Wednesday 27 April 2011
Monday 25 April 2011
Wazazi wa sasa na Malezi!!!!!!!
Katika pitapita zangu nimekutana na malezi tofauti ya Watoto.Hasa ya kule Nyumbani Afrika/Tanzania na Wanaoishi nje ya Nchi.Watoto wa Nyumbani wengi wao bado wanaheshima kwa wakubwa wote awe mzazi au jilani,kwa Mgeni au Mwenyeji,Akufahamu/kukujua au Asikufahamu/Kukujua.Unyenyekevu na Usikivu. na mengine mengi.
Watoto wa waishio nje ya Afrika/Ng'ambo Wengi wao ni wabinafsi, wanauthubutu wa kukujibu lolote analoweza,anaweza asikusalimie,hawana karibu wala heshima kwa wakubwa,wanamaamuzi zaidi na matakwa yao,Akisema sitaki na hataki,Na baadhi ya wazazi wao wanawasilkiliza zaidi, Hata hawana Aibu kwa matendo ya watoto wala Hofu.
Je Msomaji wewe unamawazo gani katika haya,je ni Mazingira,Maendeleo,Malezi ya kisomi au ni nini kwa hawa wa Nje?.
Na jee hawa wa Nyumbani ni Waoga,Hofu,Kutojiamini au Washamba na wanapitwa na wakati?
Karibuni sana kwa Kuelimishana na Kufundishana .
Saturday 23 April 2011
Mshumaa wangu Uliozimika!!!!!!!!!
Saa,Siku,Wiki,Miezi.Leo Tarehe 23/04/2011 Imetimia Miaka 17.Tangu ulipotutoka Tarehe 23/04/1994.Baba yetu Mpendwa Mzee M.S.KIWINGA.Ulituacha katika Majonzi/Huzuni na kukata tamaa ya maisha.Lakini Mungu ni muweza wa yote ametusaidia na kusimama tena.Tulikupenda lakini Mungu mwenyeezi alikupenda zaidi.Daima hatuwezi kukusahau kwa yote na mengi katika malezi yako.Utakumbukwa daima na Mke wako mpendwa,Watoto,Wajukuu,Ndugu,Jamaa,Marafiki na Majirani.
Shukurani za Dhati ziwaendee Wote walioshiriki nasi katika wakati ule mgumu.Tunaheshimu sana Michango,faraja zenu kwa wakati ule na hata sasa!Pia niwatakie kila la kheri na lililo jema kila siku.
Kwaniaba ya Familiya ya Mzee KIWINGA wa Ilala Sharifu/Shamba,Nasema asanteni sana wote na Tunawapenda.

Monday 18 April 2011
Wednesday 13 April 2011
Watoto naTV!!!!!!!!
Wapendwa vipi watoto na kusogelea TV.Kumekuwa na dhana kwamba watoto hasa wa Afrika wakikaa karibu sana na TV wanaonekana/kuwaita Washamba.Hivi unafikiri kwa nini wanapenda kusogelea TV?.Ili waone vizuri au ndiyo Ushamba? Hata hapa mtoto wangu mmoja tunakosana mara nyingi kwa tabia hiyo!!!!Wewe unamaoni/mawazo gani kuhusiana na hili? Karibu sana tuelimishane.
Monday 11 April 2011
Jikoni leo ni Pilau!!!!!Kinapendwa sana,unafikiri kwa nini???
Kitu Pilau kipo jikoni hapa, harufu yake mpaka mtaa wa tatu!!!!!!
Leo tunakula kwa Kachumbari si Saladi,mimi hupenda kula na Kachumbari!!!!
Kimepakuliwa kitu Pilau bila ya chochote, wengine hupenda hivyo!
Hapa nimeongezea Kachumbari na ndizi mimi hupenda hivyo!
Hicho ni Chakula kinachopendwa na Waswahili wengi, Sherehe/mikusanyiko/Misiba, niliyowahi kushiriki
sikosi kukuta chakula hiki!!
Je wewe unakipenda?na unapenda kuongezea na nini pia kushushia na kinywaji gani?
Karibu sana tukijadili hiki Chakula kwanini unafikifili kinachukua nafasi kubwa?
Asanteni na karibu sana!!!!!!

Thursday 7 April 2011
Maisha ni Kitendawili!!!!!!!!
Huyu amejikunyata na hana furaha kabisa. Kuna kinacho Msibu Maishani!!!.
Huyu naye amejiinamia na rafiki wako pembeni,lakini haitaji maongezi nao.Kuna anachowaza!!!!!!!!
Hii ndiyo dunia yenye mengi Mazuri na Mabaya,yenye Kupendeza na Kuchukiza,yenye Raha na Karaha,yenye Hudhuni na Furaha,yenye Vicheko na Vilio,yenye Kupata na Kukosa, yenye Kutia moyo na Kuvunja moyo.!!!Mmmhhh!!Tunahitaji Upendo na Faraja. Wapendwa nini chanzo cha haya na mwishowake nini?..

Subscribe to:
Posts (Atom)