Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 20 October 2012

Chaguo La Mswahili Leo,Mdumange,Chiwoda,Sindimba,Wamasai na Wagogo.Kiasili Zaidi!!!!!

Waungwana;"Chaguo La Mswahili "Leo kinyumbani/Kiasili Zaidi.
Haya twende sote sasa,Lakini wewe unajua kucheza Ngoma za Asili au Unajua Ndombolo tuu?
Unafikiri ipi Ngoma Nzuri zaidi ya Zote Tanzania?
Ngoma ya kwenu Inaitwaje?
Utamaduni Tanzania unaendelea au Unakufa?...

Mtu Kwao Ungana Nami........"Swahili NA Waswahili" Mkataa  Kwao Mtumwa!!!!!!

Thursday 18 October 2012

Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, Nd Omary Mjenga akutana na Balozi wa Marekani Nchini Siera Leone leo.!!!




Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, Nd Omary Mjenga, akipiga picha ya kumbukumbu Pamoja na Balozi wa Marekani Nchini Sierra Leone Bw Michael Owen, alipomtembelea leo na kufanya mazungumzo naye.

Bwana Omary Mjenga akiagana na Mh. Balozi wa Marekani Nchini Siera Leone baada ya kumaliza mazungumzo.

Balozi Michael Owen, aliwahi kuwa Naibu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania mnamo mwaka 2001 hadi 2004.

Wednesday 17 October 2012

Wanaume na Mitindo ya Nywele!!!!!!!!




Waungwana
"Wanaume na Mitindo" Leo tuangalie Mitindo ya Nywele, ki-Leo/kisasa..haya Wewe unaionaje? Inakubamba/kuipenda au...

 Jee Wanawake mnasemaje baba watoto, Mchumba,Kaka,Mwanao na Mitindio hii, upi umeupenda zaidi?...
Wenyewe Jee kina Kaka,Baba,Mojomba mnatuambiaje?

 Mengi sina Nawasikilizawenzangu....

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima...

Kuona picha zaidi, ingia kwenye Kibaraza chetu kipya;http://mitindoafrica.blogspot.co.uk/


Sunday 14 October 2012

Nawatakia J'Pili Yenye Neema na Tumaini;Burudani-Rebecca Malope - Thank You Lord, Na nyingine nyingii!!!!

Wapendwa;Muwe na J'Pili yenye Neema,Tumaini,Amani na Upendo.
Msiwiwe na mtu cho chote,isipokuwa Kupendana;Kwa maana ampendae mwenzake ametimiza sheria.

Neno la Leo;Warumi:13:8-10 Pendo halimfanyii jirani neno baya;Basi Pendo ndilo utimilifu wa Sheria.

"Swahili NA Waswahili" MUNGU Atubariki Sooteeee.

Saturday 13 October 2012

Chaguo La Mswahili Leo;Mbilia Bel - Nadina.Mario na Franco na Nyingine Nyingiiii!!!!!


Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo""Mambo Ya zamani Kidogo.
 Nakusikiliza wapi unakumbuka na nini kilikuwa kinavaliwa wakati huo? Scania,Mwanameka, Raizoniii,Fundi Nimwagie,Soroo, Vishati Vyembamba na Ulipiga Picha za Studio wewe? hahahah umeshika kiuno kwenye Maua!!!!

Twende Sote sasa ,Mario na Lelieeeehhh Mhhh.....

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday 10 October 2012

Wanawake na Mitindo ya Nywele!!!!





Waungwana;"Wanawake na Mitindo" Leo tuangalie Nywele, jee wewe Mama/Dada unapenda kutengeneza Nywele na unapendelea Mitindo gani? Baba/kaka jee unapenda  Mkeo,Dada na... atengeneze vipi Nywele?

Jee Nywele ndiyo Kivutio kikubwa kwa Wanawake/Kina dada?

Kuona picha zaidi ingia kwenye Kibaraza chetu kipya cha;Mitindo Africa

"Swahili NA Waswahili" Karibuni Wooote!!!!!

Tuesday 9 October 2012

Kisa cha Leo na Mswahili;Emu-Three-Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi;Sehemu ya 5!!!!!


Maua alikuwa katulia kwenye chumba huku akimuomba mungu wake, mwanzoni alikuwa anashindwa hata aombe nini. Akawa anajiuliza je nimuombe Mungu  anisamehe kwa hayanmakosa niliyofanya, lakini akajiuliza kichwani makosa gani, na kama ni makosa mbona ni yeye peke yake ndiye anayeadhibiwa, mbona mwenzake waliyeshirikiana naye , hayupo, je na yeye hastahili kuadhibiwa.

Alipowaza hilo akamkumbuka mwenzake, akakumbuka jinsi walivyokuwa wakiandikiana barua, lakini ghafla akawa hamjibu barua zake tena, hasa pale alipoandika kumuelezea jinsi gani anavyojisikia,na kumwambia anaogoa isije ikawa ni mimba. Ilikuwa barua ya mwisho kumwandikia, na hakuweza kupata jibu, na hata alipoandika nyingine, na nyingine, hakiweza kupata jibu kwa mtu aliyetokea kumpenda sana.

‘Hivi huyu mtu yupo aua kapotolea nchi gani, nakumbuka mara kwa mara anakwenda Arusha kwa mjomba wake, ambaye ni tajiri mmoja wa madini,na nia na lengo lake na yeye ni kujiunga kweney biashara hiyo, lakini kwanini asimwambia, au kumjibu baraua zake,lazima nimtafute tusaidiane hili tatizo’akasema huku akiangalia nje kwa kupitia dirishani.

Akawa bado anawaza ni mambo gani kwasasa anahitajika kumuomba Mungu wake, `Au  nimuombe Munguwangu anisaidie nisiweze kuangukia kwenye mikono ya baba, baba ambaye anataka kuitoa roho yangu, bila makosa, ‘ akasema na alipofikia kuwaza hili akatikisa kichwa na akili yake ikawa anajiuliza ‘Ina maana kweli mimi sio mkosaji,hivi kweli sistahili kuadhibiwa kwa kosa hili?’akatulia na kujarabi kutafakari zaidi. Hapo akakumbuka kauli ya baba yake, ambaye kila mara wakiwa naye alipenda kumuasa nayo;

‘Binti yangu nakupenda sana, na jinsi ninavyo kupenda,  nisingelipenda ukaja kuvunja huu upendo nilio nao juu yako, nakuomba  sana usije ukaniangusha, maana kila mtu hapa kijijini anakuona kama mtoto wa mfano, na mimi huwa natamba kwao kuwa  wewe ni binti mwenye akili, binti mwenye nidhamu, binti ambaye hakuna anayeweza kumfikia kwa jinsi ulivyo hapa kijijini’ilikuwa sauti ya baba yake.

Baba yake kweli alikuwa akimpenda, lakini sio ule upndo wa kumdekeza, kwani akifanay kosa alikuwa akiadhibiwa, mpaka anawaza vibaya kuwa baba yake anataka kumuua, na sio kweli anampenda kiasi hicho. Lakini kaam hajafanay kosa, baba yake alikuwa akribu sana na yeye na kila mwaka wakifanya sherehe za shule anakwenda kushuhudia mtoto wake akipewa zawadi ya kuwa mtoto wa kwanza, na wakirudi nyumbani huchinjiwa kuku kama zawadi maalumu. Na alipofaulu kwenda sekondari, baba alimnunulia zawadi nyingi sana.

`Sasa huyu ndiye binti , binti ambaye baba alikuwa akitamba kuwa ndiye binti wa mfano..’, Maua akajikuta akifuta machozi, akaliangalia tumbo lake, ambalo bado lilikuwa halijaonyesha dalili yoyote kuwa kuna kiumbe ndani , akakunja uso na kuanza kujpiga piga tumboni huku akilaani,i hicho kiumbe kilichopo tumboni,utafikiri ndicho chenye makosa akasema;Inaendele ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

Diary 

Yangu

Yakeeeeeeeee!!!!!

"Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima...