Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 7 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..9...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu.! Baba wambinguni Tunakushukuru na kukusifu..
Asante kwa wema na fadhili zako,
Asante kwa ulinzi wako wakati wote na kutuamsha salama..

Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii.
Tunakuja mbele zako Mfamle wa Amani tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mokononi mwako Mungu wetu..
Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mungu wetu....kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Utuepushe katika majaribu,Utuokoe na yule mwovu na kazi zake Baba wa Mbinguni..
Ututakase na kutufunika kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Utupe moyo wenye Hekima,Busara,Amani ya moyo,Upendo wa kweli,kuchukuliana/kuvumiliana,kusameheana na Upole Kiasi..
Tupate kujitambua/kutambua..
Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Baba wa Mbinguni tunaiweka siku hii mikononi mwako,Ukatubariki,ukatamalaki maishani mwetu na ukatuatamie..
Ikawe siku njema na yenye kukupendeza wewe..
Ukabariki Kazi zetu,Biashara,Masomo,vilaji/vinywaji,kuingia/kutoka kwetu,vyombo vya usafiri na tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Jehovah..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Tazama wenyeshida/tabu,wanaopitia magumu/majarubu mbalimbali,waliokatika vifungo mbalimbali,wagonjwa,wafiwa ukawe mfariji wao..Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye na kuwaoko,ukaonekane kwenye mahitaji yao,wakapate kupona kimwili na kiroho pia..


Ee Mungu wetu tunaweka Nchi hii tunayoishi mikononi mwako Ukaibariki na kuwabariki watu wote tunaoshia humu,Ukatusamehe pale tulipokwenda kinyume,pale tulipokuasi na kufuata mambo yetu wenyewe..Ee Baba ukasikie kulia kwetu,ukasikie maombi yetu,ukasimame nasi katika yote,Ukatuepushe na Udini/ukabila,chuki na hasira,ukawabariki Viongozi wetu wa KIROHO Baba wa Mbinguni ukawape macho ya rohoni, ukabariki Familia zao pia,Ukawabariki na wanaotuongoza Baba wa Mbinguni wakatuongoze katika haki na kweli..
 Tuungane pamoja kuombea Amani kwenye Taifa hili,Mungu wetu ukaonekane na kutawala Milele...

Ee Mungu wetu tunaiweka Tanzania mikononi mwako,Amani ya kweli,Upendo wa Kweli,Ukaibariki na kuwabariki watu wake popote walipo,walio ndani ya Nchi na walio nje kwa sababu ya kusoma,kwa sababu ya kutafuta maisha,waliokatika matibabu na mengine yote Mfalme wa Amani ukatawale maisha yao, Ukatuongoze vyema na ukatupe mwanga katika maisha yetu,ukaonekane Mungu wetu,Kuna sababu ya kuwa Wa Tanzania haijalishi watu wanaishi wapi,wako wapi Mungu wetu yupo nasi..
Mungu wetu tunaiweka Afrika yote yote mikononi mwako waafrika popote walipo Baraka na Amani ziwafuate..
Mungu wetu tunaiweka Dunia hii mikononi mwako wewe ukawe mtawala mkuu na ukawabariki na kuwaongoza wote wanaotuongoza, Kiroho na kidunia wakatuongoze vyema kwa misingi yako Mungu wetu..

Wapendwa/waungwana tusikome kuombea Mtaifa yetu,watu wetu,Viongozi wetu wa KIROHO na wakimataifa/kidunia..
Tusichoke kuombeana mema hata kama tulikoseana tuombane msamaha na kuendela vyema katika maisha yetu,Muombee mwenzio mema,Ombea watoto wa wenzio,Tuombee Nchi tunazoishi na tulipotokea/zaliwa na watu wake Kwani Amani ikitawala hapo ulipo au ulipotokea/zaliwa nawe utakuwa na Amani ya moyo..
Ombea kazi,Karama za wengine walizobarikiwa na Mungu nawe una zako pia wengnine hawana hizo,Mungu wetu ni muweza wa yote..
Ombea adui yako,Samehe kama Mungu anavyotusamehe..
Tuachane na wivu,visasi na kukwamishana utachelewesha tuu kwani vinamwisho Mungu akimbariki mtu amembariki..

Mungu akatulinde na mabaya yote yaliyonenwa,yaliyotendwa kwa sababu yetu..Mungu akabariki vinywa vyetu na kutusamehe..tulipowanenea mabaya wengine,Tulipoadhibu,Tulipo hukumu na kusababisha makwazo kwa wengine..
Mungu akatubariki katika yote na tukajue kweli..

“Katika mwaka Dario mwana wa Ahasuero, Mmedi, alipoanza kutawala juu ya milki ya Wakaldayo, mimi Danieli nilikuwa nikivisoma kwa makini vitabu vitakatifu, na humo nikaelewa maana ya jambo lile Mwenyezi-Mungu alilomfahamisha nabii Yeremia kuhusu ile miaka sabini, muda ambao utahusika na kuharibiwa kwa Yerusalemu. Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, kwa moyo, nikimtolea dua pamoja na kufunga, nikavaa vazi la gunia na kuketi kwenye majivu. Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuungama, nikisema: “Ee Bwana, wewe ni Mungu mkuu na wa kuogofya. Wewe ni mwaminifu kwa agano lako na unawafadhili wakupendao na kuzitii amri zako. Tumetenda dhambi, tumekosa, tumetenda maovu na kukuasi. Tumezikiuka amri zako na kanuni zako. Hatukuwasikiliza watumishi wako manabii, ambao kwa jina lako waliongea na wafalme wetu, wakuu wetu, wazee wetu na taifa letu lote. Kwako, ee Bwana, kuna uadilifu, lakini sisi daima tumejaa aibu. Jambo hili ni kweli kwetu sote tuishio Yudea, wakazi wa mji wa Yerusalemu na Waisraeli wote ambao umewatawanya katika nchi za mbali na za karibu kwa sababu ya kukosa uaminifu kwako. Aibu, ee Bwana, ni juu yetu, wafalme wetu, wakuu wetu na wazee wetu, kwa sababu tumekukosea. Wewe, Bwana Mungu wetu, una huruma na msamaha, ingawa sisi tumekuasi. Tulikataa kukusikiliza, ee Bwana, Mungu wetu; hatukuishi kulingana na sheria zako ulizotupa kwa njia ya watumishi wako manabii. Waisraeli wote wameiasi sheria yako, wamekuacha wakakataa kukutii. Kwa sababu tumekukosea, tumemwagiwa laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Mose, mtumishi wako. Umethibitisha yale uliyosema utatutenda sisi pamoja na watawala wetu kwa kuuadhibu mji wa Yerusalemu vikali zaidi ya mji mwingine wowote duniani. Umetuadhibu kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, lakini mpaka sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hatukuomba msamaha wako kwa kuziacha dhambi zetu na kutafakari uaminifu wako. Kwa hiyo, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ulikuwa tayari kutuadhibu, na ukafanya hivyo, kwa kuwa daima unafanya yaliyo ya haki, nasi hatukukusikiliza. “Na sasa ee Bwana, Mungu wetu, uliyewatoa watu wako nchini Misri kwa nguvu yako kuu na kulifanya jina lako litukuke mpaka sasa, tunasema kwamba tumetenda dhambi; tumefanya maovu. Ee Bwana, kwa kadiri ya matendo yako ya haki usiukasirikie wala kuughadhibikia mji wako wa Yerusalemu, mlima wako mtakatifu. Watu wote wa nchi za jirani wanaudharau mji wa Yerusalemu na watu wako, kwa sababu ya dhambi zetu na maovu waliyotenda wazee wetu. Kwa hiyo, ee Mungu, isikilize sala yangu na maombi yangu mimi mtumishi wako. Kwa hisani yako, uifadhili tena maskani yako iliyoharibiwa. Tega sikio, ee Mungu wangu; angalia uone taabu tulizo nazo na jinsi unavyotaabika huo mji uitwao kwa jina lako. Tunakutolea maombi yetu si kwa sababu tumetenda haki, bali kwa sababu wewe una huruma nyingi. Ee Mwenyezi-Mungu, utusikie; utusamehe ee Mwenyezi-Mungu. Ee Mwenyezi-Mungu, kwa hisani yako utusikie na kuchukua hatua, wala usikawie, ee Mungu wangu, kwa ajili ya mji huu na watu hawa wanaoitwa kwa jina lako!
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..
Tunayaweka haya yote  mikononi mwako Mungu wetu..
Kwakua Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wote mnaotembelea hapa..
sina neno zuri lakusema..zaidi ya kuwaombea
Baraka na Amani zikamiminike katika maisha yenu..
Nawapenda.

Aroni anatoa sadaka

1Siku ya nane baada ya siku saba za kuwekwa wakfu, Mose akamwita Aroni na wanawe pamoja na wazee wa Israeli. 2Mose akamwambia Aroni, “Chukua ndama dume kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; wanyama wote wasiwe na dosari. Kisha watoe sadaka mbele ya Mwenyezi-Mungu. 3Waambie Waisraeli wachukue beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na ndama mmoja na mwanakondoo mmoja wote wa umri wa mwaka mmoja na wasio na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, 4fahali mmoja na kondoo dume mmoja kwa ajili ya sadaka za amani, wakamtolee Mwenyezi-Mungu pamoja na sadaka ya nafaka iliyochanganywa na mafuta kwa maana leo Mwenyezi-Mungu atawatokea.”
5Waisraeli wakaleta vyote hivyo mbele ya hema la mkutano kama Mose alivyowaamuru na jumuiya yote ikaenda kusimama mbele ya Mwenyezi-Mungu. 6Mose akawaambia, “Hili ndilo jambo ambalo Mwenyezi-Mungu aliwaamuru mlifanye ili utukufu wake uonekane kwenu.” 7Hapo Mose akamwambia Aroni, “Nenda kwenye madhabahu, utolee hapo sadaka yako ya kuondoa dhambi na sadaka ya kuteketezwa na kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili yako na kwa ajili ya watu wa Israeli. Kisha tolea hapo sadaka za watu na kuwafanyia ibada ya upatanisho kama alivyoamuru Mwenyezi-Mungu.”
8Basi, Aroni akaikaribia madhabahu, akamchinja yule ndama aliyemtoa awe sadaka ya kuondoa dhambi yake mwenyewe. 9Wanawe wakamletea damu, naye akachovya kidole chake katika damu hiyo na kuzipaka pembe za madhabahu. Damu iliyosalia akaimwaga kwenye tako la madhabahu. 10Lakini mafuta na figo akaviteketeza vyote juu ya madhabahu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose. 11Lakini ile ngozi akaiteketeza kwa moto nje ya kambi.
12Kisha Aroni akamchinja mnyama wa sadaka ya kuteketezwa. Wanawe wakamletea damu, naye akainyunyizia madhabahu pande zote. 13Kisha wakamletea sadaka ya kuteketezwa, kipande kimojakimoja, na kichwa; naye akaviteketeza juu ya madhabahu. 14Akaosha matumbo na miguu na kuiteketeza pamoja na ile sadaka ya kuteketezwa kwenye madhabahu.
15Kisha, Aroni akaweka mbele sadaka ya watu. Alimchukua mbuzi wa sadaka ya watu ya kuondoa dhambi, akamchinja na kumtoa sadaka ya kuondoa dhambi, kama alivyofanya kwa yule wa kwanza. 16Kisha akaweka mbele ile sadaka ya kuteketezwa akatolea sadaka hiyo kulingana na agizo. 17Kisha akaweka mbele sadaka ya nafaka akijaza konzi moja na kuiteketeza juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya kila asubuhi.
18 # Taz Lawi 3:1-11 Halafu Aroni akamchinja pia fahali na yule kondoo dume wa sadaka za amani kwa ajili ya watu. Wanawe wakamletea damu ambayo aliinyunyizia madhabahu pande zote. 19Mafuta ya fahali huyo na kondoo dume, mkia wa kondoo, mafuta yaliyofunika matumbo, figo na sehemu bora ya ini 20wakayaweka juu ya vidari, naye akaviteketeza kwenye madhabahu. 21Lakini vile vidari na ule mguu wa nyuma wa kulia, Aroni alifanya navyo ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu, kama Mose alivyoamuru.
22 # Taz Hes 6:22-26 Aroni alipomaliza kutolea sadaka zote: Sadaka za kuondoa dhambi, sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, aliwainulia watu mikono, akawabariki, kisha akashuka chini. 23Ndipo Mose na Aroni wakaingia ndani ya hema la mkutano; walipotoka waliwabariki watu, nao utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukaonekana kwa watu wote. 24Mwenyezi-Mungu akawasha moto ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wote walipouona huo moto walipaza sauti na kusujudu.

Mambo Ya Walawi9;1-24


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 6 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..8...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Ni siku nyingine tena Mungu wetu ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona tena leo hii..
Tumshukuru Muumba wetu kwa wema na fadhili zake..
Asante Baba wa Mbinguni kwa ulinzi wako na kutuamsha salama..
Asante kwa siku hii na tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako..

Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe kwa kuwaza,kunena,kutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa mbinguni nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Mfalme wa Amani tunaomba utuepushe katika  majaribu utuokoe  na yule mwovu na kazi zake,Ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike na Damu ya mwanao mpendwa Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,Yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..
Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena na kutenda tupate kutambua/kijtambua na tukawe na kiasi..
Tukawe barua njema na tukasomeke sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo /zitokazo nasi ukatupe Neema ya kuwabariki wengine..
Ukabariki tuingiapo/tutokapo,Vilaji/vinywaji,vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Jehovah..Vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..

Tazama wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,waliokwenye vifungo mbalimbali,waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu/mashaka,Wagonjwa,wafiwa ukawe mfariji wao..Ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,ukawaponye kiroho na kimwili..wakakuone kwenye shida zao Mungu wetu,wanaokutafuta wakuone,wanaokulilia ukawafute machozi,wanaokuomba ukawajibu Mungu wetu,Ukawainue wanyonge,waliodhulumiwa wakapate haki zao,ukawatendee sawasawa na mapenzi yako..



Kwa wimbo nitalisifu jina la Mungu, nitamtukuza kwa shukrani. Jambo hili litampendeza Mwenyezi-Mungu zaidi, kuliko kumtolea tambiko ya ng'ombe, kuliko kumtolea fahali mzimamzima. Wanyonge wataona hayo na kufurahi; wanaomheshimu Mungu watapata moyo. Mwenyezi-Mungu huwasikiliza fukara; hatawasahau kamwe watu wake wafungwa. Enyi mbingu na dunia msifuni Mungu; bahari na vyote vilivyomo, msifuni. Maana Mungu atauokoa mji Siyoni, na kuijenga tena miji ya Yuda. Watu wake wataishi humo na kuimiliki; wazawa wa watumishi wake watairithi, wale wanaopenda jina lake wataishi humo.

Mpendwa haijalishi unapitia nini Mungu wetu yu mwema na kamwe hawezi kukuacha,jipe moyo,Muombe, muite naye ataitika,Mungu wetu hakawii wala hachelewi,Yeye yupo,yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho,Yeye anatujua zaidi tunavyojijua,yeye atosha..Usife moyo,simama,usikatishwe tamaa na wanadamu,Mungu wetu hashindwi yeye ni mwingi wa Rehema/Neema..Yeye ni muweza wa yote..yeye hawezi kukuacha,Mungu wetu si kiziwi anasikia,Mungu wetu si kipofu anaona,Mungu wetu si Bubu anajibu..
Inuka anza na Bwana yeye atakushindia..Bado hujachelewa,Haijalishi umeanguka kiasi gani,haijalishi umehasi kwa muda gani..Mungu wetu husamehe na kuokoa,Anaponya moyo wako na mwili wako..yeye ni Ndimi Mungu wetu..Hachoki,Halali wala hasinzii..
Mungu akubariki na kukuinua..

Asante Baba wa Mbinguni..

Tunayaweka haya yote mikoni mwako Mungu wetu..Tunaamini wewe ni Mungu wetu hakuna Mungu mwingine..
Wewe unatujua kulikotunavyojijua..

Tunakushukuru Mungu wetu,Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe..

Kwakua Ufalme ni Wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana kwakutumbelea hapa..
MUNGU akawabariki katika yote..
Nawapenda.


Kuwekwa wakfu kwa Aroni na wanawe

(Kut 29:1-37)

1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Mwite Aroni na wanawe wakutane mbele ya mlango wa hema la mkutano; chukua mavazi matakatifu, mafuta ya kupaka, ng'ombe wa sadaka ya kuondolea dhambi, kondoo madume wawili, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu. 3Kisha, ikusanye jumuiya yote ya Waisraeli mbele ya mlango wa hema la mkutano.” 4Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, akaikusanya jumuiya yote mbele ya mlango wa hema la mkutano. 5Mose akaiambia jumuiya yote hivi: “Lifuatalo ni jambo ambalo Mwenyezi-Mungu ameamuru lifanywe.” 6Hapo Mose akawaleta Aroni na wanawe na kuwatawadha. 7Kisha akamvika Aroni joho na kuifunga kwa mkanda, akamvika kanzu, akamvalisha kizibao na kukifunga kiunoni mwake kwa mkanda uliofumwa kwa ustadi. 8#Taz Kut 28 Kisha akaweka kifuko kifuani pa Aroni na ndani ya kifuko hicho akatia mawe ya kauli. 9Halafu akamvika Aroni kilemba na upande wa mbele wa kilemba hicho akaweka pambo la dhahabu, taji takatifu, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru.
10Kisha Mose akachukua mafuta ya kupaka, akaipaka ile maskani na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake akaviweka wakfu. 11Alinyunyiza sehemu ya mafuta hayo juu ya madhabahu mara saba, akaipaka mafuta na vyombo vyake vyote, birika na tako lake, kuviweka wakfu. 12Vilevile Mose akampaka Aroni mafuta kichwani ili kumweka wakfu. 13Kisha Mose akawaleta wana wa Aroni akawavika joho na kuwafunga mikanda viunoni, na kuwavisha kofia kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.
14Kisha Mose akamleta ng'ombe wa sadaka ya kuondoa dhambi, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha ng'ombe huyo. 15Mose akamchinja huyo ng'ombe, akachukua damu akazipaka pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake kuitakasa. Kisha akachukua damu iliyobaki akaimwaga chini kwenye tako la madhabahu ambayo aliweka wakfu kwa kuifanyia ibada ya upatanisho. 16Kisha, akachukua mafuta yote yaliyokuwa kwenye matumbo yake, sehemu bora ya ini pamoja na figo zote mbili na mafuta yake na kuviteketeza juu ya madhabahu. 17Lakini nyama ya ng'ombe huyo, ngozi yake na mavi yake, akaviteketeza kwa moto nje ya kambi kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.
18Kisha, Mose akamleta kondoo dume wa sadaka ya kuteketezwa. Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo huyo. 19Mose akamchinja na damu ya kondoo huyo akairashia madhabahu pande zake zote. 20Alimkata huyo kondoo vipandevipande, akaviteketeza pamoja na kichwa chake na mafuta yake. 21Baada ya matumbo na miguu kuoshwa kwa maji, Mose aliviteketeza vyote juu ya madhabahu pamoja na sehemu nyingine za huyo kondoo kama sadaka ya kuteketezwa. Hiyo ni sadaka itolewayo kwa moto, yenye harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu. Mose alifanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. 22Kisha akamleta kondoo dume mwingine, kwa ajili ya kuweka wakfu. Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo huyo. 23Mose akamchinja. Akachukua damu ya kondoo huyo na kumpaka Aroni kwenye ncha ya sikio lake la kulia, kidole gumba cha mkono wake wa kulia na cha mguu wake wa kulia. 24Wanawe Aroni nao wakaja, naye Mose akawapaka kiasi cha damu kwenye ncha za masikio yao ya kulia, vidole gumba vya mikono yao ya kulia na kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu nyingine akainyunyizia madhabahu pande zake zote. 25Kisha, akachukua mafuta yote, mkia pamoja na mafuta yake, mafuta yote yanayofunika matumbo, sehemu bora ya ini, pamoja na figo zote mbili, mafuta yake na paja la mguu wa kulia wa nyuma wa huyo kondoo dume. 26Kisha, kwenye kile kikapu cha mikate iliyowekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu akatoa mkate mmoja usiotiwa chachu, mkate mmoja wenye mafuta na mkate mmoja mdogo, akaviweka vyote juu ya vipande vya mafuta na ule mguu. 27Mose akaviweka mikononi mwao Aroni na wanawe, nao wakafanya ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu. 28Kisha Mose akavichukua vitu hivyo vyote kutoka mikononi mwao na kuviteketeza juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa. Hii ni sadaka ya kuwekwa wakfu, yenye harufu ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu; ni sadaka itolewayo kwa moto. 29Kisha Mose akachukua kile kidari na kufanya ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu. Sehemu hiyo ya yule kondoo dume wa kuweka wakfu ni mali yake Mose kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.
30Halafu Mose akachukua mafuta ya kupaka na damu kutoka madhabahu akamnyunyizia Aroni na wanawe hata na pia mavazi yao. Hivyo Mose akamweka wakfu Aroni na wanawe pamoja na mavazi yao.
31Mose akamwambia Aroni na wanawe, “Chemsheni ile nyama mbele ya mlango wa hema la mkutano, muile hapo mlangoni pamoja na mkate kutoka katika kikapu chenye sadaka za kuwekea wakfu. Fanyeni kama nilivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, kwamba sehemu hiyo italiwa na Aroni na wanawe. 32Nyama yoyote au mkate wowote utakaosalia ni lazima kuteketezwa. 33Hamtatoka nje ya mlango wa hema la mkutano kwa muda wote wa siku saba, yaani mpaka muda wenu wa kuwekwa wakfu umekwisha, muda ambao utachukua siku saba. 34Mwenyezi-Mungu ameamuru tufanye kama tulivyofanya leo ili tuwafanyieni ibada ya upatanisho. 35Mtabaki mlangoni mwa hema la mkutano usiku na mchana kwa muda wa siku saba, mkifanya mambo aliyoamuru Mwenyezi-Mungu, la sivyo mtakufa. Ndivyo nilivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu.” 36Basi, Aroni na wanawe wakafanya mambo yote aliyoamuru Mwenyezi-Mungu kwa njia ya Mose.

Mambo Ya Walawi8;1-36

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 5 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..7...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu, Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,Mfalme wa Amani, Muweza wa yote, Alfa na Omega, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.. Yahweh..!Jehovah..!
Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mfalme wa Amani..

Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Baba..kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..


Utuepushe na majaribu na utulinde na yule mwovu na kazi zake, Ututakase Miili yetu na Akili zetu utufunike na Damu ya mwanao mpendwa Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka ili sisi tupate kupona..

Asante kwa ulinzi wako usiku wote na siku zote Mfalme wa Amani umekuwa nasi..
Tazama Jana imepita Baba wa Mbinguni Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine...

Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii..
Tunaomba ukatubariki na kubariki katika  yote tunayoenda kufanya/kutenda na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Tukawe chombo chema na tukatumike sawasawa na mapenzi yako..
Tukaanze siku/wiki hii nawe Mungu wetu,ikawe yenye Baraka,Amani,Upendo,utuwema,fadhili na kuchukuliana..

ukatupe Hekima,Busara katika kila jambo, tupate kutambua/kujitambua na Utukufu tukurudishie wewe Muumba wetu..


Yesu aliendelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri. Mtu mmoja akamwuliza, “Je, Mwalimu, watu watakaookoka ni wachache?” Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza. Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Nyinyi mtasimama nje na kuanza kubisha mlango mkisema: ‘Bwana, tufungulie mlango.’ Lakini yeye atawajibu: ‘Sijui mmetoka wapi.’ Nanyi mtaanza kumwambia: ‘Sisi ndio wale tuliokula na kunywa pamoja nawe; na wewe ulifundisha katika vijiji vyetu.’ Lakini yeye atasema: ‘Sijui nyinyi mmetoka wapi; ondokeni mbele yangu, enyi nyote watenda maovu.’ Ndipo kutakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo na manabii wote wapo katika ufalme wa Mungu, lakini nyinyi wenyewe mmetupwa nje! Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini na kukaa kwenye karamu katika ufalme wa Mungu. Naam, wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza; na wale walio wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Baba wa Mbinguni tunaiweka" Coventry "mikononi mwako ,
Tunaiweka "LONDON- UK "Nchi nzima mikononi mwako..
ukailinde na kutulinda wote tunaoishi hapa,ukatuokoe na wenye nia mbaya..ukatuepushe na Udini/Ukabila na tofauti zozote zinazoendelea na ukawafariji waliopatwa na  msiba na ukawaponye waliopatwa na maumivu/kuumizwa..Tunaomba Amani itokayo kwako,Tunaomba ukatawale ee Mungu wetu tunaomba ukatupe hekima na busara na uvumilivu kwenye  wakati huu mgumu...Mungu wetu ukaonekane na kututendea...

Tazama wenye shida/tabu na wote wanaopitia magumu/majaribu, wenye vifungo mbalimbali Mfalme wa Amani ukawaguse na mkono wako wenye nguvu  kuwaponye kimwili na kiroho pia..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako Mungu wetu, Tuliyoyanena na tusiyoyanena Baba wa Mbinguni unayajua na kutujua zaidi ya tunavyojijua..
Kwa kuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..

Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea..
wote mnaopita hapa na akawape sawasaswa na mapenzi yake..
Asanteni sana kwakuwa nami/kunisoma..
Nawapenda.


Sadaka za fidia

1“Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa hatia. Sadaka hiyo ni takatifu kabisa. 2Mnyama wa sadaka ya kuondoa hatia atachinjiwa mahali wanapochinjiwa wanyama wa sadaka za kuteketezwa, na damu yake itarashiwa madhabahu pande zake zote. 3Mafuta yake yote: Mafuta ya mkia na yale yanayofunika matumbo yatatolewa na kuteketezwa 4pamoja na zile figo mbili pamoja na mafuta yake na ile sehemu bora ya ini. 5Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni sadaka ya kuondoa hatia. 6Wanaoruhusiwa kula sadaka hiyo ni wanaume wa ukoo wa makuhani peke yao; ni sadaka takatifu kabisa. Italiwa katika mahali patakatifu. 7Sheria ni moja kuhusu sadaka ya kuondoa hatia na sadaka ya kuondoa dhambi: Kuhani anayefanya ibada ya upatanisho ndiye atakayeichukua. 8Kuhani anayetoa sadaka ya kuteketezwa ya mtu yeyote, atachukua ngozi ya mnyama aliyetolewa. 9Sadaka yoyote ya nafaka iliyookwa jikoni au katika sufuria au katika kikaango itakuwa mali ya kuhani anayeitoa. 10Kila sadaka ya nafaka, iwe imechanganywa na mafuta au kavu, itakuwa ya wazawa wa Aroni, na wote wagawiwe kwa sawa.

Sadaka za amani

11“Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka za amani ambazo mtu aweza kumtolea Mwenyezi-Mungu. 12Ikiwa mtu anatoa sadaka hiyo ya kumshukuru Mungu, basi, ataitoa pamoja na maandazi yasiyotiwa chachu yaliyopakwa mafuta, mikate myembamba iliyopakwa mafuta na maandazi ya unga laini uliochanganywa na mafuta. 13Pamoja na sadaka hiyo yake ya amani ya kumshukuru Mungu, ataleta maandazi yaliyotiwa chachu. 14Kutokana na maandazi hayo, atamtolea Mwenyezi-Mungu andazi moja kutoka kila sadaka; maandazi hayo yatakuwa yake kuhani anayeirashia madhabahu damu ya sadaka za amani. 15Nyama ya sadaka hiyo ya amani ya kumshukuru Mungu italiwa siku hiyohiyo inapotolewa; hataacha hata sehemu yake hadi asubuhi. 16Lakini kama sadaka hiyo ya amani ni ya nadhiri au ya hiari, italiwa siku hiyohiyo inapotolewa na sehemu nyingine yaweza kuliwa kesho yake. 17Lakini nyama yoyote ya sadaka hiyo inayobaki hadi siku ya tatu itateketezwa. 18Tena nyama yoyote ya sadaka ya amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitapokelewa kwa faida yake mtu aliyeitoa. Nyama hiyo ni chukizo na mtu atakayeila atawajibika kwa uovu wake.
19“Nyama yoyote inayogusa kitu najisi isiliwe. Nyama hiyo itateketezwa kwa moto. Wote walio safi wanaweza kula nyama 20iliyotolewa sadaka ya amani kwa Mwenyezi-Mungu. Lakini mtu yeyote aliye najisi, akila nyama hiyo, atatengwa na watu wake. 21Mtu yeyote anayegusa kitu chochote kilicho najisi, au kitu najisi cha mtu, au mnyama aliye najisi, au kitu chochote najisi ambacho ni chukizo, akila nyama ya sadaka ya amani aliyotolewa Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atatengwa na watu wake.”
22Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 23“Waambie Waisraeli hivi: Msile mafuta ya ng'ombe au ya kondoo au ya mbuzi. 24Mafuta ya mnyama yoyote aliyekufa mwenyewe au ya mnyama aliyeuawa na mnyama wa porini yaweza kuwekwa kwa matumizi mengine, lakini kamwe msiyale. 25Mtu yeyote akila mafuta ya mnyama aliyetolewa kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto, atatengwa na watu wake. 26#Taz Mwa 9:4; Lawi 17:10-14; 19:26; Kumb 12:16,23; 15:23 Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi. 27Mtu yeyote akila damu yoyote, atatengwa na watu wake.”
28Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 29“Waambie watu wa Israeli hivi: Mtu yeyote akitoa sadaka ya amani, atampa Mwenyezi-Mungu sehemu ya sadaka hiyo. 30Atamletea kwa mikono yake mwenyewe kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Ataleta mafuta yake pamoja na kidari ambacho atafanya nacho ishara ya kumtolea Mwenyezi-Mungu. 31Kuhani atayateketeza mafuta yote juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Aroni na wanawe makuhani. 32Mguu wa kulia wa nyuma wa mnyama wa sadaka zenu za amani mtampa kuhani. 33Mguu huo utakuwa mali ya kuhani aliye mzawa wa Aroni anayetoa damu ya sadaka za amani na mafuta yake. 34Mwenyezi-Mungu amewaagiza watu wa Israeli watenge kidari hicho na mguu huo wa mnyama wa sadaka zao za amani, wampe kuhani Aroni na wazawa wake, maana sehemu hiyo wamewekewa hao makuhani milele. 35Hiyo ndiyo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe kutoka katika sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto, tangu siku walipotawazwa kuwa makuhani wa Mwenyezi-Mungu. 36Walipowekwa wakfu kwa kupakwa mafuta, Mwenyezi-Mungu aliamuru Waisraeli wawape sehemu hiyo ya sadaka; hiyo itakuwa daima haki yao.”
37Basi, hayo ndiyo maagizo kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya kuondoa dhambi, sadaka ya kuondoa hatia, kuhusu kuwekwa wakfu na kuhusu sadaka ya amani. 38Mwenyezi-Mungu alimpa Mose amri hizi mlimani Sinai siku ile alipowaamuru Waisraeli wamletee sadaka zao, kule jangwani Sinai.

Mambo Ya Walawi7;1-38


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday 2 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..6...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu..
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako..
Asante kwakutulinda usiku na wakati wote..
Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuona leo hii..
Tunakuja mbele zako Baba wa Mbinguni tukijinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako..

Tunaomba utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe kwa kuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe waliotukosea..
Utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake..
Roho mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..

Jehovah.. tunaomba ututakase Miili yetu na Akili zetu..Tupate kutambua na kujitambua..
Tukawe barua njema na tukasomeke popote tutakapopita sawasawa na mapenzi yako.

Yahweh..Tazama Yatima na Wajane,wagonjwa,wafiwa ukawe mfariji wao, waliomagerezani pasipo na hatia,waliokatika vifungo vya mwovu,wenye shida/tabu na wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Baba wa Mbinguni Nyoosha mkono wako wenye nguvu,ukawaguse na kuwaponya Baba..ukawafungue na wakawe huru kiroho na kimwili,ukaonekane kwenye mapito yao Mungu wetu..

Wapendwa/waungwana yupo aponyae na kumaliza kabisa matatizo.
Mtabibu wa ajabu,Mwokozi wetu,ukiamini na kufuata njia zake
mkabidhi maisha yako,mwamini yeye anaweza,hakuna mganga wala mponyaji kama yeye,hakuna dawa kubwa kama Imani..
Amini yeye anaweza yote,Amini yeye anaponya,Amini yeye atakutendea, Amini yeye atakufungua..


Basi si kwamba nikisema muamini muamini kizembe na kukosa maarifa..
Siyo unatafuta kazi au kuongeza kipato unalala saa zote sababu unaamini
Mungu yupo,Acha uvivu na ukajitume..Acha kuishi maisha ya miujiza haijeleti yenyewe huku umekaa ndani au umelala tuu unasubiri Mungu akutendee sababu una Imani..



Watu wangu wameangamia kwa kutonijua, maana wewe kuhani umekataa mafundisho. Nimekukataa kuwa kuhani wangu. Kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, nami pia nitawasahau watoto wako.

Kama unacho hicho kidogo anza nacho na uku ukiomba Mungu akupe maarifa zaidi,Kulala tuu au kukaa kijiweni hakuta kusaidia kitu hata ukisema unaamini Mungu....


Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu amefariki, na kama ujuavyo, alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia fedha amekuja kuwatwaa wanangu wawili wawe watumwa wake.” Elisha akamwuliza, “Sasa nikusaidieje? Niambie kile ulicho nacho nyumbani.” Mama huyo mjane akamjibu, “Mimi mtumishi wako sina kitu chochote ila chupa ndogo ya mafuta.” Elisha akamwambia, “Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadiri utakavyopata. Kisha uende, wewe pamoja na wanao, mjifungie ndani ya nyumba, na muanze kujaza mafuta. Kila chombo mnachojaza, kiwekeni kando.” Akaenda na kujifungia ndani ya nyumba na wanawe na kuanza kumimina mafuta ndani ya vyombo. Vilipojaa vyote, akamwambia mwanawe mmojawapo, “Niletee chombo kingine.” Mwanae akamjibu, “Vyote vimejaa!” Hapo mafuta yakakoma kutiririka. Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Naye mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki.”

Hasa kunavijiwe sugu siku hizi "MITANDAONI" Kutwa mtu unashinda huko mitandaoni basipo na faida, wapo wanaofaidika na kujifunza mengi kupitia mitandao pia,tutumie kwa faida kama siyo tuwe na kiasi...

Yesu akaendelea kuwaambia, “Je, watu huwasha taa wakaileta ndani na kuifunika kwa debe au kuiweka mvunguni? La! Huiweka juu ya kinara. Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa. Mwenye masikio na asikie!” Akawaambia pia, “Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa. Aliye na kitu atapewa zaidi; asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.”
Mungu atupe macho ya kuona na masikio ya kusikia..Mungu akatupe 
ufahamu na kuelewa,tukatambue/kujitambua..

Asante Baba wa Mbinguni, Mungu wetu na Baba yetu..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako..Tukiamini na kushukuru..

Kwakua Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!


Asanteni sana wote mnaotembelea hapa
Mungu aendelee kuwafunulia na kuwaongoza katika maisha yenu

Mbarikiwe sana.
Nawapenda.



1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Ikiwa mtu yeyote ametenda dhambi na kumwasi Mwenyezi-Mungu kwa kumdanganya jirani yake juu ya amana au dhamana aliyowekewa, au kumnyanganya au amemdhulumu mwenzake, 3au amepata kitu cha jirani yake kilichopotea, akasema kwamba hakukiona, au ameapa uongo juu ya chochote ambacho watu hufanya wakawa na hatia, 4mtu huyo anapokuwa ametenda dhambi na amekuwa na hatia, ni lazima arudishe alichoiba au alichopata kwa dhuluma, au amana aliyopewa, au kitu cha jirani yake kilichopotea akakipata, 5au chochote alichoapa kwa uongo. Atalipa kila kitu kikamilifu na kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Mara atakapojua kosa lake atamrudishia mwenyewe. 6Kisha atamletea kuhani kondoo dume au mbuzi dume asiye na dosari amtolee Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa hatia; thamani ya mnyama huyo itakuwa ile ya kawaida ya kuondoa hatia. 7Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho mbele ya Mwenyezi-Mungu, naye atasamehewa kosa ambalo alikuwa amelifanya.”

Sadaka za kuteketezwa
8Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 9“Mpe Aroni na wanawe maagizo haya: Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuteketezwa. Sadaka ya kuteketezwa itakuwa motoni juu ya madhabahu usiku kucha hadi asubuhi na moto wake uchochewe, usizimike. 10Kisha kuhani akiwa amevaa vazi lake rasmi la kitani na kaptura yake ya kitani, atachukua majivu ya ile sadaka kutoka madhabahuni na kuyaweka kando ya madhabahu. 11Halafu baada ya kubadilisha mavazi yake atayapeleka yale majivu nje ya kambi mahali palipo safi. 12Moto wa madhabahu lazima uendelee kuwaka, na wala usizimwe. Kila siku asubuhi kuhani ataweka kuni kwenye moto huo na juu yake atapanga sadaka ya kuteketezwa, kabla ya kuteketeza mafuta ya sadaka ya amani. 13Moto utaendelea kuwaka daima juu ya madhabahu bila kuzimishwa kamwe.

Sadaka za nafaka

14“Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya nafaka. Wazawa wa Aroni ndio walio na uwezo wa kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo juu ya madhabahu. 15Mmoja wa makuhani atachukua konzi moja ya unga wa sadaka ya nafaka pamoja na mafuta na ubani wote na kuviteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho; harufu yake itampendeza Mwenyezi-Mungu. 16Unga uliosalia atakula Aroni na wazawa wake makuhani bila kutiwa chachu. Wataula kwenye mahali patakatifu uani mwa hema la mkutano. 17Kamwe usiokwe pamoja na chachu. Nimewapa wao sehemu hiyo kutoka sadaka wanazonitolea kwa moto. Ni sadaka takatifu kabisa kama zilivyo sadaka za kuondoa dhambi na za kuondoa hatia. 18Wazawa wa kiume wa Aroni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa daima kwa ajili yao kutoka sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mtakatifu.”
19Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 20“Tangu wakati wa kuwekwa wakfu kwa Aroni na wazawa wake wanapaswa kumtolea Mwenyezi-Mungu kilo moja ya unga laini kwa siku, nusu moja ya unga huo ataitoa asubuhi na nusu nyingine jioni. 21Unga huo utachanganywa na mafuta na kuokwa; kisha utauleta ukiwa vipandevipande na kumtolea Mwenyezi-Mungu; na harufu ya sadaka yake itampendeza Mungu. 22Kuhani aliye mzawa wa Aroni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka hiyo; hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa. 23Sadaka yoyote ya nafaka iliyotolewa na kuhani itateketezwa yote; haitaliwa kamwe.”

Sadaka za kuondoa dhambi
24Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 25“Mwambie Aroni na wanawe kuwa ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa dhambi, mahali pale ambapo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa ndipo atakapochinjiwa mnyama wa sadaka ya kuondoa dhambi, mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka takatifu kabisa. 26Kuhani anayetolea sadaka hiyo ndiye atakayeila. Italiwa mahali patakatifu, uani mwa hema la mkutano. 27Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu; vazi lolote likidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, vazi hilo litaoshewa mahali patakatifu. 28Sadaka hiyo ikichemshiwa katika vyombo vya udongo, vyombo hivyo vitavunjwa. Lakini ikiwa vyombo hivyo ni vya shaba, basi, vitasafishwa na kusuzwa kwa maji. 29Wanaoruhusiwa kuila ni wanaume wa ukoo wa makuhani peke yao kwa vile hiyo ni sadaka takatifu kabisa. 30Lakini kama damu ya sadaka yoyote ya kuondoa dhambi imeletwa ndani ya hema la mkutano ili kufanyia ibada ya upatanisho katika mahali patakatifu, sadaka hiyo itateketezwa kwa moto.”

Mambo Ya Walawi6;1-30

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 1 June 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..5.


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..


Haleluyah..!Haleluyah..!Haleluyah!!
Mungu wetu yu mwema sana na Fadhili zake za dumu milele..

Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Baba yetu,Mungu wetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo ni mali yako,Mfalme wa Amani,Muweza wa Yote,Baba wa Yatima,Mume wa Wajane,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Yahweh..,Jehovah, Eli Shaddai, Wewe Ndimi Mwenyezi- Mungu,wewe ndimi Mungu wetu..Unatosha Baba wa Mbinguni, Hakuna kama wewe..!!
Leo ni siku mpya Baba wa Mbinguni Tazama Jana imepita na kesho ni siku nyingine..!
Tazama tumemaliza vyema mwezi wa 5 na tunaanza mwezi huu mpya wa 6 Jehovah..!
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako..

Asante kwa ulinzi wako usiku wote na siku zote umekuwa nasi ..
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha  kuendelea kuiona tena siku hii/Mwezi huu..
Tunakuja mbele zako Baba wa Mbinguni tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..

Tunaomba utusamehe Dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mfalme wa Amani tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kusameheana na kuchukuliana..

Jehovah utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake..
Utufunike kwa Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Roho Mtakatifu atuongoze kwenye kunena/kutenda na tukawe na kiasi..

Jehovah..Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo yeye alikufa ili sisi tupate kupona..
Baba wa Mbinguni ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi ukatupe Neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..
Ukatubariki tuingiapo/tutokappo na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..


Mfalme wa Amani tunapoanza mwezi huu Baba wa Mbinguni uwe nasi na ukatubariki na kutufungulia milango ya Neema na Baraka,Tusipungukiwe mahitaji yetu na ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Ukatuongoze,tupate kutambua/kujitambua,ukatupe Amani ya moyo,Furaha,Utuwema,Upendo wa kweli,Upole kiasi,Unyenyekevu,msukumo/shauku ya kujua zaidi/kujifunza zaidi Neno lako na likawe kinga,likawe mwanga,likawe nguzo,lika stawi maishani mwetu,likatufae sisi na wengine pia..
Jehovah ukaonekane kwenye maisha yetu na ukatufanye chombo kipya na tukatumike sawaswa na mapenzi yako..

Furaha ya kweli

(Luka 6:20-23)
“Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. Heri walio wapole, maana watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa. Heri walio na huruma, maana watahurumiwa. Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu. Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu. Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao. “Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.
Ukawaguse na mkono wako wenye nguvu na kuwaponya wote wanaopitia magumu/majaribu/mapito mbalimbali..Ukawafungue waliokatika vifungo mbalimbali na ukawaponye kiroho na kimwili pia..

Tunayaweka haya yote mikononi mwako tuliyoyanena na tusiyoyanena
Baba unajua mioyo yetu na unatujua kuliko tunavyojijua..


Tunakushukuru na kukuabudu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..

Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana..
wote mnaopitia hapa..sina Neno zuri kwenu zaidi ya kuwaombea

na Mungu aendelee kuwabariki..
Nasema..Asanteni sana sana ..
Nawapenda mno.


Sadaka nyingine za kuondoa dhambi

1“Kama mtu yeyote akitakiwa kutoa ushahidi kwenye baraza juu ya jambo aliloona au kulisikia naye akakataa kusema kitu, basi, huo ni uovu na atauwajibikia. 2Au kama mtu yeyote miongoni mwenu amekuwa najisi bila kukusudia kwa kugusa kitu chochote najisi, iwe ni mzoga wa mnyama wa porini au wa kufugwa au wadudu, atakuwa na hatia. 3Au mtu akigusa chochote kilicho najisi cha binadamu, kiwe kiwacho, ambacho humfanya mtu kuwa najisi, naye hana habari, basi, atakapojua atakuwa na hatia. 4Au, kama mtu akiapa kufanya chochote kile, chema au kibaya, kama wafanyavyo watu bila kufikiri, atakapojua atakuwa na hatia. 5Basi, mtu akiwa na hatia kuhusu mambo hayo lazima akiri dhambi yake aliyotenda 6na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.
7“Lakini kama hawezi kutoa mwanakondoo wa sadaka ya kuondoa hatia kwa ajili ya dhambi aliyotenda, basi atamletea Mwenyezi-Mungu hua wawili au makinda mawili ya njiwa: Mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, na mwingine kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. 8Atawaleta kwa kuhani, naye kuhani atamtoa mmoja awe sadaka ya kuondoa dhambi kwa kumkongonyoa shingo yake bila kukichopoa kichwa chake. 9Sehemu ya damu yake ataipaka pembeni mwa madhabahu na ile nyingine ataimimina chini kwenye tako la madhabahu. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi. 10Kisha atamtoa yule wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa kulingana na maagizo. Kuhani atamfanyia huyo mtu upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
11“Ikiwa hawezi kutoa hua wawili au makinda mawili ya njiwa kama sadaka yake ya kuondoa dhambi aliyotenda, basi, ataleta unga kilo moja. Lakini hatautia mafuta wala ubani kwani ni sadaka ya kuondoa dhambi. 12Atamletea kuhani, naye atachukua unga huo konzi moja na kuuteketeza juu ya madhabahu kama sehemu ya ukumbusho, pamoja na sadaka anazotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi. 13Basi, kuhani atamfanyia huyo mtu ibada ya upatanisho kwa ajili ya dhambi, naye atasamehewa. Unga unaobaki utakuwa wake kuhani kama ifanyikavyo kuhusu sadaka ya nafaka.”

Sadaka za fidia
14Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 15“Kama mtu yeyote akikosa kwa kutenda dhambi bila kujua kuhusu kutotoa vitu vitakatifu anavyotolewa Mwenyezi-Mungu, atamletea kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake. Wewe utapima thamani yake kulingana na kipimo rasmi cha mahali patakatifu. Hiyo ni sadaka ya kuondoa hatia. 16Zaidi ya hayo, huyo mtu atalipa madhara yote aliyosababisha kuhusu vitu vitakatifu kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake na kumpatia kuhani yote. Basi, kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa huyo kondoo dume aliye sadaka ya kuondoa hatia, naye atasamehewa.
17“Mtu yeyote akitenda dhambi bila kujua, kwa kuvunja amri yoyote ya Mwenyezi-Mungu, yeye ana hatia, na atalipa adhabu ya hatia yake. 18Atamletea kuhani kondoo dume asiye na dosari kutoka kundi lake akiwa na thamani sawa na ile ya sadaka ya hatia. Na kuhani atamfanyia upatanisho kwa kosa alilofanya, naye atasamehewa. 19Hiyo ni sadaka ya hatia; yeye ana hatia mbele ya Mwenyezi-Mungu.”

Mambo Ya Walawi5;1-19


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Wednesday 31 May 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mambo Ya Walawi..4...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?

Tumshukuru Mungu wetu yeye yu mwema..

Haleluyah..!Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi na vyote vilivyomo,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Muweza wa yote,Yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho,Alfa na Omega..!Yahweh..!Jehovah..!Unatosha Baba.. Hakuna kama wewe..!

Tazama Jana imepita Baba wa Mbinguni Leo ni siku mpya Kesho ni siku nyingine...!!
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako,Umekuwa nasi usiku wote na wakati wote..
Asante kwa kutupa kibali cha kuendelea tena kuiona Leo hii ..

Tunakuja Mbele zako tukijinyenyekeza,Tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Baba wa Mbinguni..
Tunaomba utusamehe pale tupokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni kwa kuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua...
Mungu wetu tunaomba nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe nasi waliotukosea..
Tunaomba utuepushe na majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake..

Tunaomba ututakase Miili yetu na Akili zetu na utufunike na Damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena na kutenda na tukawe na kiasi..


Tunaomba ukabariki kuingia kwetu/kutoka kwetu,Vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..

Ukabariki vilaji/vinywaji,Kazi zetu,Biashara,Masomo na vyote tunavyoenda Kugusa/Kutumia Mfalme wa Amani ukavitakase kwa Damu  ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Ukabariki Ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi utupe Neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Baba wa Mbinguni..


Ukawaguse na mkono wako wenye Nguvu wote wanaopitia Magumu/majaribu Mbalimbali,walio kwenye vifungo mbalimbali na Ukawainue wanyonge na waliodhulumiwa wakapate haki yao..
Ukaonekane Jehovah..!! kwenye shida/tabu zao na wote wanaokulilia ukawafute machozi,wanaokuomba Baba ukawajibu sawasawa na mapenzi yako.
Wapendwa yanini mteseke na mizigo ?
Yanini kuteseka na kuugua rohoni?
Yanini kukata tamaa na kuwa na hofu/mashaka?
Baba anawapenda sana..
Asema..


 Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha...!!


Wakati huo Yesu alisema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima na wenye elimu mambo haya, ukawafunulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza. “Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anapenda kumfunulia. Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mkajifunze kwangu, maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtatulizwa rohoni mwenu. Maana, nira niwapayo mimi ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”


Mfalme wa Amani tuyaweka maisha yetu mikononi mwako..Baba wa Mbinguni Tazama watoto wetu wanaondelea na mitihani na wanaojindaa na mitihani ukawabariki na ukawaguse na mkono wako wenye nguvu..wapate kukumbuka na kuelewa yote waliyofundishwa.. wakawe kichwa na si mkia..


Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanya kuwa wa kwanza kwa nguvu na sio wa mwisho. Mtaendelea mbele na sio kurudi nyuma kama mkishika amri zake ambazo ninawapeni leo na kuwa waangalifu kuzitekeleza, bila kugeuka kulia au kushoto kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
Asante Mungu wetu Baba yetu Tunaweka Ndoa zetu Mikononi mwako Mfalme wa Amani ..Kila mmoja akafuate/kufanya jukumu lake..
Mke na akawe mke kama ulivyoagiza,Mume na akawe Mume kama ulivyoagiza..ukatupe kuelewa na kujtambua katika Nyumba zetu na tufuate Neno lako Mungu wetu na si Maneno ya Binadamu..



Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya heshima mliyo nayo kwa Kristo. Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote. Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. Alifanya hivyo ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safi kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. ( Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa, maana sisi ni viungo vya mwili wake). “Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.” Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake. Lakini yanawahusu nyinyi pia: Kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe.
Kanisa linaanzia Nyumbani ..!
 Hasa wa mama mmhh..tumekuwa na mambo mengi mengi kisingizio Maombi,Mikutano,Makundi,Kusaidiana,kushikamana,sisi tunaosema hivyo ndiyo sisi wakwanza kusahau majukumu yetu..Maombi yooote,Mungu tunayemtafuta saa zooote, Mafundisho tunayopeana kila wakati sijui yanaishia wapi..?

 Msinielewe Vibaya  sipingani na haya mambo ya wamama hapana .. Basi yakazae matunda na tuwe na kiasi ..

Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini.

Ee-Mungu Baba tusaidie tuijue kweli yako na tujitambue..
Mungu akinipa kibali cha kuongelea hili ipo siku nitaongea..

Asante Mungu wetu.Tunakushukuru na kukuabudu wewe..
Tunayaweka haya yote mikononi mwako..
Kwakua Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata milele..
Amina..!!

Asanteni sana kwa wote mnaotembelea hapa..
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea 

sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda sana.



Sadaka kwa ajili ya dhambi zisizokusudiwa
1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2“Waambie watu wa Israeli hivi: Kama mtu ametenda dhambi bila kukusudia, akafanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu, atafanya kama ifuatavyo: 3Ikiwa kuhani ambaye amepakwa mafuta ndiye aliyetenda dhambi hata akawatia watu hatiani, basi huyo atamtolea Mwenyezi-Mungu fahali mchanga asiye na dosari awe sadaka ya kuondoa dhambi. 4Atamleta huyo fahali mchanga kwenye mlango wa hema la mkutano, mbele ya Mwenyezi-Mungu; naye ataweka mkono wake juu ya kichwa cha fahali huyo na kumchinja mbele ya Mwenyezi-Mungu. 5Huyo kuhani, aliyepakwa mafuta atachukua kiasi cha damu na kuingia nayo ndani ya hema la mkutano. 6Atachovya kidole chake katika damu hiyo na kuirashia mara saba mbele ya Mwenyezi-Mungu upande wa mbele wa pazia la mahali patakatifu. 7Kuhani atachukua sehemu ya damu na kuzipaka pembe za madhabahu ya kufukizia ubani wa harufu nzuri, mbele ya Mwenyezi-Mungu katika hema la mkutano. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyoko karibu na mlango wa hema la mkutano. 8Kisha atayaondoa mafuta yote ya ng'ombe huyo: Mafuta yanayofunika matumbo, 9figo mbili na mafuta yaliyo juu yake na yale yaliyo kiunoni, na yale yaliyoshikamana na figo na ini; hizi ni sehemu zilezile zinazoondolewa kwa mnyama wa sadaka ya amani. 10Kuhani atazichukua na kuziteketeza juu ya madhabahu ya kuteketezea sadaka. 11Lakini ngozi ya huyo ng'ombe, nyama, kichwa, miguu, matumbo na mavi yake, 12yaani ng'ombe mzima aliyesalia atampeleka na kumteketeza nje ya kambi mahali safi ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni; atachomwa moto hapo mahali pa kumwagia majivu.
13“Iwapo jumuiya yote nzima ya Israeli imetenda dhambi bila ya kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu 14mara dhambi hiyo itakapojulikana, jumuiya yote itatoa fahali mchanga awe sadaka ya kuondoa dhambi. Watamleta kwenye hema la mkutano. 15Wazee wa jumuiya ya watu wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo fahali, kisha atachinjwa mbele ya Mwenyezi-Mungu. 16Yule kuhani aliyeteuliwa rasmi kwa kupakwa mafuta ataleta sehemu ya damu ya huyo fahali ndani ya hema la mkutano. 17Atachovya kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza mbele ya pazia mara saba, mbele ya Mwenyezi-Mungu. 18Kisha, sehemu ya damu atazipaka pembe za madhabahu iliyoko katika hema la mkutano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyo karibu na mlango wa hema la mkutano. 19Mafuta yote ya mnyama huyo atayachukua na kuyateketeza kwenye madhabahu. 20Kwa hiyo atamfanya fahali huyu kama alivyomfanya yule mwingine wa sadaka ya kuondoa dhambi. Basi, huyo kuhani atawafanyia watu ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi, nao watasamehewa. 21Kisha atamchukua fahali huyu na kumpeleka nje ya kambi na kumteketeza kwa moto kama alivyomfanya yule mwingine. Hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi ya jumuiya.
22“Ikiwa mtawala ametenda dhambi bila kukusudia kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, na hivyo akawa na hatia, 23mara akijulishwa dhambi hiyo aliyotenda, ataleta sadaka yake ya beberu asiye na dosari. 24Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha beberu na kumchinjia mahali wanapochinjia sadaka za kuteketezwa mbele ya Mwenyezi-Mungu; hiyo ni sadaka ya kuondoa dhambi. 25Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka. 26Mafuta yote ya beberu huyo atayateketeza madhabahuni, kama afanyavyo na mafuta ya mnyama wa sadaka ya amani. Kwa hiyo kuhani atamfanyia mtawala ibada hiyo ya upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.
27 # Taz Hes 15:27-28 “Kama mtu wa kawaida ametenda dhambi bila kukusudia, kwa kufanya kitu kilichokatazwa na amri ya Mwenyezi-Mungu na hivyo akawa na hatia, 28mara atakapojulishwa kuwa ametenda dhambi, ataleta sadaka ya mbuzi jike asiye na dosari kwa ajili ya kuondoa dhambi aliyotenda. 29Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mbuzi huyo wa sadaka ya kuondoa dhambi, na kumchinjia mahali wanapochinjia wanyama wa sadaka za kuteketezwa. 30Kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu iliyobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu. 31Mafuta yote ya mbuzi huyo atayaondoa kama aondoavyo mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, naye kuhani atayateketeza madhabahuni, na harufu yake nzuri itampendeza Mwenyezi-Mungu. Basi, kuhani atamfanyia huyo mtu hiyo ibada ya upatanisho, naye atasamehewa.
32“Ikiwa mtu huyo ataleta mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi, basi, ataleta mwanakondoo jike asiye na dosari. 33Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mwanakondoo huyo wa sadaka ya kuondoa dhambi, na kumchinjia mahali pale wanapochinjia wanyama wa sadaka za kuteketezwa. 34Kisha kuhani atachovya kidole chake katika damu ya sadaka ya kuondoa dhambi na kuzipaka pembe za madhabahu ya kuteketezea sadaka. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu. 35Kisha atayaondoa mafuta yote kama aondoavyo mafuta ya mwanakondoo wa sadaka ya amani, na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka zitolewazo kwa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Naye kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.”

Mambo Ya Walawi4;1-35


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.