Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 26 July 2011

Kaka Joel Ahitimu!!!!!!!!!

                          Kaka Joel mwenye Furaha.
                                 Duhh sitakuwa nao tena rafiki zangu,hii sasa mbaya kwangu!
                        Dada Jolen akimpongeza kaka.
               Nimeshakuwa mwanakijiji sasa!


Kaka Joel Amehitimu Nursery tayari kwa kuanza/kuingia Reception hapo September.
Joel!! Baba na Mama pamoja na Familia ya Mwasanjala na Shushu,Wanakutakia kila lililo jema katika safari yako ya kutafuta Elimu.


Rafiki[dada] yako kipenzi Tracey anakutakia mema katika masomo yako!


Nasi SwahilinaWaswahili tunakuombea Mungu awe pamoja nawe katika yote.


Mpendwa wewe ulipitia VIDUDU/Nursery?...Je unakumbukumbu gani katika hayo ni Uji,Nyimbo,Kulialia,Ulikutana na watoto Wababe au wewe ndiyo ulikuwa Mbabe!!!!!!


Karibuni sana Waungwana katika Yote!!!!!!!!

Sunday 17 July 2011

Sandra Atimiza miaka 13!!!!!!

                                 Sandra-Neema, akishangaa duh13!

                         Leo natimiza 13,kweli siku hazigandi,kaka Brian akihakikisha.
                    Sandra na Tracey, mwenzangu tumekuwa sasa.
                 Wageni kutoka Birmingham nao walikuwepo.
                               Dada Damari akisimamia watoto wa Swahili Fellowship.
                   Joel,Jolin na Tracey katika poziiiiii.
                     Manjula,Eireen,Shambara na mgeni wao hawakukosa.
                        Miriam na kaka Ebeneza nao walikuwepo.
                                      Sandra &Tracey wakishukuru wageni kwakuwa nao pamoja.
                   Mama na Sandra Tunamalizia.
Familia ya Isaac tuna Mshukuru sana Mungu kwa Yote aliyotutendea,Pia tunawashukuru wote mlio jumuika nasi kwa namna moja au nyingine.Shukrani za pekee kwa Uongozi wa Watoto wetu Coventry Swahili Fellowship,Chini ya Mwenyekiti Da'Mija na msaidizi wake da'Damari.
Mungu awabariki  wote na Tunawapenda sana.

Wednesday 13 July 2011

Bucha Zetu/Utumbo Wenyewe Twalia ......!!!!

Wapendwa hivi kwanini  Bucha nyingi TZ/Bongo, zipo katika mazingira machafu?UTUMBO ndiyo kabisa  Sehemu nyingi zinazouzwa Utumbo ni chafu sana.Kama kwenye maduka kuchafu, Je Machinjioni kutakuwaje?
Na nimesikia[sina uhakika] kwenye kununua uwe makini,Kwani wanaongeza kitu au kufanyia maalifa kwenye Mzani ili kuongezea uzito na kuibia wateja.Kama ulinunu kilo mmoja basi utapata pungufu.


Jewewe Unamawazo gani katika hili, Tuache kula Utumbo,waelimishwe,Wafungiwe au wenyewe tumeshazoea na Vichafu kwani tutapika na kuua Vijidudu?
Utumbo wenyewe twalia Ndizi!!!!!

Saturday 9 July 2011

Mtoto Wetu leo ni Arianna Mbwambo!!!!!!!

                                            dada Arianna katika poziiii
                               Nina mapozi yakutosha.
                                 Nikibeba kipochi jee?

Watoto wa leo na mapozi yao!Wapendwa hivi hawa watoto haya mapozi wanayatoa wapi?
wanayaona kwenye Tv,kwa Wazazi/walezi,kwa rafiki zao au.......

Hata wakubwa nao wana mapozi ,Wengine kunyanyua mguu juu,kushika kiuno,kuweka dole,mikono kifuani na....
zile picha zetu za Studio kushika maua,je mpendwa wewe unazo?.Karibuni sana Waungwana!!!!!

Thursday 7 July 2011

Baba wa Blogger Evarist Chahali Apata Ajali Mbaya!!!!

Mzee Philemon Chahali,Amepeta Ajali mbaya asubuhi ya leo huko Ifakara Tanzania.
Tuungane pamoja katika kipindi hiki kigumu kwake Mzee wetu Chahali na familia yote ya Chahali kwa Maombi,Sala/Dua.

Kaka Chahali pole sana  Mungu akupe nguvu na Tupo pamoja nawe.

Kwamaelezo zaidi unaweza kuyapata.  http://www.chahali.com [Kulikoni Ughaibuni].

Tuesday 5 July 2011

Mama Lwanji Asema, Shikamoo zikizidi ni ukosefu wa Akili!!!

                                 Mwalimu Lilian Lwanji [mke wa muheshimiwa Lwanji].
                                 Muheshimiwa Lwanji akitoa machache na mama pembeni.
                              Mama Lwanji akiwa na binti yake.
Nanukuu;  Hivi mtoto wako ukikutana nae Sebuleni akakuamkia Shikamoo,Muda mfupi baadae unakutana nae chumba cha stoo akakupa Shikamoo, Tena unakukutana nae chumba cha Kulia chakula anakuamkia Shikamoo,Je hiyo itakuwa ni Heshima au ni ukosefu wa Akili?

Maneno hayo  ya Mwalimu Liliana Lwanji, Jee wazazi/walezi manasemaje kuhusu hizo Shikamoo?

Karibuni sana Waungwana!!!!!!

Habari na Picha,zaidi  zinapatikana;kwa, Mohammed Dewji blog!!!!!!Thursday 30 June 2011

Leo Anita Nyotu Atimiza Miaka 5!!!!!!

                                    Dada Anita katika tabasamu.

                               Keki ikikatwa.
                                    Baba akilishwa.
                        Mama akilwalikuwa wanatupata  Live.ishwa, huko Kenya
                                Mama Soph akituwakilisha Wazazi tuliokuwepo.
                             Watoto wasipo onja keki ,hakitaeleweka hapo.
                        Hapa ndipo penyewe kwa Watoto.
                             Hapa tulilegeza mikanda,Nyama choma kwa ugali,wenyewe waita[SIMA].
                            Baba na Mama wakitoa zawadi.
                                         Sandra&Tracey wakitoa chao.
                           Dada Soph&Ruth na  kaka Joseph & Nick walito chao.
                              Saviour & Tiffany walito zawadi yao.
                                 kaka James na wadogo zake nao walitoa yao.
                 Shosho[bibi] na familia huko Kenya tuliungana nao moja kwa moja,Kama unavyoona!!
                      Hali ya hewa leo ilikuwa inaruhusu kucheza nje!
                                Michezo ndiyo kama hiyo ni mwendo wa kuruka.
                                 Picha ya pamoja,hizi baada ya miaka 10 duhh.
                           Bibi ya Nyotu [mke wa Nyotu] Akitoa shukrani kwa waliofanikisha siku hii.
                        Bila kuwasahau Nyumbani Kenya kwa kuwa pamoja.


Nami kwa niaba ya wote tulioshiriki tunasema Ahsante sana.Pia kwa kujali muda,
Tuliambiwa saa 5 mpaka saa 8 mchana, na ilikuwa hivyo, mwenye kwenda kazini haya,
mwenye kuwahi kumpika mumewe [bwana] haya!!!!!!!