Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 25 August 2013

Tumalizie J'Pili hii kwa Amani na Upendo;Brudani-Angela Chibolonza!!!

Wapendwa;Tumalizie J'Pili hii Vyema.

Lakini,ndugu, kwa habari ya nyakati na majira,hamna haja niwaandikie..........
Neno La Leo;1:Wathesalaonike:5:1-28..
[4]Bali ninyi,ndugu, hammo gizani,hata siku ile iwapate kama mwivi[5]Kwakuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana;sisi si wa usiku, wala wa giza.[6]Basi tusilale usingizi kama wengine,bali tukeshe na kuwa na kiasi.

[16]Furahini siku zote;[17]Ombeni bila kukoma;[18]Shukuruni kwa kila jambo;maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika Kristo YESU.

[25]Ndugu,tuombeeni.[26]Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.[27]Nawaapisha kwa BWANA, ndugu wote wasomewe waraka huu.

[28]Neema ya BWANA wetu YESU Kristona iwe pamoja nanyi.










"Swahili Na Waswhili" Mbarikiwe Wote.

Wednesday 21 August 2013

Kisa Cha Leo na Mswahili Emu-Three;Wema Hauozi-Sehemu ya 52!!!!!



Tulitoka nje ya lile pango huku tukiwa tumekata tamaa ya kumpata huyu mtu tena,ikizingatia kuwa yeye analifahamu hilo pango lilivyo, na sisi japokuwa tupo wengi, lakini njia za kupita zilihitajia mtu mmoja mmoja,…

Bado tukiwa na matumaini ya kumpata huyo mtu akiwa hai, tuliharakisha kutoka, ili kuungana na wenzetu waliokuwa wakijibisha risasi na huyo jamaa, na baadaye kukawa kimiya, ikiashiria kuwa huenda huyo mtu alishatoka nje,

Swali likawa je kama huyo mtu kawahi kutoka nje, itakuwaje, kwani hatukukumbuka kumuacha askari zaidi ya mwanasheria, wote tulikimbilia kuingia ndani..na je hiyo amri ya kutokutumia risasi huko nje, itawezaje kuepukika, na mtu kama huyo?

Tuendelee na kisa chetu......

Tukajitahidi na sisi kutoka nje kwa haraka haraka, na tulipofika nje, tuliwaona askari wetu wamesimama huku wameelekeza silaha zao upande wa pili, kama wanawinda kitu, na mkuu ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka na bastola yake mkononi, akawauliza vijana wake

‘Yupo wapi’ akauliza

‘Mkuu kaingia kwenye hicho kichaka, na cha ajabu haonekani tena, lakini tuna uhakika yupo hapo, na tunahisi kuwa hayupo peek yake,…’akasema mmoja wapo, na wote wakaelekea kwenye hicho kichaka na kwa mbele wakaona watu wawili wakiwa kwenye mapigano na kila mmoja akiwa kamshika mwenzake mkono, ili kuzuia silaha yake, isielekezwe kwake.

Msaidieni mwanasheria, lakini msitumie silaha, kumbukeni tulivyoambiwa, ….’akasema mkuu, huku nay eye akielekea kule ambapo mwanasheria alikuwa akipambana na huyo mtu, na ilikuwa vigumu kuingilia kwani zile silaha walizoshika zingeliweza kufyatuka na kuleta madhara kwa yule ambaye angeliwakaribia, kwahiyo ikawa kutafuta jinsi ya kusaidia.

Mwanadada ambaye alikuwa nyuma akiwa na yule binti, alifika eneo hilo na kuona hiyo hali, na hapo akasema;.

`Mbona mumesimama, hamumsaidi mwenzenu…’akasema mwanadada, akikimbilia kule kwenye mapigano kati ya mwanasheria na huyo jamaa na alipofika tu, akasikia mlipuko wa risasi,…..oh, mwanasheria akapanua mdomo, na kudondoka chini, na yule mtu alipoona hivyo, akainuka kutaka kukimbia, lakini hakuweza hata kuinua mguu.

Risasi ililengwa bara bara, kutoka kichani, na yule mtu akatoa macho ya uwoga, na kudondoka chini, na hapo mwanadada na mkuu, wakawa wameduwaa, ina maana kazi yote imekuwa ni bure, ina maana masharti ya msituni yamevunjwa, na haijulikani ni kitu gani kitatokea.

Mkuu akamkimbilia yule mtu, na kuhakikisha hana silaha, na akamshika kuangalia kama yupo hai, na akainua kichwa kumwangalia mwanadada na kusema;

soma zaidi ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

Tupo pia kwenye: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three
https://twitter.com/emuthree



"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Tuesday 20 August 2013

Afya Na Jamii;TATIZO LA MIFUPA AU KUUMWA MIGUU/MAGOTI: OSTEOPOROSIS:


Tatizo hili hujulikana kwa jina la kitaalamu kama Osteoporosis. Ugonjwa huu unatokana na kupunguka kwa protini na madini kwenye mifupa (madini chokaa/calcium). Hali hii hupelekea mifupa kuwa milaini na myepesi ambapo inaweza kuvunjika kirahisi. Kipindi cha utoto hadi kufikia umri wa miaka 30, ni kipindi ambacho mifupa hujijenga zaidi. Baada ya hapo mifupa huwa ina kawaida ya kupoteza madini zaidi.
Tatizo hili linatokea sana kwa watu wazima, hasa zaidi kwaa wanawake ambao wamefikia kipindi cha kukoma hedhi (menopause), kuanzia miaka 50. Ni kipindi ambacho wanawake hupungukiwa na homoni yenye kazi ya kuilinda na kuikinga mifupa. Tatizo hili huwapata wanawake zaidi kwa kuwa wana mifupa midogo na myembamba kuliko wanaume. Miaka mitano (5) hadi aba (7) tangu mwanamke kukoma hedhi hupungukiwa na madini chokaa kwa asilimia ishirini (20%), zaidi ya wanaume. Kuanzia miaka 65 hadi 70 wanawake na wanaume hupoteza madini chokaa kwaasilimia sambamba.
NINI CHA KUFANYA
1. Mazoezi hasa kipindi ambacho umriu mepiga hatua
2. Kwa wale wenye uzito uliozidi, jitahidini kufanya utaratibu wa kupunguza
3. Jitahidi kupata madini chokaa (calcium) kwa wingi (maziwa freshi, maziwa mgando, mboga za majani)
4. Jitahidi kupata Vitamini D (mayai, maziwa, samaki, mboga za majani, pata jua)
VIRUTUBISHI
Kwa ambao tatizo limekuwa kubwa, inawapasa kujitahidi kupata virutubishi ili kuirejeshea mifupa nguvu na uimara, pia kuondokana na maumivu.
Virutubishi vifuatavyo vimewasaidia wengi wenye tatizo hili.
1. Calcium
2. Chitosan
3. Lycopen



KUKOSEKANA KWA UTE KATIKATI YA VIUNGO (JOINTS) - CARTILAGE

Kajiraba fulani ambako hujulikana kwa jina la kitaalamu kama “Cartilage” (katileji) ambako hupatikana katikati ya mifupa. Kuna kitu fulani huwa kinapatikana katikati ya mifupa miwili ya goti la mnyama (ng’ombe, mbuzi) huwa wengi wanapenda kukila kwenye baada ya kuchemshwa au kupikwa. Kama unaijua hii, basi ndio katileji yenyewe.
Katileji inasaidia kuikinga mifupa isiumie.Vilevile inafanya kazi ya kusaidia kuubeba uzito wakati wa kutembea, kuinama, kunyoosha viungo au kukimbia.
Zaidi ya asilimia 85 (85%) ya katileji ni maji, na jinsi umri unavyosonga mbele, maji hayo huwa yana kawaida ya kupungua. Na asilimia 15 niprotini.
Tatizo hili lipo zaidi kwenye sehemu ya magoti. Endapo katileji inakuwa ina tatizo, husababisha maumivu makali hasa unapotaka kusimama au kutembea, vile vile kwenye mabega, au nyonga. Pia inaweza sababisha uvimbe (goti au nyonga au bega kuvimba).
Mtu ambaye katileji yake ina tatizo aidha imelika au kutokuwepo kabisa, anatakiwa kupatiwa vitu au virutubishi ambayo vitasaidia kuirekebisha katileji au kuijaza kwa upya.
Virutubishi vifuatavyo vimesaidia wengi wenye tatizo hili:
1. Shark Cartilage
2. Calcium
3. Chitosan

OFISI ZETU ZIPO karibu na huduma zifuatazo:
1. Ofisiya TRA, au karibu na
2. Afya Dispensary, au karibu na
3. Mjasiriamali kwanza, au karibu na
4. Kanisa la Sabato au karibu na
5. Kanisa la Lutherani au karibu na
6. Uwanja wa mpira wa Mwenge.

Anaye hitaji ufafanuzi zaidi tuwasiliane: 0715 594 564 au 0756 594 564

Au tembelea website yetu www.1000ufahamu.com

Sunday 18 August 2013

J'Pili ya Leo;Tuendelee Kuwaombea Wenye Shida Na Tabu,Burudani-Upendo Nkone na Abiudi Misholi.!!!!!

Wapendwa;J'Pili hii tuendelee kuwaweka mikononi mwa BWANA wenye Shida na Tabu.
Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali,Kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.
Neno La Leo;Matendo ya Mitume:16:16-34;






Muendelee kuwa wakati mwema Kila iitwapo Leo.

"Swahili na Waswahili" MUNGU ni mwema.

Saturday 17 August 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Mary Mary-Shackles na Nyingine!!!



Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo...Mary Mary..[Erica na Tina]Mimi Huwa nawakubari/Nawapenda/Wananibambaaa saaana..Pia huwa nafuatilia sana vipindi vyao kwa Tv.
Je vipi wewe? 
Mengi sina,Nisikuchoshee..Pata Burudani Kitu Roho napenda......









"Swahili na Waswahili" Pamoja Daima.

Sunday 11 August 2013

Natumaini J'Pili inaendelea Vyema;Burudani-Hakuna Mungu kama Wewe na Nyingine!!!!!

Natumaini J'Pili Inaendele Vyema..
Ni neno jema kumshukuru BWANA, Na kuliimbia jina lako,Ee Uliye juu.

Neno La Leo:Zaburi:92:1-5;Ee BWANA jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
Wapendwa/Waungwana; Nawatakia kila lililo Jema, Baraka,Amani na Furaha.






"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Wote.