Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 8 September 2012

Siku kama ya Leo da'Sabrina Kiwinga Alizaliwa!!!

Bint Kiwinga kapoziii!!!

         Mhhhh Shangazi langu hiloo,Anatafakari  miaka 2. si mchezo!!
OOhh yahh  ndiyo mimi Sabrina[SAB'K]!!!
Siku kama ya Leo Familia ya Bibi na Bwana H.S.KIWINGA  wa  HOLLAND walipata mtoto wa Kike wakamwita SABRINA!!! da'Sabrina Leo Ametimiza miaka 2.Familia inamshukuru sana MUNGU kwa Yoote,Wanakutakia kila la kheri maishani,Uwe Baraka kwetu na  watu wote.

"Swahili NA Waswahili" Tunakutakia Baraka,Amani, Upendo na Makuzi mema.MUNGU awe nawe kila iitwapo Leo.

Burudani ya Leo mambo ya ki DUTCH tuu, hahahaah wapi shangazi Rabia. watachekea kwao....................

Waungwana;Kama unapenda kutuma picha za Sherehe na Mengineyo tumia.rasca@hotmail.co.uk
Pamoja Daima

Thursday 6 September 2012

Wanawake na Mitindo;Ya Kale ni Dhahabu!!!!!!


Waungwana; Wanawake na mitindo,"Ya Kale ni Dhahabu" Umemuona Mrembo wa zamani?nini Unakumbuka kupitia picha hizi na nini kimekuvutia?
Huo unywele wa kwenye picha ya juu sijui aliweka dawa gani,Zazuu,Alizichoma au........
 Huo Unywele wa kwenye Picha ya chini  hakuna Dawa hapo.

Unalolote unaweza kuongezea katika Picha hizi? Karibu sana.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Yanayoendelea baada ya mauaji ya mwandishi wa channel Ten

habari hii kutoka StarTV. shukraniTangibovu

Tuesday 4 September 2012

Waswahili na Maisha Yao;Leo Tupo IRINGA-Village Schools International-Shamba Darasa!!!!!!!!!



"Waungwana, Waswahili na Maaisha Yao". Leo tupo IRINGA.

Watu wa vijijini wengi wao bado ni wanyeyekevu  kwa Wageni,Shukrani na Kujitoa.
Hapo wakiimba kwa Sauti Taaamu. Pamoja na Mgeni wao,Wakimshuruku MTALAAMU.

Wewe unafikiri kwanini watu wa Vijijini  wengi wao bado wanaukarimu,Shukrani na Unyeyekevu?
 Hawajafunguka,Hawaendi na Wakati,Hawajaumizwa au Mazingira yanachangia?
Jee Vipi watu wa Mjini?Yaani ukiachana na mtu mwaka mmoja  tuu baadhi yao  inabidi Utulize Akili na kuchunguzana upya, kwani Wengi Tabia imebadilika.
Jee  Washalizwa sana/kutapeliwa,Ugumu wa Maisha, Waelevu au Wajanja  Au.......?

 Karibuni sana kwa Maoni/Mawazo,Ushauri na Tuelimishane kwa Amani na Upendo.
[KILIMO KWANZA AU...?]

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Monday 3 September 2012

Tamko La Klabu Ya Waandishi Wa Habari Mkoa Wa Iringa Juu Ya Kifo Cha Daudi Mwangosi!!!



KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC) na waandishi wa habari wote mkoani Iringa na nchini kwa ujumla wamepokea kwa mshutuko na masikitiko makubwa kifo cha Mwenyekiti wa IPC, Daudi Mwangosi.

Mwangosi ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, alifariki jana majira ya saa 10 jioni baada ya kupigwa bomu katika vurugu za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakitawanywa na jeshi la Polisi.


Utata wa nani anahusika na tukio hilo umeendelea kugubika huku jeshi la Polisi likitoa tamko linalodhihirisha dhahiri kwamba wanataka kujiondoa katika kosa hilo kabla uchunguzi haujafanyika.


Katika taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na Polisi hii leo imedai kwamba bomu linalodaiwa kumuuawa mwandishi huyo lilitoka katika kundi la wafuasi wa Chadema, wakati Mwangosi akitafuta msaada wa kujinusuru kwa askari waliokuwepo katika eneo hilo.


Lakini wakati jeshi hilo likitoa taarifa hiyo inayokinzana yenyewe, limeshindwa kueleza ni kwasababu gani bomu lililorushwa kutoka katika kundi la wafuasi hao likamdhuru na kumuua mwandishi huyo pekee yake wakati alikuwa ameshikiliwa na mmoja wa askari wa jeshi hilo baada ya kupigwa virungu alipotaka kujua sababu ya kukamtwa kwa mwandishi mwingine Godfrey Mushi aliyekuwa akipiga picha tukio hilo.


Uchunguzi wa awali wa IPC unapingana kwa asilimia zote na taarifa ya jeshi hilo kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa na baadhi ya waandishi waliokuwepo katika tukio hilo na zile zilizoandikwa na kurushwa na vyombo mbalimbali vya habari toka jana.


Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu zinaonesha kwamba Mwangosi alipigwa kwa virungu kabla ya kulipuliwa na bomu hilo ambalo kwa vyovyote vile muhusika wake mkuu anaweza kuwa jeshi hilo.


Ili taarifa hiyo potofu isiendelee kuugubika umma, IPC imeamua kutoa tamko linalolenga kuviarifu vyombo huru viiingilie kati katika uchunguzi huo.


Na kwa kuzingatia mazingira hayo, IPC kwa kushirikiana na waandishi wote wanaofanya kazi mkoani Iringa, kuanzia leo wanatangaza rasmi kusitisha ushirikiano wa kikazi baina yao na jeshi hilo mpaka pale taarifa au majibu sahihi kutoka kwa vyombo huru vitakavyolifanyia kazi suala hilo yatakapotolewa.


Kazi hizo ni pamoja na kuwataarifu waandishi wa habari kusitisha mara moja kwenda katika Ofisi ya RPC kwa ajili ya kupata taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu yanayotokea kila siku.


Aidha IPC inawataka wanachama au viongozi wake waliokuwa wajumbe wa kamati zozote zile zinazolihusu jeshi hilo ikiwemo ile ya maandalizi ya wiki ya usalama barabarani kujitoa kwenye kamati hizo.


IPC inawaomba waandishi wa habari kushikamana katika kipindi hiki kigumu kwa kuzingatia kwamba yaliyomkuta ndugu yetu Mwangosi yanaelekea kumkuta mwandishi yoyote Yule nchini.


Tukio hilo linadhihirisha jinsi uhuru wa habari na vyombo vya habari unavyozidi kukandamizwa hasa katika kipindi hiki ambacho watanzania kwa ujumla wao wanatakiwa kushiriki kikamilifu kuandika Katiba Mpya wanaoitaka.


Tukio hilo haliwezi kuvumiliwa na kwa msimamo huu, IPC inaomba waandishi wote wawe na wimbo mmoja utakaowezesha muhusika wa mauaji hayo akamatwe na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.


Pamoja na kukamwata kwa muhusika, IPC inataka kuona jeshi la Polisi ambalo kimsingi halipo juu ya sheria linatimiza wajibu wake kwa kuzingatia sheria kama ilivyo kwa taasisi zingine.


Aidha kwa sasa wanahabari mkoa wa Iringa tunatangaza rasmi kusitisha mahusiano yetu na jeshi la polisi kwa kuandika habari za polisi .


Pia tunatambua kuwa wakati Mwangosi akikamatwa alikuwa katika kutimiza wajibu wake kama mwanahabari hivyo hata kama alikosa kwa kufika hapo hukumu yake haikuwa kuuwawa .


Hivyo kutokana na tukio hilo kubwa ambalo halikuwa na chembe ya siasa kwa mwanahabari huyo kwa kuwa hakuwa ni kiongozi wa chama cha Siasa IPC na Chanel Ten kama mwajiri wake na familia tunachukua dhamana ya kusimamia mazishi hayo bila huku tukiviomba vyama vya siasa kutovuruga taswira ya Tasnia hii ambayo kamwe haifungamani ya chama chochote cha Siasa .


Na tunalitaka jeshi la Polisi litoe ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi na za kweli kwa makundi huru yanayoendelea kulichunguza suala hilo.


Kifo cha Mwangosi kimetufanya wanahabari kote nchini kujipanga upya katika kutathimini upya mahusiano yetu na jeshi la polisi .


Mungu ailaze mahali pema roho ya Marehemu Daud Mwangosi. Amin


Francis Godwin

katibu msaidizi IPC

Shukrani;http://www.mjengwablog.com/

Hyena Square - Tanzania.Nani alaumiwe? Pole da'Eliza!!!!!!




Waungwana, Dunia inamambo, haya yote yanasababishwa na nini? jee Nani alaumiwe?.MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Tuelimishane kwa Upendo.

Sunday 2 September 2012

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani-Kinondoni Revival Choir;Mtu wa Nne ,Dini iliyosafi,New Season!!!!



Wapendwa Nawatakia J'Pili njema, Yenye Amani,Upendo na Baraka.
Hata alipotoka kwenda njiani,mtu mmoja akaja mbio,akampigia magoti,akamwuliza,Mwalimu mwema,nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?
Neno la Leo;Marko Mtakatifu:10:17-31.

"Swahili NA Waswahili" MUNGU ATUBARIKI SOOOOTE.