Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 4 August 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Zekaria 11...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!


Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka Misri. Huo ulikuwa mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni juu ya Israeli, katika mwezi wa Zifu, yaani mwezi wa pili.

1 Wafalme 6:1

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Nyumba hiyo ambayo mfalme Solomoni alimjengea Mwenyezi-Mungu ilikuwa na urefu wa mita 27, upana wa mita 9, na kimo cha mita 13.5. Ukumbi wa sebule ya nyumba ulikuwa na upana wa mita 4.5 toka upande mmoja wa nyumba mpaka upande mwingine. Na kina chake mbele ya hiyo nyumba kilikuwa mita 9.

1 Wafalme 6:2-3

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...



Aliiwekea nyumba hiyo madirisha mapana kwa ndani na membamba kwa nje. Pia alijenga nguzo kuzunguka, ili kutegemeza ukuta wa nje; akatengeneza na vyumba vya pembeni kila upande.

1 Wafalme 6:4-5

Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.



Kuanguka kwa wenye nguvu 
1Fungua milango yako, ewe Lebanoni ili moto uiteketeze mierezi yako! 2Ombolezeni, enyi misunobari, kwa kuwa mierezi imeteketea. Miti hiyo mitukufu imeharibiwa! Enyi mialoni ya Bashani, ombolezeni, kwa kuwa msitu mnene umekatwa! 3Sikia maombolezo ya watawala! Fahari yao imeharibiwa! Sikia ngurumo za simba! Pori la mto Yordani limeharibiwa! Wachungaji wawili 4Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, alisema hivi: “Jifanye mchungaji wa kondoo waendao kuchinjwa. 5Wanunuzi wao wanawachinja lakini hawaadhibiwi; na wauzaji wao wanasema, ‘Na ashukuriwe Mwenyezi-Mungu! Sasa tumetajirika’. Hata wachungaji wenyewe hawawaonei huruma. 6Mimi Mwenyezi-Mungu nasema kwamba, sitawahurumia tena wakazi wa dunia. Nitamwacha kila mtu mikononi mwa mwenzake, na kila raia mikononi mwa mfalme wake. Nao wataiangamiza dunia, nami sitamwokoa yeyote mikononi mwao.” 7Basi, nikawa mchungaji wa kondoo waliokuwa wanakwenda kuchinjwa, kwani niliajiriwa na wale waliofanya biashara ya kondoo. Nikachukua fimbo mbili: Moja nikaiita “Fadhili,” na nyingine nikaiita “Umoja,” nikaenda kuchunga kondoo. 8Kwa muda wa mwezi mmoja, nikaua wachungaji watatu wabaya. Tena uvumilivu wangu kwa kondoo ukaniishia, nao kwa upande wao, wakanichukia. 9Basi, nikawaambia, “Sitakuwa mchungaji wenu tena. Atakayekufa na afe! Atakayeangamia na aangamie! Na wale watakaobaki na watafunane wao kwa wao.” 10Nikaichukua ile fimbo yangu niliyoiita “Fadhili,” nikaivunja, kuonesha kwamba agano alilofanya Mwenyezi-Mungu na watu wake limevunjwa. 11Na agano hilo likavunjwa siku hiyohiyo. Wale wafanyabiashara ya kondoo waliokuwa wananiangalia, wakajua kwamba Mwenyezi-Mungu alikuwa ameongea kwa matendo yangu. 12Kisha nikawaambia, “Kama mnaona kuwa ni sawa, nilipeni ujira wangu; lakini kama mnaona sivyo, basi kaeni nao.” Basi, wakanipimia vipande thelathini vya fedha mshahara wangu. 13Kisha Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Ziweke katika hazina ya hekalu.”11:13 Ziweke … hekalu: Makala ya Kiebrania: Mpe mfinyanzi. Mshahara huo ulikuwa ni malipo halali kwa kazi yangu. Hivyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha, nikazitia katika hazina ya hekalu la Mwenyezi-Mungu. 14Kisha nikaivunja ile fimbo yangu ya pili niliyoiita “Umoja;” na hivyo nikauvunja umoja kati ya Yuda na Israeli. 15Mwenyezi-Mungu akaniambia tena, “Jifanye tena mchungaji, lakini safari hii uwe kama mchungaji mbaya! 16Maana nitaleta nchini mchungaji asiyemjali kondoo anayeangamia, au kumtafuta kondoo anayetangatanga, au kumtibu aliyejeruhiwa wala kumlisha aliye hai: Bali atakula wale kondoo wanono, hata kwato zao. 17“Ole wake mchungaji mbaya, ambaye anawaacha kondoo wake! Upanga na uukate mkono wake, na jicho lake la kulia na ling'olewe! Mkono wake na udhoofike, jicho lake la kulia na lipofuke.”


Zekaria11;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe

Monday 3 August 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Zekaria 10...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki/Mwezi mwingine tena Mungu wetu ametuchagua

na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!



Kisha, nikamwona malaika mmoja amesimama katika jua. Akapaza sauti na kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juu angani, “Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuu ya Mungu. Njoni mkaitafune miili ya wafalme, ya majemadari, ya watu wenye nguvu, ya farasi na wapandafarasi wao; njoni mkaitafune miili ya watu wote: Walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa.”

Ufunuo 19:17-18

Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona

Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona....

Kisha, nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi pamoja na jeshi lake.

Ufunuo 19:19

Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu

Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotosha wale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambao walikuwa wameiabudu sanamu yake). Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti. Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wote wakajishibisha kwa nyama zao.

Ufunuo 19:20-21

Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimamie Neno lako nalo likawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.
Mungu anaahidi ukombozi 
1Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika. Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua; ndiye awapaye watu mvua za rasharasha, na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote. 2Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu, na waaguzi wao wanaagua uongo; watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu, na kuwapa watu faraja tupu. Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo; wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji. 3Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji, nami nitawaadhibu hao viongozi.10:3 viongozi: Kiebrania: Beberu. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda. Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita. 4Kwa ukoo wa Yuda kutatokea: Watawala wa kila namna, viongozi imara kama jiwe kuu la msingi, walio thabiti kama kigingi cha hema, wenye nguvu kama upinde wa vita. 5Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitani watawakanyaga maadui zao katika tope njiani. Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao; nao watawaaibisha hata wapandafarasi. 6“Watu wa Yuda nitawaimarisha; nitawaokoa wazawa wa Yosefu. Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma, nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao. 7Watu wa Efraimu watakuwa kama mashujaa vitani; watajaa furaha kama waliokunywa divai. Watoto wao wataona hayo na kufurahi, watajaa furaha mioyoni kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu. 8“Nitawaita watu wangu na kuwakusanya pamoja; nimekusudia kuwakomboa, nao watakuwa wengi kama hapo awali. 9Japo niliwatawanya kati ya mataifa, hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo. Nao pamoja na watoto wao wataishi na kurudi majumbani mwao. 10Nitawarudisha kutoka nchini Misri, nitawakusanya kutoka Ashuru; nitawaleta nchini Gileadi na Lebanoni, nao watajaa kila mahali nchini. 11Watapitia katika bahari ya mateso,10:11 mateso: Au Misri. nami nitayapiga mawimbi yake, na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitavunjwa na nguvu za Misri zitatoweka. 12Mimi nitawaimarisha watu wangu, nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”


Zekaria10;1-12

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe

Friday 31 July 2020

Kikombe Cha Asubuhi; Zekaria 9...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!


Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwa yamepanda farasi weupe na yamevaa mavazi ya kitani, meupe na safi.

Ufunuo 19:14

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako,
Tukijinyenyekeza,tukijiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunamomba utusamehe dhambi zetu
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
 ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea

Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwa upanga huo atawashinda watu wa mataifa. Yeye ndiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu ya Mungu Mwenye Nguvu.

Ufunuo 19:15

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....


Juu ya vazi lake, na juu ya paja lake, alikuwa ameandikwa jina: “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”

Ufunuo 19:16

Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...

Nawapenda.

Hukumu juu ya mataifa jirani
1Kauli ya Mwenyezi-Mungu:
Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadraki
bali pia dhidi ya Damasko.
Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu,
kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli.
2Hali kadhalika mji wa Hamathi unaopakana na Hadraki;
na hata miji ya Tiro na Sidoni
ingawaje yajiona kuwa na hekima sana.
3Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa,
umejirundikia fedha kama vumbi,
na dhahabu kama takataka barabarani.
4Lakini Bwana ataichukua mali yake yote,
utajiri wake atautumbukiza baharini,
na kuuteketeza mji huo kwa moto.
5Mji wa Ashkeloni utaona hayo na kuogopa,
nao mji wa Gaza utagaagaa kwa uchungu;
hata Ekroni, maana tumaini lake litatoweka.
Mji wa Gaza utapoteza mfalme wake,
nao Ashkeloni hautakaliwa na watu.
6Mji wa Ashdodi utakaliwa na machotara.
Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Kiburi cha Filistia nitakikomesha.
7Nitawakomesha kula nyama yenye damu,
na chakula ambacho ni chukizo.
Mabaki watakuwa mali yangu,
kama ukoo mmoja katika Yuda.
Watu wa Ekroni watakuwa kama Wayebusi.
8Mimi mwenyewe nitailinda nchi yangu,
nitazuia majeshi yasipitepite humo.
Hakuna mtu atakayewadhulumu tena watu wangu,
maana, kwa macho yangu mwenyewe,
nimeona jinsi walivyoteseka.”
Mfalme wa amani
9Shangilieni sana enyi watu wa Siyoni!
Paazeni sauti, enyi watu wa Yerusalemu!
Tazama, mfalme wenu anawajieni,
anakuja kwa shangwe na ushindi!
Ni mpole, amepanda punda,
mwanapunda, mtoto wa punda.
10Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu,
na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu;
pinde za vita zitavunjiliwa mbali.
Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa;
utawala wake utaenea toka bahari hata bahari,
toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.
Kurudishwa kwa watu wa Mungu
11Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Kwa sababu ya agano langu nanyi,
agano lililothibitishwa kwa damu,
nitawakomboa wafungwa wenu
walio kama wamefungwa katika shimo tupu.
12Enyi wafungwa wenye tumaini;
rudini kwenye ngome yenu.
Sasa mimi ninawatangazieni:
Nitawarudishieni mema maradufu.
13Yuda nitamtumia kama uta wangu;
Efraimu nimemfanya mshale wangu.
Ee Siyoni! Watu wako nitawatumia kama upanga
kuwashambulia watu wa Ugiriki;
watakuwa kama upanga wa shujaa.”
14Mwenyezi-Mungu atawatokea watu wake;
atafyatua mishale yake kama umeme.
Bwana Mwenyezi-Mungu atapiga tarumbeta;
atafika pamoja na kimbunga cha kusini.
15Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawalinda watu wake,
nao watawaangamiza maadui zao.
Watapiga kelele vitani kama walevi
wataimwaga damu ya maadui zao.
Itatiririka kama damu ya tambiko
iliyomiminwa madhabahuni kutoka bakulini.9:15 maana ya aya hii katika Kiebrania si dhahiri.
16Wakati huo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, atawaokoa,
maana wao ni kundi lake;
nao watang'aa katika nchi yake
kama mawe ya thamani katika taji.
17Jinsi gani uzuri na urembo wake ulivyo!
Wavulana na wasichana watanawiri
kwa wingi wa nafaka na divai mpya.

Zekaria9;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe