|
Wapendwa natumai Jumapili ilikuwa/inaendelea vyema.. Mungu azidi kuwabariki katika yote..
Hapa kwetu Jumapili ni njema kabisaa Leo tunaungana na binti yetu mpendwa kwa kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa Siku kama ya leo Mungu alitubariki na kutujaalia mtoto wa kike da'Trace-Sarah Mungu anaendelea kumtunza vyema katika yote.. Mungu yu mwema sana tunamrudishia sifa na utukufu kwakwe Tunamwachilia binti huyu mikononi mwake Baba wa Mbinguni katika yote Aendelee kuwa Baraka kwetu kama wazazi,walezi, Ndugu,Jammaa,Marafiki na Jamii yote Mungu yu Mwema mnoooo Happy Birthday da'Tracey-Sarah.
|
8Mungu asema: “Nitakufunza
na kukuonesha njia unayopaswa kufuata.
Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.
Neno La Leo;Zaburi:32:8-11
9Usiwe mpumbavu kama farasi au nyumbu,
ambao lazima wafungwe lijamu na hatamu,
la sivyo hawatakukaribia.”
10Watu waovu watapata mateso mengi,
bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.
11Furahini na kushangilia kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu;
pigeni vigelegele vya shangwe enyi wanyofu wa moyo.
Bible Society of Tanzania