Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 2 October 2012

Kisa cha Leo na Mswahili ,Emu-Three;Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi!!!!!!




Katika maisha haya, unaweza ukakutwa na majanga na kufikia hata kukufuru, ukizania wewe tu ndiye unayeonewa, lakini ugumu na matatizo ya kimaisha yapo katika watu wengi, ila ni kwasababu tu hujawahi kusikia au kukutana na watu kama hao. Nalisema hili pale nilipokumbuka kisa cha huyu mwanadada ambaye nilimkuta akiwa kainama upembezoni mwa nyumba huku kashika shavu na michirizi miwili ya machozi ikiwa imeshajichora mashavuni.

Niliingiwa na huruma nilipoona ule ukaaji aliokuwa kaka huyo binti, hasa kwa binti mkubwa kama yule, na ile nguo nyepesi aliyovaa asubuhi kama ile licha ya baridi kali.  Pembeni yake kulikuwa na ndoo ya maji, iliyo tupu. Niliingiwa na moyo wa huruma nikamsogelea kwa tahadhari, kwani dunia hii haina wema, unaweza ukajitia una huruma, na huruma hiyo ikakutokea puani.

Wakati namsogelea kwa tahadhari,nilikumbuka kisa cha jamaa yetu mmoja, ambaye alienda kusota jela, baada ya kujifanya msamarai mwema, kwa kumoenea huruma binti kama huyu. Yeye alimkuta huyo binti  njiani, akiwa analia, na hali aliyomkuta nayo, ilikuwa ya kusikitisha, kwani kama alivyodai, ana siku mbili , kula hali, anachoambulia ni makombo. Yule jamaa yangu alipomuona kwenye hiyo hali akamchukua kwake, lakini  kabla hajatahamaki polisi hawa wapo mlangoni pake.

‘Tumeskilia wewe umemchukua msichana  wa watu, umemficha hapa kwako , yupo wapi?’ akaulizwa.

‘Afande, mimi nimemuona huyu binti njiani, akiwa analia, nikajaribu kumuuliza ana tatizo gani, akawa hanijibu, lakini kwa hali aliyokuwa nayo ilionyesha dhahiri kuwa ana njaa, nikaona nimchukue kwangu, ili anywe chai, halafu atanielekeza kwao, au polisi ikibidi, kwani hali aliyokuwa nayo hata wewe ungelimuonea huruma, inaonyesha wazi ana njaa, na pia mahala kama pale nilipomkuta hapana usalama’akajitetea huyo jamaa yangu.

Wale maaskari wakaangua kicheko, na kusema;
‘Hivi wewe kweli una akili, ukutane na binti wa watu,tena msichana, badala ya kwenda naye polsi unampeleka kwako, kwanza wewe una mke, au ndio ulitaka awe mkeo wa muda baadaye umeshamuharibia maisha yake unamtelekeza!’ akasema yule askari  huku akiangalia huku na kule kama ataona mke wa jamaa yangu huyo.

‘Mimi ninaye mke, na kwasasa hayupo kaenda kwao,  hivi sasa nipo peke yangu, alikwenda kwao kusalimia.’akajitetea jamaa yangu huyo

‘Kwahiyo ukaona uchukue mwanya huo, kutorosha mabinti za watu,wewe huoni hilo ni kosa kubwa, linalinganishwana kuteka nyara. Na wewe hujui kuwa utakuwa na mtoto kama huyo siku za baadaye? 

’akasema yule askari huku akitikisa kichwa na mwenzake akatikisa kichwa kukubaliana naye.

‘Jamani, huyu binti wala sijamtorosha, sivyo kabisa mnavyozania nyie, kwanza yupo hapo ndani anakunywa chai, hebu ingieni mumuhoji wenyewe‘akasema na wale maaskari wakaingia ili kuhakikisha, na wakamkuta yule binti akiwa anakunywa chai, na alipowaona wale maaskari, akakurupuka pale mezani akitaka kukimbia, wakamshika.

‘Wewe ulikuwa wapi muda wote huo, ulikuwa na huyu muhuni, ndiyo yeye anayekuhadaa kila siku ehe, utatumabie vyema?’akasema yule askari huku kamkazia macho yule binti.

Inaendelea....Kusoma zaidi ingia;
http://www.miram3.blogspot.com


Kwa Visa vya kusisimua na kufundisha, Ungana na EMU-Three... Na;
Diary Yangu.
Yakeeeee!!!!!!!!!

"Swahili NA Wswahili" Pamoja Daima

USIKOSE KUANGALIA TANZANIA WORSHIP EXPERIENCE KILA JUMAMOSI SAA 3:30 (9:30 PM) USIKU TBC1...!!!



For more on Tanzania Worship Experience Talent Show like their page on Facebook http://www.facebook.com/TanzaniaWorshipExperience

Monday, 1 October 2012

SUNDAY FABIAN & PRISCA'S ENGAGEMENT PARTY HELD IN LEICESTER UK !!!!!



 Will you????
 Yes I will
 Prisca show's off her engagement ring
 The new couple soon to be Mr & Mrs Sunday
 The couple posing with friends and family
 The bride to be posing with well wishers
 Prisca & her sis-in-law Femmy


Femmy & Sunday
 High Table
 Peter & my bro Abeid in the house
 Happy people dancing
 Watu weweeeeeeee
Mr & Mrs Okoye at the party

"Swahili NA Waswahili" Tunawatakia Maandalizi Mema ya Arusi..

Sunday, 30 September 2012

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani,Bony Mwaitege - Fungua Moyowako,Sisi Sote na Nyingine...!!!

Wapendwa; Nawatakia J'Pili yenye  Furaha,Baraka,Amani,Utuwema,Fadhili na Shukrani.
Basi ndugu zangu,wapendwa wangu,ninaowaonea shauku,Furaha yangu,na taji yangu,hivyo simameni imara katika BWANA.
Neno la Leo;Wafilipi:4;1-23.

"Swahili NA Waswahili" 
Neema ya BWANA YESU kristo na iwe Pamoja na roho Zenu.
AMINA.

Saturday, 29 September 2012

Chaguo La Mswahili Leo;Mchanganyoo-Chaka Demus & Pliers,Shabba ranks na Shaggy!!!!!






Waungwana;
"Chaguo la Mswahili Leo" 

Maneno si Meeengi ,jee wewe ulicheza nyimbo hizi, basi hata kuzisikia?Jee kuna lolote unakumbuka kupitia Mchanganyo wa Leo au Nyimbo moja kati ya hizo?
Tuelezeeee.

Karibu kwa Yoote..Twende Soote sasa....Aaaaaa aaaaaahhh aaahhhh... Mhhhh Sauti imegoma.......kaaaziii kwelikweli ngoja niendelee na Chumvi.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja sana

Friday, 28 September 2012

JESTINA GEORGE BLOG NOMINATED FOR BLOG OF THE YEAR BEFFTA AWARDS 2012...!!!


Jestina-George.Com has been nominated for Blog of the Year at the Black Entertainment Film Fashion Television and Arts Awards (BEFFTA)UK  2012. 
The press and nominees announcement launched in a star-studded event in Mayfair, London hosted by the legendary fashion designer Adebayo Jones. Among the press in attendance were BBC’s Julius Mbaluto, Sixoone Media’s David Mbiyu, New African Woman Magazine editor Regina Jere-Malanda and more. BEFFTA entertainment icon and founder of Sutara Performing Arts academy Lorna Sutara Gayle was also among the special guests on the night. 
BEFFTA UK 2012  online voting will begin on Sunday 7th October and end on Sunday 21st October.
The main award ceremony will take place 27th October.
I would like to thank you all for the endless love & support through my blogging years and let's continue supporting each other.
Much love & God bless.
Jestina George
Owner & Founder 
Swahili NA Waswahili inakutakia mafanikio mema na MUNGU azidi kubariki kazi za mikono yako.......
Pamoja Tunaweza.

Thursday, 27 September 2012

Wanawake na Urembo;Burudani-P-Square - Beautiful Onyinye ft. Rick Ross!!!!







 Waungwana;"Wanawake na Urembo" Urembo ni nini na Jee wewe kwamtazamo wako Mwanamke Mrembo  yukoje?Au wewe nini kinakuvutia kwa Mwanamke?
Sina Meengi ngoja Tusikie Wengine Mnasemaje.

Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.......