Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 10 February 2012

Harambee ya Msiba wa Mtanzania Mwenzetu,Washington DC.Kutoa ni Moyo!!!

Marehemu Christavina Kusaga Cryor
Familia ya Kusaga inawaomba watanzania wote walioko Marekani na hasa eneo la Washington DC na vitongoji vyake kushirikiana nao katika harambee (fundraising) ili kupata pesa ya mazishi ya mtanzania mwenzetu Christavina Kusaga Cryor aliyefariki February 7, 2012 kwa sarakani ya utumbo.

Marehemu alikuwa akiishi Landover, MD. Ameacha mume na watoto wawili- mvulana wa miaka 4 na msichana wa miaka 2. Alikuwa akisumbuliwa na cancer ya utumbo.

Tafadhali fika tushirikiane kusaidia mume wake na watoto na familia wamzike mpendwa wao. Jumla ya gharama za mazishi ni $11,000, na mpaka sasa tuna $3,000. Tunashukuru kwa waliokwisha saidia.

Harambee itakuwa Jumapili February 12, 2012, kuanzia saa 8.30 mchana (2.30pm).

Anuani ni: 3621 Campus Drive, College Park, MD 20740.

Kwa wale wa mbali au wasioweza kuhudhuria tafadhali tusaidie mchango wako kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing # 255071981. Jina la Account ni Lavorn Cryor. Tafadhali eneza habari hii kwa ndugu na marafiki wote. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu katika wakati huu mgumu.

Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile (240.938.3177); Teddy (301.254.4169); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au Rebecca (202.580.4648).

M/Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen

No comments: