Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 30 January 2014

Mswahili Wetu Leo; Tupo Kigoma Tanzania na Fundi Khamiss!!!!
Waungwana,Mswahili Wetu  Leo ;
Tupo Kigoma kwa Fundi Khamiss,Yeye ni Mshonaji na Mbunifuni.

Jee unamtazamo gani na Mafundi Nguo wa [Mitaani/Vibarazani] kwa sasa,Soko lao linazidi kupanda au Linashuka?
Haya tumuunge mkono. Unaweza kuwasiliana naye kupitia:Email;Khamiss@gmail.com,Simu,+255 714481790.
Kuona kazi zake zaidi ingia;http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/

Monday 20 January 2014

Tupo pamoja Wapendwa/Waungwana!!!


Nimatumaini yangu wote hamjambo.Samahani niliadimika/potea kidogo, Ni mbio za hapa na pale katika maisha, Pamoja na yote Tupo salama kabisa na niliwakumbuka Sanaa.Tupo pamoja tena Waungwana, Asanteni.                                                                         Swahili na Waswahili Pamoja Daima.

Monday 9 December 2013

Mheshimiwa January Makamba akihutubia waTanzania DMV‏


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba alipohutubia waTanzania na jamii zao waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika Laurel Maryland Desemba 7, 2013 kwa uratibu wa blog ya VIJIMAMBO


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

Sunday 8 December 2013

Tumalizie J'Pili kwa Upendo na Amani;Burudani-Bonni Mwaitege,Fungua Moyo Wako na Nyingine!!!!

Wapendwa;Tumalizie J'Pili hii kwa Wema,Busara,Hekima,Amani,Unyenyekevu na Upendo..

Malaika wa BWANA hufanya kituo,Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.


Neno La Leo;Zaburi 34:1-12.
Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema;
Heri mtu yule anayemtumaini
.

"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Friday 6 December 2013

RIP Nelson Mandela Dead at 95 - Hanson Baliruno New UgandanDunia yaomboleza kifo cha Mandela;Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Mandela amefariki huko Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza Afrika Kusini kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.

Habari Na;http://www.bbc.co.uk/swahili/

Thursday 5 December 2013

Jikoni Leo;How to Make Mabuyu na Vingine vingi Kutoka kwa-Sheikha Agil

Waungwana ni Jikoni Leo; Tuangalie Mapishi mbalimbali kutoka kwa da'Sheikha..
Mmmhh hakika sikuhizi kama wewe ni mpikaji na unataka kujifunza mapishi tofauti hakuna linaloshindikana.
Usitafute visingizio, Oohh mama nanihii nipikie oohhh sijafundishwa na mama/shangazi/dada,Nyumbani...


Pia kama unakinyaa,Hupendi kula chakula cha mtu usiyemjua/sehemu usiyoiamini usafi wake.Ingia Mitandaoni tuu kila kitu utapata  maelekezo yoote na upike mwenyewe...
Haya TEAM[Timu] Mapishi kazi kwenu............


Shukrani;Sheikha Agil

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.