Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 28 August 2012

Pitapita ya Mswahili Mitaani-Coventry!!!!

                                   Alikutana na Wapiga Ngoma
                                   Ikapigwa na Akacheza
Mswahili mtoto akapiga ngoma nae


Banda la Wazungu, wanauza vitu kutoka kwa Waswahili wa KENYA                            Banda la M'SENEGAL,Ameshona hizo Nguo na hivyo vidude wanatengeneza.

Waungwana ni "Pitapita ya Mswahili Mitaani" Ilikuwa Coventry.  kulikuwa na Mabanda mbalimbali ya Bidhaa , Vyakula na Michezo.

Kwabahati mbaya WaTanzania hatukuwa na Banda.
Nimatumaini yangu siku/wakati mwingine tutakuwa na Banda hata la Mchezo wa Bao,Kijiwe cha Kahawa ile Chunguu yanywewa kwa Vikombe Vidoogo na Kashata.

 Ndugu wa mimi/Blogger Mwenza EMU wa Three.Mmmhhh Ushauri wako Naufanyia Kazi.Hahahaha Eti Ndugu wa mimi ananishauri  nijiunge na Michezo kama Miereka,Judo,Sarakasi ,Kuogelea na.........Uwiiii Kweli umenichoka, Sikuweza Mikundeni itakuwa Michorokoni? hhahaha na Uzee huu mwili umekomaaa.Hahah Usichekeshe walionuna.

Sina Meengi,Unalolote la kuongezea,Maoni,Ushauri?
Pamoja sana "Swahili NA Waswahili"

3 comments:

emuthree said...

Ndugu wa mimi peny nia kuna njia, kwani hiyo michezo hakuna wazee, na una uzee gani weye...umo kabisa, ukuchukua mazoezi, aah, hauna linaloshidikana.
Tupo pamoja ndugu wa mimi nashukuru kwa kutupa vitu hivyo adimu, tungeviona wapi, kama sio hapa kwako!

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki sasa mbona hukulicheza sana hilo lingoma natamani ningekuwa hapa nawe..LOL Aise. Kachiki kama asemavyo ndugu wetu hakuna linaloshindikana ni kuamua tu...mie ntakuunga mukono :-)

Rachel Siwa said...

Haya ndugu wa mimi nimekusikia, nitajitahidi!!!!!!

Kadala nililicheza wee acha tuu, nilisahau kukuwekea video!!haya nimewasikia Ndugu wa mimi.Nanyi mjiotahidi ili tuwakilishe vyema TZ.