjambo na kufurahia majira aliyoyaweka MUNGU na kushangilia. Ikiwa snow kama Greenland  Mchanga na Joto kama Sahara Baridi kama Himaya Mvua na Radi za Ikweta.Tusilalamike Nawatakia Kila la Kheri.....

Ujumbe huu  Wa kutia Moyo Nilitumiwa na Kaka yangu ALEX LUKUNDO Wa hapa COVENTRY .


Nami nimependa kushiriki nanyi  NA Kuongezea....Hasa mliokuwa kwenye Hali ya hewa kama hii isiwe sababau ya kukosa Kushiriki IBADA.




Wapendwa Muwe na J'Pili Njema, Yenye Unyenyekevu,Upendo,Busara ,Ushindi na Shukrani.Msijiwekee hazina duniani,nondo na kutu viharibupo,na wevi huvunja na kuiba;

Neno La Leo:Mathayo Mtakatifu:6:19-21;Kwakuwa hazina yako ilipo,ndipo utakapokuwapo na Moyo wako.

          "Swahili NA Waswahili" MUNGU Awabariki Sana.

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-Recipe of Basic Cupcakes for beginners - Mapishi ya (In swahili subtitle...!!!!!!!!



This is a video showing how to make basic Cupcakes for beginners, for East-African users and all the swahili speakers all around the world. It's also subtituled in English. Please, subscribe to our channel if you like it. We are working to offer you more video-recipes in swahili, in our Youtube channel and in our web-sitehttp://www.tupikepamoja.com/

Haya Waungwana si lazima kila kitu Mnunue......Jaribu mwenyewe na watoto watafurahi!!!!!!!

Jikoni Leo na Tupike Pamoja..Mmmmmhhhh Tamuuuuu Sanaaaaaaaaa.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Saturday 19 January 2013

Chaguo La Mswahili Leo:Mambo ya Pwani;AT - Bi Harusi,Mzee Yussuf-Na hiili Kaseme,Offside Trick-Aambiwe na Nyingine nyingiii!

w

Waungwana;Chaguo la Mswahili Leo ni Mambo ya Mduara/Taarab..... Ralaralaaaaaa...lalalaaaahhhh..Mmmhh ....mimi sina Mengi kama wewe unayo Funguka /Ongea tuu.

Swali la Kizushi;-Eti nyimbo za Taarab/Mduara nyingi zinauchochezi,Ushari,Vidongo na Umbea ......Haswa sa siku hizi.Za Zamani nyingi zilikuwa Kimapenzi Zaidi......Unasemaje Muungwana?

         "Swahili NA Waswahili" Twende Soteeee sasa.


Friday 18 January 2013

Watoto na Shangwe;Leo ndani ya Coventry ipo hivi!!!!!!!













Waungwana;Leo hali ya hewa Coventry ipo hivi...Lakini watoto wanafurahi sana....
Kwetu Bongo tunacheza kwenye Mchanga.....huku wacheza kwenye Snow!!!!!!!!
Baadhi ya Shule zilifungwa  mapema Leo.

Swali la Kizushi;Kule Nyumbani nilikuwa nasikia kuna Ugonjwa wa Ngiri kwa wanaume, Wakati wa Mvua/Baridi hasa Pwani.Jee waliokuwa wanaumwa huko Nyumbani Wakija huku wanapona?

"Swahili NA Waswahili" Pamoja sana.

Thursday 17 January 2013

SIMANZI KUBWA; JUDITH CHIKAKA AWALIZA CHUO KIKUU CHA ARDHI, WAFANYAKAZI WENZAKE WIZARA YA ARDHI, WANA CCM TEMEKE, CHAMA CHA WANARIADHA TANZANIA, MUMEWE ERASTO MAPUNDA NA WANAMICHEZO KWA UJUMLA.



Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.


Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga.
Marehemu Judith Chikaka alifariki siku ya Jumapili  ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa bahati mbaya na mapenzi yake muumba alifariki kabla ya kujifungua.


Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe.
Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka

Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi

Padre kutoka Parokia ya Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya Kigamboni Kibada.
Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa rambi rambi zao.
Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
Kushoto ni mwakilishi wa Familia ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa marehemu kutoka wizara ya Ardhi
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake.

Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda.

Marehemu Judith  alizikwa jana katika makaburi ya Kibada maeneo ya Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEME MAHALI PEMA PEPONI.
AMIN.


"Swahili NA Waswahili" Inawapa pole wafiwa na wote walioguswa na Msiba huu.

Wednesday 16 January 2013

Siku Kama Ya Leo Kaka Simon kitururu Alizaliwa!!!!

Kitururu na Utaifa..
Kitururu utotoni na wazazi..
Mtoto  Max ....ni Zawadi Kubwa kwake..... kitururu 
Kitururru..Baba Max na Ulezi..
Kitururu Mawazoni...Ametulia......

Kitururu na Mapishi....
Simon wa Kitururu Mitaani...


Waungwana;Siku kama ya Leo,Kaka Simon Kitururu,Babake Max....Muzee wa Yeah...kaka Kadoda.......duuhh Majina mengine atakuja kumalizia kaka  Ihayabuyaga Chacha O' Wambura.

Tunakutakia kila la kheri na Baraka Maishani mwako.Uwe na Wakati Mzuri Leo na Siku zote!!!!!

Swali La Kizushi...Unamfahamu /Kufikiri  ni Mtu wa Aina Gani  kaka Simon Kitururu? 

kujua zaidi kuhusu kaka huyu ingia;http://simon-kitururu.blogspot.co.uk/


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Watoto Na Malezi;Child Prostitution - South Africa!!!!







Waungwana;Watoto wetu ni Wapendwa wetu!!!!..Janga la Dunia...Nani wa kulaumiwa?

Mtoto wa mwenzio ni Wako au Mtoto wa mwenzio mkubwa Mwenzio?

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.


Monday 14 January 2013

Siku kama Ya Leo Kaka Isaac Alizaliwa!!!!!!

Siku kama ya Leo miaka kadhaa ilitopita, kaka ISAAC, babake Sandra na Tracey,Mume ya Madame Rachel.... Alizaliwa!!!!!

Tunakutakia kila lililojema Maishani, MUNGU azidi kukulinda na kukubariki kila iitwapo Leo.Akujaalie miaka mingi  yenye Amani,Furaha,Upendo na Upole Kiasi.. Ufanikishe Malengo yako na Uzidi kuwa Baraka kwetu na kwa Jamii.

 Na Iwe kama Tulivyo NENA.
AMEEEEEN!!!!!!!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.



Sunday 13 January 2013

Tumalizie J'Pili Vyema na Amani;Burudani-Solomon Mukubwa na Ambassadors of Christ!!!!




Wapendwa Natumaini mlikuwa na J'Pili Njema..kama kuna iliyokuwa na vikwazo,shida na Tabu..Mtegeemee MUNGU!!
Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake,Aliwaambia Enyi wazao wa nyoka,ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?

Neno La Leo;Mathayo Mtakatifu:3:1-17:Na tazama,sauti kutoka mbinguni ikisema,Huyu ni Mwanangu,mpendwa wangu,ninayependezwa naye.

   "Swahili NA Waswahili" Neema na Baraka za MUNGU  ziwe Nanyi Daima.

Saturday 12 January 2013

Chaguo la Mswahili Leo;Kutoka kwa Mdau -Image Profession;Burudani-Question:J.Kassam Ft. Ivan!!!!!!

 Mwimbo mwingine wa mwanamuziki chipukizi Juma Kassam akisindikizwa na Ivan ,anakuja kivingine 

akiuliza swali"Question",ni zaidi ya ubunifu.


Muelekeo mpya zaidi ya vile tulivyozoea ya nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi.





"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Friday 11 January 2013

Afya na Jamii;Na Mswahili John Haule- Nyama tamu, Inaua!


Historia yake:
Kwa miaka mingi sana nyama imekuwa chakula cha asili kabisa katika nchi yetu. Nyama imekuwa ikiliwa na inaendelea kuliwa na vyakula vya wanga, na hapo ndipo nyama ilikutana na jina jipya la kitoweo. Lakini pia nyama hailiwi tu kwa staili hiyo, nyama pia ilijikuta ikipata jina lingine kwenye mabaa na vilabu vya pombe iliposhushiwa na mafunda ya pombe na kuitwa asusa.
Nyama ni tamu sana. Kuna uhakika wa kitaalamu kabisa unasema nyama ikipikwa au kuchomwa basi utamu na mahitaji yake kiafya mwilini huongezeka mara dufu. Lakini nyama ukiikuta mezani itakutatiza sana kujua hii ni ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, au sungura. Vilevile inawezekana pia hata hisia zako zikawa tena mbali na ukweli maana nyama ipo pia ya porini kama vile pofu, nyati, mbuni, swala, digidigi na wengineo wengi tu, hivyo kuuliza kabla ya kula nyama ni muhimu sana hasa kwa wale wenye miiko na baadhi ya vyakula na waislamu ambao baadhi ya nyama kwao zimeharamishwa. Ila mimi nawaongezea jicho la tatu ndugu zangu hao kuwa IMEHARAMISHWA tu lakini HAIKUKATAZWA kuila kama hutakuwa na jazba kunielewa utagundua hivyo. Na mimi nafikiri leo naziharamisha nyama za aina zote hapa kwa ushahidi wa madhara ya kiafya na kiroho pia.
Mungu pia hapendi nyama:
Kama mtakumbuka mliosoma Biblia, Wajukuu wa Mungu Kaini na Abeli walijikuta siku moja wakimtolea babu yao sadaka. Kaini akiwa kama mfugaji alichinja akamletea Mungu nyama. Mungu alikataa na sadaka yake haikuteketea! Lakini Abeli akiwa kama mkulima yeye alileta mazao ya shamba lake. Mungu alipokea! Ikawa Kaini akamwuua nduguye Abeli na kizazi cha wafugaji kikajimegea dhambi ile mpaka leo.
Nyama inajenga matabaka:
Enzi zetu za kujisomea hapa nchini kila nyumba ilikuwa na “Book Shelf” Leo zipo wapi? Sisi tulisoma kitabu kilichoitwa UPUMBAVU WA MWAFRIKA na ndani kulikuwa na hadithi nyingi tamu ikiwemo “Uchu wa Mzee Mikidadi” ambayo tulipoisoma tulielewa kuwa nyama ina nguvu ya kuwagawa watu kimatabaka kwa uchu tu wa wenye madaraka, ukiachilia mbali madhara makubwa zaidi ya kiafya.
Uharamu wa nyama umeifanya jamii iwatenge wanyonge na kuwakweza wenye nguvu na mamlaka katika kila Nyanja ya maisha. Angalia, Katika vitoweo vyote nchini na duniani hakuna ambacho ni ghali kama nyama. Wanakula wenye pesa tu. Wapo akina mama wa kambo walioripotiwa kuwalisha nyama watoto wao na kuwalisha maharage wale watoto wa kambo. Katika jamii yoyote wenye mamlaka na nguvu ndio wanao faidi nyama huku wengine wakiambulia mchuzi na mifupa. Ukiandaa sherehe usipoleta nyama watu watakuwa hawakuelewi kabisa toka miguuni hadi utosini. Nyumba Fulani Fulani nyama hupakuliwa na mama. Mboga za aina nyingine ni ruksa yeyote kujipakulia. Wengine wameripotiwa kuwahesabia finyango za nyama wake zao. Wapo pia wanawake waliopewa nyama kilo moja wapike ikafika mezani robo kilo tu, lakini watu watakuambia wapo wanaume wanaokula kilo ya nyama wakiwa baa na huku mke na watoto wanalalia uji. Huku utasikia mtoto kachomwa mikono kisa eti kadokoa nyama, na mikasa kadha wa kadha inayotutahadharisha kuwa nyama itatutoa roho!
Nyama inaua:
Lakini umeona jinsi tulivyoiangalia nyama kwa historian a taswira tu bila kuiangalia madhara yake kiafya ambayo ni lukuki kiasi hayaorodhesheki hapa leo. Nyama inatakiwa iliwe kwa dharura tu na sio kama mlo kamili kwa kuwa nyama ina rekodi ya kuua walaji wake kimya kimya bila wao kujijua kama wanateketea. Mfano watu mia waliokula nyama kilo moja kila mtu kwa siku, watu 30 walikufa baada ya miaka kumi na kuwaacha wengine taabani kwa magonjwa ya moyo kama kisukari, BP, kupooza, ganzi n.k. Si hayo tu, bali magonjwa ya ini, figo na mapafu yalisababisha vifo pia.
Unapokula nyama unaongeza lehemu na mafuta yabisi mwilini ambayo hupenya na kuingia katika mishipa ya damu na kuganda katika kuta zake. Kadiri mgando unavyoongezeka ndivyo njia ya damu inavyopungua na mwisho kuziba kabisa! Sumu hizo zinapoanza kuganda mgonjwa ataanza kuhisi matatizo na akipimwa atakuta mapigo ya moyo yamefeli yaani BP. Kadiri atakavyoendelea kula nyama na kuziba mishipa basi siku moja damu itapita kwa shida sana na ataanza kusikia ganzi sehemu zote zisizopata damu. Mwisho mishipa ikiziba kabisa ndio huwa tunaita mtu amepooza. Maana hakuna damu inayoenda huko tena! Dawa za wagonjwa hawa ni kitunguu swaumu na mafuta ya Sardine toka Ueskimo tu. Kitunguu swaumu niliwahi kukiongelea na nafikiri walionisikia wanaelewa cha kufanya. Ila haya mafuta ya Sardine toka Ueskimo nitayaongelea siku nyingine.
Nyama inadhuru kisaikolojia pia:
Watu wa jamii za wafugaji na walaji wakubwa wa nyama kwa ujumla ni wakorofi sana. Ni waoga na wanaweza wakakudhuru bila kuwa na sababu za kutosha. Hawa jamaa wanaamini kuwa kama huna silaha basi wewe si mwanaume. Hii imetokana na kujilundikia kiasi kikubwa cha lehemu na sumu nyingine toka katika ulaji wa nyama uliokithiri. Hupenda kulala wakiweka silaha kwenye mto ili wajiridhishe kuwa wanalala salama. Kama ni hohehahe ataweka sime hata kisu tu, wakati mwenye pesa ataweka bastola kabisa. Cha kukuchekesha msomaji wangu leo ni kuwa watu hao nchini tumewapa “kibali baridi” cha kutembea na silaha popote! Kama huamini toka wewe na jambia lako mkononi kama utafika popote kabla polisi na watu wa usalama hawajakukamata. Utakamatwa kwa sababu si sheria kutembea na silaha hadharani wote tunalijua hili, lakini hawa ndugu zetu asili yetu imewakubali watembee hata na mikuki na hatuwaulizi kulikoni.
Ikaja pia staili mpya ya kuwaajiri kazi za ulinzi baadhi ya wala nyama hawa. Wenye akili zetu tulibaki midomo wazi tukiamini staili hii itakufa siku si nyingi baada ya wanaowaajiri kukutana na hasara ya kuibiwa kila kukicha. Na kweli leo hii wamesahaulika… Mtu mwenye kiasi kikubwa cha lehemu mwilini ni mwoga, hajiamini, na vitu kama hivyo kwa kuwa damu haitembei ipasavyo. Sasa mtu mwoga atalindaje wakati yeye mwenyewe hajiamini na anatembea na silaha lundo! Yatakuwa maajabu sana.
Madhara ziada ya nyama:
Lakini madhara ya nyama bado hayaishi kama nilivyodokeza hapo awali. Kuna hili ambalo sitaliacha. Ng’ombe, mbuzi, kondoo na mifugo mingine huwa wanakula chochote kitamu kwao wanachokiona ardhini sote tunajua. Lakini tumeshuhudia wanyama hao wakila nailoni, misumari, nywele bandia, na sumu nyingine nyingi tu tunazozalisha binadamu. Sumu hizi tunakutana nazo tunapokula nyama na hakika zinatudhuru vilivyo. Haya, Wanyama hao hao huwa tunawapeleka josho kuua wadudu mwilini. Sumu ya zile dawa ni lazima ukutane nazo ukila nyama. Unalijua hilo? Wachilia mbali sumu hizo, wanyama hupewa dawa wanapopatwa na maradhi tena dawa kali (antibiotics) ambazo utazila na nyama na hatari yake ni kukujengea usugu dhidi ya dawa za kibinadamu pale utakapougua. Ni hatari sana.
Kwa mila na desturi zetu watanzania tuna nunua nyama pale buchani. Utakuta gogo moja limevilia damu na ndilo linalotumika kukatakata nyama. Pale utajiuliza kwanza usalama wa nyama juu ya lile gogo upoje maana hujui ni mti gani, una kamikali gani, zinaua au ni salama na maswali mengine lukuki. Lakini ukimwuliza muuza nyama hatakupa jibu lolote la kukuridhisha pale. Hajui. Upo mtaa Fulani wanaume walikuwa wafanyakazi wa reli ambao walikuwa wakila nyama kwa wingi kuliko wake na watoto wao. Leo hii mtaa hauna baba wote wamefariki. Kwa niaba ya watanzania wote naishauri wizara ya afya kupitia mamlaka husika kuangalia uwezekano wa kufunga misumeno ya kukatia nyama katika mabucha ya nyama maana ndio utaratibu duniani kote na ndio ustaarabu. Vinginevyo kuna watu wanakufa kimya kimya.
Bado tu nyama inaonekana ina maambukizi dhidi ya maradhi zaidi kuliko mboga za majani, matunda na nafaka. Nyama hubeba wadudu wanaojulikana na wasiojulikana kila unapoila kuja kukuambukiza maradhi ya aina mbalimbali.
Nile ua nisile nyama?
Lakini, nyama bado ina utetezi wa kutosha kuwa na faida za kiafya. Msomaji wangu ona nyama jinsi ilivyo shetani maana haieleweki kama tule, au tusile. Nyama hasa nyekundu ni muhimu sana kwa afya yako lakini, inakubidi ule kidogo sana kama finyango tatu tu kwa wiki, hiyo ni kitaalamu. Ukiifanya mlo rasmi utakufa! Cha ajabu wakati vyakula vingine vikipikwa hupoteza ladha na uthamani wake, kwa nyama mambo ni tofauti kabisa maana ikipikwa, ikichomwa, ikikaangwa ikiokwa nk ladha huwa tamu ajabu na uthamani wake mwilini huongezeka mara dufu. Ukila nyama unajipatia madini ya chuma, zinki, na protini kwa wingi mno.
Wengi wa wagonjwa walioshindwa vitandani wanahitaji sana chuma, zinki na protini kuamka na kupona haraka. Chuma humsaidia mtu kuwa na kinga dhidi ya maradhi sasa kama hukupata virutubisho vya madini hayo basi unaweza kufa hapo kitandani kwa kuwa hukula nyama mpaka chuma imeisha mwilini, hivyo usubiri ugonjwa utakaofuata Anemia na baadaye kaburini. Mgonjwa huyu utamjua kwa dalili hizi: Kapoteza uzito, ngozi imemkauka, mapigo yake ya moyo yanaenda mbio au taratibu sana, Hana pumzi, kifua kinambana, kizunguzungu, hakumbuki tena kitu, kichwa kinamuuma lakini sio malaria, miguu na mikono imekufa ganzi nk.
Usipokula nyama pia tumesema utakosa madini ya zinki. Zinki pia ni kiboko kukupa kinga ya mwili upambane na maradhi sasa kama hamna lazima maradhi yakulaze kitandani. Wanandugu mpeni virutubisho vya zinki kabla hamjampoteza ndugu yenu. Mkitaka kumjua kuwa anahitaji zinki angalieni yafuatayo: Mgonjwa hana utulivu na usiku hapati usingizi, kama ana vidonda haviponi, ana vidoadoa au alama ya nusu mwezi katika kucha zake vidoleni, anakosa nguvu nk. Ukiona dalili hizo hebu wahi umpe virutubisho vya zinki apone vinginevyo mtamkosa.
Lakini pia usipokula nyama unajikosesha protini. Protini ikipungua mwilini utaona mgonjwa anapata tabu kupona vidonda, analalamika viganja vinawaka moto, analalamika miguu inamuuma na muda mwingine atasema tumbo pia linamuuma mara kwa mara, hana nguvu, anashambuliwa na maradhi ya ngozi na wengine hukonda vibaya.
NATIVA ni suluhu:
Hapa Tanzania kuna virutubisho vya kurejesha afya ya mgonjwa huyo haraka na salama. Makampuni mengi yapo kiushindani katika biashara hiyo kila mtu akikushauri kutumia zake. Mimi kwa uzoefu wa maradhi haya nakuelekeza msomaji wangu tumia virutubisho vya kampuni ya NATIVA toka Afrika Kusini kama unatafuta suluhu ya uhakika na haraka kwa mgonjwa wako. Nativa wapo mji mzima na ukihitaji dawa nipigie tu simu nitakusaidia kuzipata.
Wapo wakulima ambao si wafugaji nap engine kupata nyama si kitu rahisi. Kizazi cha Abeli yaani Wakulima wao madini ya chuma, zinki na protini wamejaziwa kwenye mazao yao hivyo utavipata vitu hivi ukila mboga za majani, karanga na jamii yote ya njugu, maharage na jamii zake, matunda kwa wingi nk. Hivyo hakuna sababu ya kungoja upungukiwe na madini hayo mwilini.
Kula nyama msomaji wangu. Lakini usiigeuze kuwa mlo rasmi, kula kama waislamu walivyoambiwa katika msaafu kuwa nguruwe ni haramu aliwe kwa dharura tu. Lakini mimi leo nakuambia wewe kula nyama yoyote kwa dharura tu. Kama Mungu alimkatalia mjukuu wake Kaini sadaka ya nyama aliyomtolea jiulize nyama ina nini?
Bwana pori mmoja alisema hivi: Baba anayekula nyama kwa wingi anajijengea uhayawani wa ndege na wanyama wanaowala wenzao (predetors) msituni. Na ndio maana huwa baba wa aina hii huzinyanyasa familia zao…
Kama umekula nyama kwa muda mrefu na unajihisi dalili zilizopo hapo juu tafadhali tuwasiliane nikusaidie. Kama una mgonjwa wa kisukari, kupooza, presha zote, kupungua na kuzidi uzito pamoja na dalili za maradhi kwa kukosa madini kama nilivyoorodhesha hapo awali basi usisite kunitafuta ili nikupe dawa za uhakika upone.
Asanteni sana kwa kunisoma na mungu awabariki sana.

            "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.