Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 8 November 2015

EXIM BANK YAFANYA USAILI KWA WANA-DIASPORA NEW YORK


Exim Bank ya Tanzania siku ya Jumamosi ilifanya usaili kwa Diaspora
Watanzania wanaoishi nchini Marekani jijini New York kwa ajili ya
kuwapa kipaumbele Diaspora na hatimaye kuwapatia kazi kwenye Benki
 hiyo yenye makao makuu yake Dar es Salaam, Tanzania.

Akiongea na Vijimambo/Kwanza Production mkuu wa human resources Bwn.
Fredirick Kanga alisema sababu kubwa ya Benki hiyo kuwafanyia usaili
Diaspora ni kutambua mchango wao na mfumo wa uchapa kazi waliouzoea
ili waweze kuutumia nyumbani katika kuleta maendeleo yenye ufanisi
katika sekta mbalimbali kwenye Benki hiyo ambayo kazi kubwa ni kutoa
huduma bora kwa wateja wake.

Bwn. Fredirick Kanga akijibu swali ni kwanini wasitafute wafanyakazi
waliopo Tanzania ambao wengi wao wamemaliza masomo ya juu na hawana
kazi. Bwn. Kanga alisema sababu kubwa ya kuja Diaspora nikutokana na
kutambua mchango mkubwa wa Diaspora na ufanisi wao katika kazi na sio
kweli kwamba hatuajili Watanzania waliopo nyumbani, tunachojaribu ni
kuchanganya ujuzi wa Diaspora na nyumbani ili kufanikisha na hatimae
kutoa  huduma bora na zenye ufanisi mkubwa, huku akisema Benki ya
Exim ndio Benki yenye asilimia ndogo ya makato kwenye akaunti za
wateja wao nchini Tanzania.

Bwn. Kanga alisema tangia tuanze kuasaili Diaspora tumeisha wapatia
kazi wapatao 25 na mwaka jana pekee tuliwapatia nafasi Diapora 6 toka
Uingereza na 3 kutoka nchini Marekani. Baadhi ya Diaspora wanapenda
kurudi nyumbani lakini wanahofia jinsi gani ya kuanza maisha yao mapya
baada ya kukaa ughaibuni kwa muda mrefu. Exim Benki imeliangalia hilo
na ndio sababu kubwa inayowafanya kufanya usaili kwa WanaDiaspora
anaporudi nyumbani anauhakika na kazi yake.
 Kulia ni Paul Rupia kutoka Massachusetts akifanyiwa usaili na
Bwn. Frederick Kanga na  Dinesh Arora (kulia) ambaye ni Chief
Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7,
2015 katika hotel ya Hilton
katikati ya jiji la New York
 Kulia ni Ability Kakama kutoka New York akifanyiwa usaili na
Bwn. Frederick Kanga na  Dinesh Arora (kulia) ambaye ni Chief
Executive Officer wa Exam Bank siku ya Jumamosi Novemba 7,
2015 katika hotel ya Hilton
katikati ya jiji la New York
 Kulia ni Pamela Mgema kutoka Texas akifanyiwa usaili na Bwn.
Frederick Kanga na  Dinesh Arora (kulia) ambaye ni Chief
Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7,
2015 katika hotel ya Hilton
katikati ya jiji la New York
 Kulia ni Peter Mgema kutoka Texas akifanyiwa usaili na Bwn.
Frederick Kanga na  Dinesh Arora (kulia) ambaye ni Chief
Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7,
2015 katika hotel ya Hilton
katikati ya jiji la New York
 Kulia ni Mariam kutoka Columbus, Ohio akifanyiwa usaili na
Bwn. Frederick Kanga na  Dinesh Arora (kulia) ambaye ni Chief
Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7,
2015 katika hotel ya Hilton
katikati ya jiji la New York
Kie Mlay (kulia) kutoka Maryland akiongea jambo na Bwn, Frederick
Kanga wakati wa usaili wa kujaribu kuwaoatia Diapora nafasi za kazi
kwenye Benki ya Exim yenye makao makuu yake jijini Da es Salaam siku
ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la
New York..





Wednesday 4 November 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 2, 2015 (Full Show)


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania.
Wiki hii, tumeangalia zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya UCHAGUZI MKUU 2015


Monday 2 November 2015

[PICHA]: MISA YA MAREHEMU MAMA GREN JUDICA MOSHI Washington DC


Ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali, jana (Novemba mosi 2015) walijumuika na wanafamilia katika misa na kusherehekea maisha ya Mama Gren Judica Moshi iliyofanyika hapa Washington DC

Watoto wawili wa Marehemu Donald na James Moshi, na ndugu wengine, waliungana kwa misa hiyo iliyofanyika alasiri na kufatiwa na chakula cha pamoja

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries Ferdnand Shideko, akiwakaribisha watu waliohudhuria misa hiyo

Mch John Kadyolo akifungua misa kwa maombi

 Wanafamilia

[PICHA] Utambulisho wa kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili Washington DC


Jumamosi,Oktoba 31, Swahili Media Network LLC kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC walitambulisha kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili JAMBO TV SHOW kitakachoonekana kwenye kituo cha Televisheni cha DCTV hapa Marekani.
Pia, Swahili Media Network inaandaa kipindi cha Radio cha Jambo America, kinachosikia kupitia WJFK ambayo ni radio-dada ya WPGC chini ya shirika la CBS Radios

Ratiba kamili ya vipindi kutoka Swahili Media Network, itawajia hivi karibuni

Mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza (katikati) akizungumza na Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi waTanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme na baadhi ya waliohudhuria uzinduzi huo

Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme (wa pili kushoto) ambaye pia alimuwakilisha Mhe Balozi Wilson Masilingi, akimsikiliza mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza

Steven Mghaza akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa kwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi, na mwakilishi wa balozi kwenye hafla hiyo, Swahiba Mndeme
Kushoto ni Meneja mauzo wa CBC Radio R.J Trzaska, mratibu wa Mis Congo na msanii toka congo

Mshereheshaji wa siku hiyo, Grace Ssebo akikaribisha wageni

Wasanii Adele na Frank wakiimba nyimbo za taifa za Marekani na Tanzania, wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo

Mwakilishi wa balozi, ambaye pia ni Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme, akisalimia wageni wakati wa utambulisho

Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme akitambulisha rasmi kipindi hicho

Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska

Mmoja wa washiriki wa Jambo Show Radio inayotayarishwa na Swahili Media Network, Sala Damali

Mwanzilishi wa Jambo Show Steven Mghaza akielezea kipindi hicho kwa wageni waalikwa
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska akielezea umuhimu wa radio kwa jamii yetu na muelekeo wake

Sunday 1 November 2015

IBADA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU GODFREY MNGODO, COLUMBUS, OHIO


Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu
Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini
Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa
kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu
Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na
kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu
mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America,
wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. PICHA NA
KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO
Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin
wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu
Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini
Marekani.
Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.
Pr. Mwakaboma akifanya maombi kwa wanafamilia.
Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake
Alvin.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa Picha zaidi bofya HAPA