Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 29 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo50...Mwisho wa Kitabu cha Mwanzo..Mungu wetu yu Mwema Sana..!!

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu kwa mema mengi aliyotutendea/anayotutendea..
Sifa na Utukufu ni kwake Daima..



Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga ladhihirisha kazi ya mikono yake. Mchana waupasha habari mchana ufuatao, usiku waufahamisha usiku ufuatao. Hamna msemo au maneno yanayotumika; wala hakuna sauti inayosikika; hata hivyo, sauti yao yaenea duniani kote, na maneno yao yafika kingo za ulimwengu. Mungu ameliwekea jua makao yake angani; nalo hutoka kama bwana arusi chumbani mwake, lafurahi kama shujaa aliye tayari kushindana. Lachomoza toka upande mmoja, na kuzunguka hadi upande mwingine; hakuna kiwezacho kuliepa joto lake. Sheria ya Mwenyezi-Mungu ni kamilifu, humpa mtu uhai mpya; masharti ya Mwenyezi-Mungu ni thabiti, huwapa hekima wasio na makuu. Kanuni za Mwenyezi-Mungu ni sawa, huufurahisha moyo; amri ya Mwenyezi-Mungu ni safi, humwelimisha mtu. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni jambo jema, na la kudumu milele; maagizo ya Mwenyezi-Mungu ni sawa, yote ni ya haki kabisa. Yatamanika kuliko dhahabu; kuliko dhahabu safi kabisa. Ni matamu kuliko asali; kuliko asali safi kabisa. Yanifunza mimi mtumishi wako; kuyafuata kwaniletea tuzo kubwa. Lakini nani aonaye makosa yake mwenyewe? Ee Mungu, niepushe na makosa nisiyoyajua. Unikinge mimi mtumishi wako na makosa ya makusudi, usikubali hayo yanitawale. Hapo nitakuwa mkamilifu, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa. Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yakubalike mbele yako, ee Mwenyezi-Mungu, mwamba wangu na mkombozi wangu!

Yeye aliyetupa Kibali cha kuiona Leo hii..
Yeye ni Mungu wetu ,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi,Yeye atosha,Yeye Mwanzo na Yeye ni Mwisho..Yeye asiyesinzia wala kulala.. Mchana yupamoja nasi Usiku yupamoja nasi Jana,Leo, Kesho na hata Milele yeye atabaki kuwa Mungu, Ije mvua lije jua Mungu yu mwema sana...!!!!Hakuna wa kufanana naye,Hakuna na hatakuwepo kama yeye..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Jehovah..!! Yahweh..!! wewe ni Mkuu wa Yote..
Tunajinyeyekeza mbele zako Baba  na kujiachilia mikononi mwaka Leo na siku zote..Utubariki Baba wa Mbinguni,Tuingiapao/Tutokapo, Tutembeapao,Hatua zetu ziwe nawe Yahweh..
Ubariki Vinywaji/Vilaji,Vyombo vya usafari na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba ukavitakase na Damu ya Mwanao, Bwana wetu Na Mwokozi wetu..Yesu Kristo wa Nazareti....!!!!
Ututakase Miili yetu na Akili zetu Baba..
Roho mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda..Kutambua/kujitambua..
Baba ukabariki Kazi zetu,Biashara,Masomo na Ridhiki zetu Baba ziingiapo na zitokapo Mfalme wa Amani..!!!!
Utusamehe dhambi zetu Baba tulizozitenda kwa kujua/kutojua..
Baba utupe Neema ya kuweza nasi kuwasamehe waliotukosea...
Baba ukawawaponye na kuwaokoa wenye Shida/Tabu, wanaopitia Majaribu/Magumu,wagonjwa,wafiwa ukawe mfariji wao,Waliomagerezani pasipokuwa na hatia,waliofungwa na mwovu, Baba nyoosha mkono wako ukawaguse na kuwaokoa wawe huru kimwili na kiroho..
Mfalme wa Amani Ukatawale na kuibariki Nchi hii tunayoishi, Ukabariki Tanzania Baba, Afrika yote na Dunia nzima..
Ukawaongoze wanaotuongoza nao wakatuongoze katika haki na kweli..
Tunakwenda kinyume na Mwovu Baba..
Tunakuja mbele zako Yahweh..! Sifa na Utukufu ni wako Jehovah..!!tunashukuru na kuaminia kwamba  wewe ni Bwana wetu

na Mwokozi wetu..Yote tunaweka mikononi mwako..
Amina..!!

Muwe na wakati mwema.

1Hapo Yosefu akamkumbatia baba yake akilia na kumbusu. 2Kisha, akawaagiza waganga wake wampake Israeli, baba yake, dawa ili asioze, nao wakafanya hivyo. 3Kama kawaida, siku arubaini zilihitajika kwa kazi hiyo. Wamisri nao wakaomboleza kifo cha Yakobo kwa muda wa siku sabini.
4Baada ya matanga kumalizika, Yosefu akawaambia watu wa jamaa ya Farao, “Ikiwa nimekubalika mbele yenu, tafadhali zungumzeni na Farao kwa niaba yangu kwamba baba yangu aliniapisha, akisema, 5‘Mimi karibu nitafariki. Yakupasa kunizika katika kaburi nililojichongea katika nchi ya Kanaani.’ Kwa hiyo namwomba aniruhusu niende kumzika baba yangu, kisha nitarudi.” 6Farao akajibu, “Nenda ukamzike baba yako kama alivyokuapisha.” 7Basi, Yosefu akaondoka kwenda kumzika baba yake akifuatana na watumishi wote wa Farao, wazee wa nyumba ya Farao, pamoja na wazee wa nchi nzima ya Misri. 8Hali kadhalika, Yosefu alifuatana na jamaa yake yote, ndugu zake na jamaa yote ya baba yake Yakobo. Katika eneo la Gosheni walibaki watoto wao tu pamoja na kondoo, mbuzi na ng'ombe wao. 9Pia waliandamana naye wapandafarasi na magari; lilikuwa kundi kubwa sana.
10Walipofika katika uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, ngambo ya mto Yordani, waliomboleza kwa huzuni kubwa, naye Yosefu akamfanyia baba yake marehemu matanga ya siku saba. 11Wakanaani wenyeji wa nchi hiyo, walipoyaona maombolezo yaliyofanywa kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, wakasema, “Maombolezo haya ya Wamisri, kweli ni makubwa!” Kwa hiyo, mahali pale pakaitwa Abel-misri, napo pako ngambo ya mto Yordani.
12Wana wa Yakobo walimfanyia baba yao kama alivyowaagiza: 13Walimchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makpela, mashariki ya Mamre. Pango pamoja na shamba hilo Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efroni Mhiti, ili pawe mahali pake pa kuzikia. 14Baada ya kumzika baba yake, Yosefu alirudi Misri pamoja na ndugu zake na watu wote waliokuwa wameandamana naye kwenda kumzika baba yake.

Yosefu awaondolea shaka ndugu zake

15Baada ya kifo cha baba yao, ndugu zake Yosefu walisemezana, “Huenda Yosefu atatuchukia na kutulipiza mabaya yote tuliyomtendea.” 16Kwa hiyo wakampelekea Yosefu ujumbe, wakisema, “Baba yako, kabla hajafariki, aliagiza hivi, 17‘Mwambieni Yosefu kwa niaba yangu: Tafadhali uwasamehe ndugu zako makosa yao mabaya na maovu yote waliyokutendea.’ Sasa basi, tafadhali usamehe uovu tuliokutendea sisi watumishi wa Mungu wa baba yako.” Yosefu alipopata ujumbe huu, alilia. 18Kisha ndugu zake wakamjia, wakainama mpaka chini mbele yake, wakasema, “Tazama, sisi tu watumishi wako.” 19Lakini Yosefu akawaambia, “Msiogope, je, mimi ni badala ya Mungu? 20Nyinyi mlitaka kunitendea vibaya, lakini Mungu alikusudia mema ili watu wengi wapate kuwa hai kama mwonavyo leo. 21Haya, msiogope. Mimi nitawapeni chakula pamoja na watoto wenu.” Basi akawafariji na kusema nao vizuri.

Kifo cha Yosefu
22Yosefu akaendelea kukaa katika nchi ya Misri pamoja na jamaa yote ya baba yake. Aliishi kwa muda wa miaka 110. 23Yosefu alijaliwa kuwaona watoto na wajukuu wa mwanawe Efraimu, na pia kuwapokea kama wanawe watoto wa Makiri mwana wa Manase.
24Baadaye Yosefu aliwaambia ndugu zake, “Mimi sasa ninakaribia kufa. Lakini Mungu hakika atawajia kuwasaidia. Atawatoa katika nchi hii na kuwapelekeni katika nchi aliyowaapia Abrahamu, Isaka na Yakobo.” 25Kisha Yosefu akawaapiza wana wa Israeli, akisema, “Mungu atakapowajia kuwasaidia, hakikisheni kwamba mmeichukua mifupa yangu kutoka huku.”
26Basi, Yosefu akafariki kule Misri, akiwa na umri wa miaka 110. Nao wakaupaka mwili wake dawa usioze, wakauweka katika jeneza kule Misri.
Mwanzo50;1-26
Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Tuesday 28 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo49...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Asante Mungu wetu Baba Yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi,Mfalme wa Amani,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...

Tunashukuru na kukusifu daima,Hakuna wa kufanana nawe,Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho...Tazama jana imepita Baba wa Mbinguni Leo ni siku mpya na Kesho ni sikunyingine Jehovah..!!!Asante kwa ktuchagua kuiona tena Leo hii Baba Mungu, Umetupa Neema/Rehema hii Mfalme wa Amani, si kwamba sisi ni watenda mema sana, kwamba ni wazuri sana,si kwamba wajuaji na wenye nguvu hapana si kwa nguvu/utashi wetu Baba..Bali ni kwa mapenzi yako..
Tunaomba ukaibariki siku hii Baba ..ikawe yenye kukupendeza wewe, Amani na Upendo..Baba Tubariki Tuingiapo/Tutokapo,vyombo vya usafiri,tutembeapo hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!! 
Vilaji/vinywaji na vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase na Damu ya Mwanao, Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo..Ukatutakase Miili na Akili zetu, Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda..
Utusamehe pale tulikwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni..Nasi utupe Neema ya kuweza kuwasamehe wengine..
Baba ukwaguse/kuwaponya wote wanaopitia Magumu/Majaribu, Wagonjwa, Wenye Shida/Tabu,Waliovifungoni Baba ukawafungue na ukaweke huru kimwili na kiroho.. 

1Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni,
ambao hautikisiki bali wabaki imara daima.
2Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima,
ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake,
tangu sasa na hata milele.[Zaburi 125:1-2]

Baba ukawabariki na kuwapa Neema ya kukujua zaidi na Kutembea nawe watoto wetu, familia na wote wakutafutao

10Wanaokujua wewe, ee Mungu hukutegemea,
wewe Mwenyezi-Mungu huwatupi wakutafutao.
11Mwimbieni sifa Mwenyezi-Mungu akaaye Siyoni.

Yatangazieni mataifa mambo aliyotenda![Zaburi 9:1o-11]

Sifa na Utukufu ni kwako Daima..
Tunajinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Muumba wetu.. Tukiamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu..
Amina..!!
Mungu awabariki.

Yakobo anawabariki wanawe

1Yakobo akawaita wanawe, akasema, “Kusanyikeni pamoja niwaambieni mambo yatakayowapata siku zijazo.
2“Kusanyikeni msikie, enyi wana wa Yakobo,
nisikilizeni mimi Israeli, baba yenu.
3“Wewe Reubeni ni mzaliwa wangu wa kwanza,
nguvu yangu na tunda la ujana wangu.
Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu.
4“Wewe ni kama maji ya mafuriko.
Lakini hutakuwa wa kwanza tena,
maana ulipanda kitandani mwangu mimi baba yako,
wewe ulikitia najisi;
naam wewe ulikipanda!
5“Simeoni na Lawi ni ndugu:
Silaha zao wanatumia kufanya ukatili,
6lakini mimi sitashiriki njama zao;
ee roho yangu, usishiriki mikutano yao,
maana, katika hasira yao, walimuua mtu,
kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.
7“Nalaani hasira yao maana ni kali mno,
na ghadhabu yao isiyo na huruma.
Nitawatawanya katika nchi ya Yakobo,
nitawasambaza katika nchi ya Israeli.
8“Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu.
Adui zako utawakaba shingo;
na ndugu zako watainama mbele yako.
9“Wewe Yuda, mwanangu, ni kama mwanasimba
ambaye amepata mawindo yake akapanda juu.
Kama simba hujinyosha na kulala chini;
simba mwenye nguvu, nani athubutuye kumwamsha?
10“Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda,
wala bakora ya utawala miguuni pake,
mpaka atakapofika yule ambaye ni yake;49:10 yule ambaye ni yake: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
ambaye mataifa yatamtii.
11“Atafunga punda wake katika mzabibu
na mwanapunda wake kwenye mzabibu bora.
Hufua nguo zake katika divai,
na mavazi yake katika divai nyekundu.
12“Macho yake ni mekundu kwa divai,
meno yake ni meupe kwa maziwa.
13“Zebuluni ataishi sehemu za pwani,
pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli.
Nchi yake itapakana na Sidoni.
14“Isakari ni kama punda mwenye nguvu,
ajilazaye kati ya mizigo yake.
15“Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema,
na kwamba nchi ni ya kupendeza,
akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo,
akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti.
16“Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake,
kama mojawapo ya makabila ya Israeli.
17“Atakuwa kama nyoka njiani,
nyoka mwenye sumu kando ya njia,
aumaye visigino vya farasi,
naye mpandafarasi huanguka chali.
18“Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe!
19“Gadi atashambuliwa na wanyanganyi,
lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia.
20“Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi,
naye atatoa chakula kimfaacho mfalme.
21“Naftali ni kama paa aliye huru,
azaaye watoto walio wazuri.49:21 azaaye … wazuri: Au naye huimba nyimbo nzuri.
22“Yosefu ni kama mti uzaao,
mti uzaao kando ya chemchemi,
matawi yake hutanda ukutani.
23“Wapiga mishale walimshambulia vikali,
wakamtupia mishale na kumsumbua sana.
24“Lakini upinde wake bado imara,
na mikono yake imepewa nguvu,
kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,
kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli;
25“kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia,
kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki;
upate baraka za mvua toka juu mbinguni,
baraka za maji ya vilindi vilivyo chini,
baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.
26Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele,
ziwe bora kuliko vilima vya kale.
Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake.
27“Benyamini ni mbwamwitu mkali;
asubuhi hula mawindo yake,
na jioni hugawa nyara.”
28Hayo ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hayo ndiyo maneno aliyowaambia baba yao alipowabariki, kila mmoja wao kama alivyostahili.

Kifo cha Yakobo

29Kisha Israeli akawaagiza wanawe hivi, “Mimi karibu nife na kujiunga na watu wangu. Nizikeni pamoja na wazee wangu katika pango lililoko shambani mwa Efroni Mhiti, 30kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia. 31Huko ndiko walikozikwa Abrahamu na mkewe Sara; huko ndiko walikozikwa Isaka na mkewe Rebeka; na huko ndiko nilikomzika Lea. 32Shamba hilo na pango lake lilinunuliwa kwa Wahiti.”
33Yakobo alipomaliza kuwausia wanawe, aliirudisha miguu yake kitandani, akatoa roho akajiunga na wazee wake.
Mwanzo49;1-33

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Monday 27 March 2017

Mahojiano na Dj D - Ommy ndani ya Kilimanjaro Studios U.S.A



Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.

Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.

Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2

Karibu usikilize

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo48...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu kwa mema mengi aliyotutendea/anayoendelea kututenda..

Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake. Utapata matunda ya jasho lako, utafurahi na kupata fanaka. Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako; watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako. Naam, ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako. Uishi na hata uwaone wajukuu zako! Amani iwe na Israeli!
Mtakatifu Mtakatifu Mtakati.. Baba Wa Mbinguni,Muumba wetu,Mungu wetu,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!!! Wewe ni Mwanzo wewe ni Mwisho Hakuna wa kufanana nawe..
Asante kwa kutuchagua  na kutupa tena Kibali cha kuiona Leo hii Baba wa Mbinguni..Tunaanza siku/wiki hii nawe Mungu wetu, Ukaibariki katika Kazi zetu,Biashara,Masomo, Vilaji/Vinywaji,Tuingiapo/Tutokapo, Hatua zetu ziwe nawe Mfalme wa Amani..
Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda..Ukatufanye chombo chombo chema na ukatutumie sawasawa na Mapenzi yako Yahweh..!!

Usiache Mguu wetu ukasogezwa Baba wa Mbingu, Utupe Afya njema,Akili ya kujitambua/kutambua Baba..Ukabariki ridhiki zetu Baba ziingiapo/zitokapo Mfalme wa Amani..
Utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Mfalme wa Amani
Nasi tupe Neema ya kuweza kusameheana Baba..
Baba wa Mbinguni Ukawaguse/Kuwaponya wote wanaopitia Magumu/Majaribu,Vifungo vyovyote vya mwovu na uonevu Baba,Wagonjwa,Wenye Shida/Tabu, Wafiwa wakawe mfariji wao Baba..
Tunajinyenyekeza na kujiachilia mikononi mwako Jehovah..!
Sifa na utukufu ni wako, wema na fadhili ni zako..
Upendo na Furaha vipo kwako..Uponyaji na Amani vipo nawe Yahweh..!!

Tunashukuru na Kuamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu..
Amina...!!
Mungu awabariki Sana.




Yakobo anawabariki Efraimu na Manase

1Baada ya hayo, Yosefu alipewa habari kwamba baba yake ni mgonjwa. Hivyo, akawachukua wanawe wawili, Manase na Efraimu, akaenda nao kwa baba yake. 2Yakobo alipofahamishwa kwamba mwanawe Yosefu amefika kumwona, akajitahidi kuinuka, akaketi kitandani. 3Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu mwenye nguvu alinitokea nilipokuwa kule Luzu katika nchi ya Kanaani, akanibariki. 4Aliniambia, ‘Tazama, nitakufanya uwe na wazawa na uongezeke; nitakufanya uwe babu wa jamii kubwa za watu. Ardhi hii nitawapa wazawa wako, waimiliki milele.’” 5Yakobo akaendelea kusema, “Wanao wawili uliowapata hapa Misri kabla sijafika, ni wanangu; Efraimu na Manase watakuwa wangu kama walivyo Reubeni na Simeoni. 6Lakini, watoto utakaopata baadaye watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao. 7Taz Mwa 35:16-19 Naamua hivyo kwa sababu ya mama yako, Raheli. Nilipokuwa narudi kutoka Padani yeye alifariki katika nchi ya Kanaani, tukiwa karibu kufika Efratha, akaniachia huzuni. Basi, nikamzika papo hapo, kando ya njia iendayo Efratha, yaani Bethlehemu.”
8Israeli alipowaona wana wa Yosefu, akamwuliza, “Ni akina nani hawa?” 9Yosefu akamjibu baba yake, “Hawa ni wanangu alionijalia Mungu nikiwa huku.” Israeli akasema, “Tafadhali, walete karibu nipate kuwabariki.” 10Macho ya Israeli yalikuwa hayaoni vizuri kwa sababu ya uzee. Basi, Yosefu akawasogeza wanawe karibu na baba yake, naye akawabusu na kuwakumbatia. 11Kisha Israeli akamwambia Yosefu, “Sikutazamia kuuona uso wako tena; lakini, kumbe, Mungu amenijalia hata kuwaona watoto wako!” 12Hapo Yosefu akawaondoa wanawe kwenye magoti ya baba yake, kisha akainama kwa heshima. 13Yosefu akawainua wanawe wawili, Efraimu katika mkono wake wa kulia, akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa baba yake, na Manase katika mkono wake wa kushoto, akimwelekeza kwenye mkono wa kulia wa baba yake, akawasogeza kwa babu yao. 14Lakini Israeli akaipishanisha mikono yake: Mkono wake wa kulia akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, ingawa alikuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza. 15Kisha Israeli akambariki Yosefu, akisema,
“Mungu ambaye babu zangu
Abrahamu na Isaka walimtii maishani mwao,
Mungu ambaye ameniongoza maishani mwangu hadi leo,
16na malaika ambaye aliniokoa katika mabaya yote,
na awabariki vijana hawa!
Jina langu na majina ya wazee wangu, Abrahamu na Isaka,
yadumishwe katika vijana hawa;
nao waongezeke kwa wingi duniani.”
17Yosefu alipoona kwamba baba yake ameuweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Efraimu hakupendezwa. Basi, akaushika mkono wa baba yake, akitaka kuuondoa juu ya kichwa cha Efraimu auweke juu ya kichwa cha Manase. 18Akamwambia baba yake, “Sivyo, baba! Huyu hapa ndiye mzaliwa wa kwanza. Tafadhali, uweke mkono wako wa kulia juu ya kichwa chake.” 19Lakini baba yake akakataa, akisema, “Najua, mwanangu, najua. Wana wa Manase pia watakuwa taifa kubwa na mashuhuri. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, na wazawa wake watakuwa mataifa mengi.” 20Taz Ebr 11:21 Basi, Israeli akawabariki siku hiyo, akisema,
“Waisraeli watayatumia majina yenu kubarikia,
watasema, ‘Mungu akutendee mema kama Efraimu na Manase!’”
Ndivyo Israeli alivyomweka Efraimu mbele ya Manase.
21Kisha Israeli akamwambia Yosefu, “Kama uonavyo, mimi niko karibu kufa. Hata hivyo, Mungu atakuwa pamoja nanyi, na kuwarudisheni katika nchi ya babu zenu. 22Zaidi ya hayo, nimekupa wewe, wala si ndugu zako, eneo moja milimani,48:22 eneo moja milimani: Kiebrania: Shekemu. nililowanyanganya Waamori kwa upanga na upinde wangu.”
Mwanzo48;1-22

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Sunday 26 March 2017

Natumaini Juma pili Ilikuwa/Inaendelea Vyema;Happy Mothers Day..Burudani-10,000 Reasons (Bless the Lord) ,I Give You My Heart | Hillsong ,I Need You More




Wapendwa/Waunngwana Natumaini mmekuwa/Mnendelea  na wakati mzuri Jumapili ya Leo....
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea katika yote yaliyo mema..Awape sawasawa na Mapenzi yake..
Hapa tulipo Leo tunasheherekea Siku Ya Mama.."Happy Mothers Day" Kwa Mama yangu Mpendwa na Nguzo yangu,
kwangu na Wamama wote..Mungu aendelee kuwabariki na kufurahia uzao wenu..!!
Mungu akawajaalie wote wanaotafuta watoto, watoto hao wakawe Baraka kwao na Jamii pia...
Mungu akabariki vizazi vyetu, watoto wetu wakamjue Mungu na wawe Baraka kwetu na Jamii pia..
Sifa na Utukufu ni kwako Mungu..

Neno La Leo;Waroma 8:18-39



Utukufu ujao
18Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe kama tukiyalinganisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu. 19Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake. 20Kwa maana, viumbe viliwekwa katika hali ya kutojiweza kabisa, si kwa hiari yao, ila vilifanywa hivyo kwa mapenzi ya Mungu. Hata hivyo yapo matumaini, 21maana hivyo viumbe navyo vitaokolewa kutoka katika utumwa wa uharibifu, vishiriki uhuru mtukufu wa watoto wa Mungu. 22Kwa maana tunajua kwamba mpaka hivi sasa, viumbe vyote vinalia kwa maumivu kama ya kujifungua mtoto. 23Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe. 24Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa. Lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kile ambacho tayari anakiona? 25Kama tunakitumaini kile ambacho hatujakiona bado, basi, tunakingojea kwa uvumilivu.
26Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka. 27Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu.
28Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kadiri ya kusudi lake. 29Maana hao aliowachagua tangu mwanzo, ndio aliowateua wapate kufanana na Mwanae, ili Mwana awe wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30Basi, wale ambao Mungu aliwateua ndio hao aliowaita; na hao aliowaita ndio hao aliowafanya kuwa waadilifu na hao aliowafanya waadilifu ndio hao aliowashirikisha pia utukufu wake.
Upendo wa Mungu
31Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga? 32Mungu hakumhurumia hata Mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote? 33Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu mwenyewe huwaondolea hatia! 34Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka kwa wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea! 35Ni nani awezaye kututenga na upendo wa Kristo? Je, ni taabu, au dhiki, au mateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, au hatari, au kifo? 36Taz Zab 44:22Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:
“Kwa ajili yako, twakikabili kifo kutwa kucha;
tunatendewa kama kondoo wa kuchinjwa.”
37Lakini, katika mambo haya yote, tumepata ushindi mkubwa kwa msaada wake yeye aliyetupenda. 38Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; 39wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN):










"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Friday 24 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo47...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tumshukuru Mungu kwa Leo hii.Baba wa Mbinguni,Mfalme wa Amani,
Muumba wetu,Muumba Mbingu Na Nchi,Mungu usiyelala wala kunsinzia,Mungu unayejibu na Kubariki,Mungu unayesamehe,wewe ni Apha na Omega...
Tazama Baba Jana imepita Leo ni siku mpya na Kesho ni siku nyingine Mfalme wa Amani..Tunajinyenyekeza mbele zako Muumba wetu ,Tunakushukuru na kukutukuza Baba.. Tunasema asante Jehovah kwa Kibali ulichotupa Baba cha kuiona Leo hii,Tunaomba ukatuongoze na Kuibariki siku hii na Tuanze nawe Baba katika yote..Tuingiapo/Tutokapo,Vilaji/Vinywaji,Vyombo vya usafiri na tutembeapo,Hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!!
Ukabariki kazi zetu Baba, Biashara,Masomo,Vyote tunavyoenda Kugusa/Kutumia tunaomba ukavitakase kwa Damu Ya Mwokozi wetu Bwana wetu Yesu Kristo iliyomwagika ili sisi tupate kupona..
Ukatutakase Miili yetu na Akili zetu Baba..
Ukabariki Ridhiki zetu ziingiapo na zitokapo,Ukatufanye chombo chema na tukatumike sawasawa na Mapenzi yako Baba Mungu..
Utusamehe pale tulipokwenda kinyume nawe Baba..
Nasi ukatupe Neema ya kusameheana..
Ukawaguse na kuwaponya wote Wanaopitia Magumu/Majaribu,Shida/Tabu..Wagonjwa,Waliokata tamaa,Waliokataliwa na Wafiwa wakawe mfariji wao..


Tena jambo hili lasemwa pia: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko.” Basi, hiyo ahadi ya kuingia bado ipo, maana wale waliohubiriwa Habari Njema pale awali walishindwa kuingia humo kwa sababu walikosa kutii. Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.” Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine. Kwa hiyo, basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu. Maana, kila aingiaye mahali pa pumziko la Mungu atapumzika kutoka katika kazi yake kama vile pia Mungu alivyopumzika kutoka kazi yake. Basi, tujitahidi kuingia katika pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwetu atakayekataa kutii kama walivyofanya wao. Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu. Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake yeye ambaye kwake tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu. Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu. Huyu Kuhani Mkuu wetu anaelewa kabisa unyonge wetu; yeye mwenyewe alijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi. Basi, na tukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida.


Asante Mungu kwa hapa tulipo tunaomba Baba ukaibariki hii Nchi na Mfalme wa Amani ukatawale hapa tulipo...Baba ukaibariki na kutawala Tanzania,Afrika na Dunia yote..Amani yako na mkono wako ukawaguse na kuwaongoza wanaotuongoza wapate kutuongoza katika haki na kweli..Upendo,Fadhili,Umoja,Kweli, Hekima na Busara zinatoka kwako...
Utupe Neema ya kutambua/kujitambua,Roho mtakatifu akatuongoze kwenye Kunena/Kutenda...

Mwenyezi-Mungu asipoijenga nyumba, waijengao wanajisumbua bure. Mwenyezi-Mungu asipoulinda mji, waulindao wanakesha bure.[Zaburi 127:1]

Tunajiachili mikononi mwako Baba,Sifa na Utukufu ni kwako Baba..Tunashukuru na kuamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu ...
Amina...!!!!
Mungu awabariki.

1Basi, Yosefu akaenda kwa Farao, akamwambia, “Baba yangu na ndugu zangu pamoja na kondoo, ng'ombe na mali yao yote, wamefika kutoka nchi ya Kanaani. Sasa wako katika eneo la Gosheni.” 2Yosefu alikuwa amewachukua ndugu zake watano, akawajulisha kwa Farao. 3Farao akawauliza, “Kazi yenu ni nini?” Wakamjibu, “Bwana, sisi watumishi wako ni wachungaji, kama walivyokuwa babu zetu.” 4Kisha wakamwambia Farao, “Sisi watumishi wako tumekuja kukaa kama wageni humu nchini kwa kuwa njaa ni kali huko Kanaani na hakuna tena malisho kwa mifugo yetu. Hivyo, bwana, tunakuomba, sisi watumishi wako, uturuhusu kukaa katika eneo la Gosheni.” 5Farao akamwambia Yosefu, “Baba yako na ndugu zako wamekujia wewe. 6Nchi yote ya Misri iko chini yako; wape baba yako na ndugu zako sehemu bora ya nchi hii. Waache wakae katika eneo la Gosheni. Na iwapo unawafahamu watu stadi miongoni mwao, wateue wawe waangalizi wa mifugo yangu.”
7Kisha, Yosefu akamleta baba yake Yakobo kumwamkia Farao; naye Yakobo akampa Farao baraka zake. 8Farao akamwuliza Yakobo, “Umri wako ni miaka mingapi?” 9Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.” 10Kisha Yakobo akambariki Farao, akaondoka. 11Basi, Yosefu akawapa baba yake na ndugu zake eneo la Ramesesi lililo bora kabisa katika nchi ya Misri, liwe makao yao, nao wakalimiliki kama alivyoagiza Farao. 12Yosefu akawa anawapatia chakula baba yake, ndugu zake na jamaa yote ya baba yake kulingana na idadi ya watu waliowategemea.

Usimamizi wa Yosefu

13Baadaye chakula kiliadimika kabisa nchini kote. Njaa ilikuwa kali sana hata ikawafanya watu wote katika nchi ya Misri na ya Kanaani kudhoofika. 14Yosefu akakusanya fedha yote ya nchi ya Misri na Kanaani kutokana na nafaka waliyonunua, akaipeleka fedha hiyo ikulu kwa Farao. 15Baada ya watu wote wa nchi ya Misri na Kanaani kutumia fedha yao yote Wamisri wote walimjia Yosefu na kumwambia, “Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele ya macho yako? Tazama, sasa fedha yetu imekwisha!” 16Yosefu akawaambia, “Kama fedha yenu imekwisha, basi nipeni mifugo yenu, nami nitawapa nafaka.” 17Ndipo wakamletea Yosefu mifugo yao: Farasi, ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda, naye akawapa chakula. Mwaka huo Yosefu akawa anawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote.
18Mwaka uliofuata wakamjia tena na kumwambia, “Bwana, ukweli ni kwamba fedha yetu yote imekwisha, na wanyama wetu wamekuwa mali yako. Sasa, bwana, sisi watumishi wako hatuna chochote tunachoweza kukupa isipokuwa miili yetu na mashamba yetu. 19Ya nini sisi tufe mbele ya macho yako na mashamba yetu yaharibike? Utununue sisi pamoja na mashamba yetu, tuwe watumwa wa Farao, mradi tu utupe chakula. Tupe nafaka, tusije tukafa; utupe na mbegu kwa ajili ya mashamba yetu.”
20Hivyo Yosefu akainunua nchi yote ya Misri iwe mali ya Farao. Kila Mmisri alilazimika kuuza shamba lake, kwa jinsi njaa ilivyokuwa kali. Nchi yote ikawa mali ya Farao, 21na Yosefu akawafanya watu kuwa watumwa,47:21 akawafanya … watumwa: Kiebrania na Septuaginta “akawahamishia mijini”. kutoka pembe moja hadi pembe nyingine ya nchi ya Misri. 22Ardhi ambayo Yosefu hakuinunua ni ile iliyomilikiwa na makuhani. Hao hawakulazimika kuiuza ardhi yao kwani waliishi kwa posho maalumu waliyopewa na Farao. 23Kisha Yosefu akawaambia watu, “Tazameni, nimekwisha wanunua nyinyi nyote na mashamba yenu kuwa mali ya Farao. Mtapewa mbegu nanyi mtapanda mashamba yenu. 24Wakati wa mavuno, sehemu moja ya tano mtampa Farao. Sehemu nne zitakazobaki zitakuwa mbegu na chakula kwa ajili yenu na jamaa zenu na watoto wenu.” 25Wakamjibu, “Bwana, umeyaokoa maisha yetu! Kwa vile umetuonesha wema wako, sisi tutakuwa watumwa wa Farao.” 26Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo nchini Misri: Kila raia lazima atoe sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa Farao. Ardhi ya makuhani tu ndiyo haikununuliwa na kufanywa mali ya Farao.

Wosia wa Yakobo

27Basi, watu wa Israeli wakakaa katika eneo la Gosheni nchini Misri. Wakiwa huko, wakachuma mali nyingi, wakazaana na kuongezeka sana. 28Yakobo alikaa katika nchi ya Misri kwa muda wa miaka kumi na saba, hadi alipofikia umri wa miaka 147.
29Wakati wa kufa kwake ulipokaribia, Yakobo akamwita mwanawe Yosefu, akamwambia, “Sasa, kama kweli unanipenda, weka mkono wako mapajani mwangu, uniahidi kwamba utanitendea kwa heshima na haki. Usinizike huku Misri, 30ila unilaze pamoja na babu zangu. Nichukue kutoka Misri, ukanizike katika makaburi yao.” Yosefu akamjibu, “Nitafanya kama ulivyosema.” 31Yakobo akamwambia, “Niapie!” Yosefu akamwapia. Kisha Israeli akainamia upande wa kichwa cha kitanda chake.Mwanzo47;1-31

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

Thursday 23 March 2017

Kikombe Cha Asubuhi;Mwanzo46...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana?
Tuende Mbele za Mungu kwa Shukrani na Utukufu..
Mtakatifu,Mtakatifu, Mtakatifu Baba wa Mbinguni, Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi, Baba yetu ,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo, Yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho,Hakuna wa kufanana naye..
Muweza wa Yote..Sifa na Utukufu ni kwako Daima..
Asante Baba kwa kutupa nafasi hii ya kuendelea kuiona leo hii..
Jana imepita Baba Leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine Mfalme wa Amani Tunaomba Utubariki katika Kazi zetu,Biashara,Masomo.Tuingiapo/Tutokapo,Vyombo vya usafiri na tutembeapo,Hatua zetu ziwe nawe Yahweh..!!
Roho Mtakatifu akatuongoze kwenye kunena/kutenda na maamuzi/kuamua Baba Ukabariki Vilaji/vinywaji na Ukavitakase na Damu ya Bwana wetu Mwokozi wetu Yesu Kristo vyote tunavyoenda kugusa/kutumia,ukatutakase Akili na Miili yetu Jehovah..
Utusamehe pale tulipoenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni..
Nasi utupe Neema ya kuweza kusameheana Mfalme wa Mbingu..
Baba ukawaguse na kuwaponya wote wanaopitia Magumu/majaribu,Wenye Shida/Tabu, Wagonjwa,Wafiwa ukawe mfariji wao..Waliovifungoni Baba ukawaweke huru na kuwaokoa Baba..
Utupe Ridhiki zetu sawasawa na Mapenzi yako Baba wa Mbinguni Uzibariki ziingiapo/zitokapo...
Utukufu ni wako,Sifa na Fadhili zako zadumu Milele..

Tunajiachilia Mikononi Mwako Baba wa Mbinguni,Tukishukuru na Kuamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu..
Amina..!!!
Solomoni alipomaliza kusema sala hiyo yote na ombi lake kwa Mwenyezi-Mungu aliinuka kutoka pale mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, mahali alipokuwa amepiga magoti akiinua mikono yake juu. Alisimama, akawabariki Waisraeli wote waliokuwa wamekusanyika hapo, akisema kwa sauti kubwa, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amewapatia starehe watu wake Israeli, kulingana na ahadi yake. Ametimiza ahadi zake zote njema alizozitoa kupitia kwa mtumishi wake Mose. Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, awe nasi, kama alivyokuwa na babu zetu; tunaomba asituache, wala asitutupe. Yeye aelekeze mioyo yetu kwake, ili tufuate njia zake, tukishika amri zake, maongozi yake na maagizo yake aliyowapa babu zetu. Basi, maneno yangu haya ambayo ni ombi langu mbele ya Mwenyezi-Mungu, yawe karibu na Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mchana na usiku, naye amjalie mtumishi wake, na watu wake Israeli, ili wafanikiwe katika haja zao za kila siku. Nayo mataifa yote ulimwenguni yatajua kwamba kweli Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu; wala hakuna mwingine. Nanyi, muwe waaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, mkifuata masharti yake na kutii amri zake zote kama mnavyofanya hivi leo.”
Mungu awabariki katika yote.


Yakobo anasafiri kwenda Misri


1Basi, Israeli akaanza safari yake pamoja na mali yake yote. Alipofika Beer-sheba, akamtolea tambiko Mungu wa Isaka, baba yake. 2Mungu akaongea na Israeli katika maono usiku, akamwita, “Yakobo! Yakobo!” Yakobo akaitika, “Naam nasikiliza.” 3Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kwenda Misri; utakapokuwa huko, nitakufanya uwe taifa kubwa. 4Mimi mwenyewe nitakwenda pamoja nawe huko Misri na kukurudisha huku. Utakapofariki, mkono wa Yosefu ndio utakaoyafumba macho yako.”
5Basi, Yakobo akaondoka Beer-sheba. Wanawe wakamchukua yeye, watoto wao wachanga pamoja na wake zao katika magari ambayo Farao alipeleka kumchukua. 6Walichukua pia mifugo na mali yao yote waliyokuwa wamechuma katika nchi ya Kanaani, wakaenda Misri. Yakobo aliwachukua wazawa wake wote: 7Wanawe, wajukuu wake wa kiume na wa kike, wote akawaleta Misri.
8Wazawa wa Israeli ambao walikwenda Misri pamoja naye walikuwa Reubeni, mzaliwa wake wa kwanza, 9pamoja na wana wa Reubeni: Henoki, Palu, Hesroni na Karmi. 10Simeoni na wanawe: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli, aliyezaliwa na mwanamke Mkanaani. 11Lawi na wanawe: Gershoni, Kohathi na Merari. 12Yuda na wanawe: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera. (Lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli. 13Isakari na wanawe: Tola, Puva, Yashubu46:13 Yashubu: Au Yobu. na Shimroni. 14Zebuluni na wanawe: Seredi, Eloni na Yaleeli. 15Hao ndio wana ambao Lea alimzalia Yakobo kule Padan-aramu, pamoja na Dina binti yake. Jumla ya wanawe, binti zake na wajukuu wake walikuwa watu thelathini na watatu.
16Gadi na wanawe: Sifioni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli. 17Asheri na wanawe: Imna, Ishva, Ishvi, Beria na Sera, dada yao. Beria na wanawe: Heberi na Malkieli. 18Hawa kumi na sita ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Zilpa, mjakazi ambaye Labani alimpa Lea, binti yake.
19Raheli alimzalia Yakobo wana wawili: Yosefu na Benyamini. 20Huko Misri, Asenathi, binti Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili: Manase na Efraimu. 21Wana wa Benyamini walikuwa Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi. 22Watu hao kumi na wanne ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Raheli, mkewe.
23Dani na Hushimu, mwanawe. 24Naftali na wanawe: Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu. 25Hao saba ni watoto na wajukuu wa Yakobo na Bilha, mjakazi ambaye Labani alimpa binti yake Raheli.
26Jumla ya wazawa wa Yakobo aliokwenda nao Misri, bila kuwahesabu wake za wanawe, ilikuwa watu sitini na sita. 27Huko nchini Misri Yosefu alikuwa amepata wana wawili. Kwa hiyo watu wote wa jamaa ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini.

Yakobo anafika Misri

28Yakobo akamtanguliza Yu
da kwa Yosefu kumwomba waonane huko Gosheni; nao wakafika katika eneo la Gosheni. 29Yosefu akapanda gari lake la farasi, akaenda kumlaki Israeli, baba yake, huko Gosheni. Alipomfikia baba yake, alimkumbatia na kulia kwa kitambo kirefu. 30Israeli akamwambia Yosefu, “Hata nikifa sasa si kitu kwa kuwa nimeuona uso wako na kujua kwamba wewe u hai!” 31Yosefu akawaambia ndugu zake na jamaa yote ya baba yake, “Nakwenda kumwarifu Farao kwamba ndugu zangu na jamaa yote ya baba yangu waliokuwa katika nchi ya Kanaani wamekuja kwangu. 32Nitamweleza kwamba nyinyi ni wachungaji kwani mmekuwa mkichunga mifugo, na kwamba mmewasili pamoja na mbuzi, kondoo, ng'ombe na mali yenu yote. 33Basi, Farao akiwaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’ 34Semeni: ‘Bwana, sisi watumishi wako, ni wafugaji wa mifugo tangu utoto wetu mpaka leo, kwani ndivyo walivyokuwa babu zetu’; semeni hivyo ili mruhusiwe kukaa katika eneo la Gosheni.” Yosefu alisema hivyo kwa sababu kwa Wamisri wachungaji wote wa kondoo ni chukizo.
Mwanzo46;1-34

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.