Katika pitapita zangu nimekutana na malezi tofauti ya Watoto.Hasa ya kule Nyumbani Afrika/Tanzania na Wanaoishi nje ya Nchi.Watoto wa Nyumbani wengi wao bado wanaheshima kwa wakubwa wote awe mzazi au jilani,kwa Mgeni au Mwenyeji,Akufahamu/kukujua au Asikufahamu/Kukujua.Unyenyekevu na Usikivu. na mengine mengi.
Watoto wa waishio nje ya Afrika/Ng'ambo Wengi wao ni wabinafsi, wanauthubutu wa kukujibu lolote analoweza,anaweza asikusalimie,hawana karibu wala heshima kwa wakubwa,wanamaamuzi zaidi na matakwa yao,Akisema sitaki na hataki,Na baadhi ya wazazi wao wanawasilkiliza zaidi, Hata hawana Aibu kwa matendo ya watoto wala Hofu.
Je Msomaji wewe unamawazo gani katika haya,je ni Mazingira,Maendeleo,Malezi ya kisomi au ni nini kwa hawa wa Nje?.
Na jee hawa wa Nyumbani ni Waoga,Hofu,Kutojiamini au Washamba na wanapitwa na wakati?
Karibuni sana kwa Kuelimishana na Kufundishana .