Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 13 July 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AWAAGA TAMCO RASMI, ASEMA UMOJA NA MSHIKAMANO WAO NI MFANO WA KUIGWA NA JUMUIYA ZINGINENa Mwandishi wetu, Washington, DC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula
 siku ya Jumapili July 12, 2014 alijumuika na wanajumuiya ya
Kiislam ya DMV (TAMCO) katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na
jumuiya hiyo na kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.Katika hotuba yake. Mhe. Liberata Mulamula  aliwakuwakumbusha
alipokuja kwa mara ya kwanza kulitumikia Taifa kama Balozi wa Tanzania
nchini Marekani , Jumuiya hiyo ndio iliyomkaribisha kwa mara ya kwanza
hapa DMV na leo nimerudi tena kuagana nanyi rasmi. Mhe. Liberata
Mulamula aliwashukuru TAMCO kwa ushirikiano na mshikamano wao na
kuzitaka Jumuiya zingine za Watanzania ziige mfano wao kwani TAMCO ni
jumiya ya Kiislam iliyoimara, isiyotetereka na yenye uongozi makini.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliushukuru uongozi wa TAMCO kwa
kumkaribisha aje azungumze na Watanzania wanajumuiya ya TAMCO na
kutumia fulsa hiyo kuwaaga rasmi.


Uongozi wa TAMCO ulimuzawadia Mhe. Balozi Liberata Mulamula zawadi na
yeye kutoa mchango wake wa mwaka kwa jumuiya hiyo inayo wakubali
Watanzania wote bila kubagua rangi, kabila wala dini.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Watanzania DMV
(TAMCO)Ustadh Ally Mohamed akimlaki Mhe. Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulaula mara tu
alipowasili kwenye ukumbi wa park iliyopo Silver Spring, Maryland
nchini Marekani alipokuja yeye Mhe. Balozi akiambatana na mumewe Eng.
George Mulamula (hayupo pichani) na mwanae Alvin Mulamula (kulia)
kujumuika na wanajumuiya hao katika futari ya pamoja na kutumia futari
hiyo kuwaaga rasmi. Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo
Blog.

 Mtunza fedha msaidizi wa TAMCO. Bi. Asha Hariz(kushotao)
akiongozana na Mhe. Liberata Mulamula kuelekea ukumbini siku ya
Jumapili July 12, 2015 siku Mhe. Balozi alipopata mwaliko wa Jumuiya
hiyo wa kufuturu pamoja na kuwaaga rasmi.


Mwenyekiti wa TAMCO ustadh Ally Mohamed akiongea machache na baadae
kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea na
wanajumuiya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Wanajumuiya wa TAMCO na
kuwaaga rasmi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akikabidhi mchango wake wa TAMCO wa
mwaka kwa mtunza fedha msaidizi ustadh Shamis Abdullah.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha
msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mtunza fedha
msaidizi wa TAMCO bi. Asha Hariz.Picha ya pamoja

No comments: