Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Imani.. Show all posts
Showing posts with label Imani.. Show all posts

Friday 14 April 2017

Nawatakia Ijumaa Kuu Njema na Maandalizi mema ya Pasaka;Burudani-Kwaya Ya Vijana KKKT Mabibo Mateso Ya Bwana Yesu,Azania Front - Kweli ni Huzuni..


Wapendwa/Waungwana nawatakia maandalizi mema ya Pasaka...
Ikawe yenye kheri na Amani,Furaha na Upendo.


         Mpendwa nini umepanga Pasaka hii? Kula na wapendwa Ndugu,Jamaa,Marafiki,Wazee,Wasiojiweza? au Utakuwa wapi?





Mimi baada ya Ibada nitakuwa Kazini ikimpendeza Mungu..!!
Muwe na wakati mwema..
Nawapenda.

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Sunday 19 April 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA MKUTANO MKUU WA WASABATO WAISHIO NCHINI MAREKANI




Mchungaji Wilbert Nfubhusa akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu wa Wasababto waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland. Kulia ni Michael Mwasumbi akitafsiri mahubiri kwa lugha ya Kiingereza.Mkutano huu umehudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo wengine kutoka Tanzania.
 Mhe. Liberata Mulamula. Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiushukuru uongozi wa Wasabato nchini Marekani kwa kuweza kufanikisha mkutano wao na kuweza kumleta mchungaji Wilbert Nfubhusa na kuelezea amefurahishwa kwa makaribisho mazuri na kuwatakia mkutano mwema huku akiomba Mwenye Mungu aushushie baraka zake.


Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mdogo wake  Joycelyne Rutageruka ambaye amekuja kumtembelea Mhe. Balozi toka nyumbani Tanzania nae akitoa neno kwenye mkutano mkuu wa Wasabato wa Watanzania waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland.  


Nchungaji Herry Mhando akifanya mamombi maalum kabla ya kumkaribisha mchungaji Wilbert Nfubhusa kutoa mahubiri,


Mshereheshaji Magoma akifafanua jambo


Mhahubiri yakiendelea
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi