Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 14 March 2012

Watoto na Urembo,Wanapaka Shedoooooo!!!!!!

Wazazi/Walezi hapo vipi?Kuna msemo sikuhizi; Aku babu najiremba mie napishana na Uzee!Nao Watoto sasa;Aku bibi nakufuata hukohuko!!Mambo ya kileo hayo, Zamani ulikuwa huruhusiwi kupaka,Wanja,Poda na vipodozi vingine, mpaka siku ya KUOLEWA!!Eti ukipaka  kabla,Siku ya Arusi hautapendeza!!Na walikuwa Wakisuka Nywele Ufunge kilemba mpaka MUMEO kwanza Aone!!''Hizi hadithi mie nazisikia''.Hahahahahha Ohiiii Leo hii nani umfungishe Kilemba?Tena ukienda salon ndiyo unafunga kilemba kama nywele zimeharibika, ukimaliza tuu kilemba kuleeee,Wataanza kuona kina baba/mama John,Juma,Neema,Pili na mnaopishana Njiani, hee dada wewe Umependeza, Umetoka Chicha na..Nani kakusuka dada mmoja anaitwa YASINTA NGONYANI!!!Muwe na Wakati Mwema Waungwa, Karibu Sana sana.

Tuesday, 13 March 2012

Wanawake na Mitindo ya Nywele,Pata na kideo Jinsi ya kuweka Nywele Bandia!!!!!!

Haya Waungwana Mitindo ya Nywele kwa Wanawake, Mmmh lakini kwa sasa hakuna cha Wanaume wala cha Wanawake, kila mmoja  anajaribu kuingilia Mitindo ya Jinsia nyingine,Au labda mimi ndiyo sielewi, kwamba hakuna Mitindo ya Wanawake na Wanaume Wote ni Sawa!!!!Wewe uliyepita hapa unaonaje?
Swali ;Wanaume wengi Wanaofanya Kazi  SALON zA Wanawake Wengi wao/Baadhi yao ni MASHOGA?

Sunday, 11 March 2012

Nawatakia j'Pili Njema Wapendwa,Burudani,Rose Muhando-Tamalaki''Na nyingine Mpya!!



Mzee,kwa Gayo mpenzi,nimpendaye katika kweli.2Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo.Neno linapatikana;WARAKA WA TATU WA  YOHANA:soma 1-13.15;Amani kwako,Rafiki zetu wakusalimu.Wasalimu hao rafiki zetu,kila mtu kwa jina lake.Mbarikiwe sana!!!mimi nabarikiwa sana na nyimbo nyingi kupitia hapa kwa Kaka yangu Matondo.http://nyimbozadini.blogspot.com/

Saturday, 10 March 2012

Wanawake na Mitindo-da'Levina na Rafiki zake!! Chaguo la Mswahili-Yvonne Chaka - Mamaland na Umgombothi


                                         Da'Levina[Aliye shika kiuno] na Rafiki katika poziii
                                         Dadazzz mmependeza mnoo,Asanteni sana  kwa kutuwakilisha.Siku ya Wanawake ,Wao walijumuika na wenzao kwa Shamim.Duuhh kivazi cha kanga kikitengenezwa, kinapendeza haswaaa.Wanawatakia Wanawake Woote Duniani ,Baraka, Amani,Upendo na Umoja.WANAWAKE JUU!!!

Thursday, 8 March 2012

Nawatakia kheri na Baraka, Wanawake wote!!Burudani,Vicky Kamata - Wanawake Maendeleo


Namshukuru Mungu kwa kuniumba  Mwanamke,Najivunia kuwa Mwanamke!Nawatakia Wanawake wenzangu woote Kheri,Baraka,Upendo,Utuwema,Fadhili na Yootee yanayostahili.Wanawake Tujiheshimu na Kuheshimu Wengine,Tupendane na Tujipende,Tushirikianae na Kuelimishana,Tusamehe nasi Tusamehewe.Wanawake wa Zamani hata akiwa mama wa Nyumbani lakini alikuwa anakitu kidogo cha kufanya,kama, Kusuka ukili,Kufuma vitambaa,Biashara ndogo ndogo,Kushona na mambo meengi ili kuongezea kipato.Hata Wanawake wa sasa hatuja chelewa, kama hakuna Ajira basi Tunaweza Kusjishughulisha,hakuna asiyeweza kufanya lolote na hakuna aliye zaliwa anaweza.Japo masoko yamekuwa magumu,lakini Tusikate Tamaa.Pale tunapokwama tusisite kutafuta Ushauri na maelekezo, Kwani kuuliza si Ujinga.Mungu awabariki sana,WANAWAKE JUUU!!!!!