Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 25 May 2015

UPENDO NKONE, MIKE KALAMBAY WANOGESHA TAMASHA LA GOSPEL COLUMBUS, OHIO


Mwimbaji wa nyimbo za injili wa Columbus, Ohio Enock Mwamba(kati) akiimba moja ya nyimbo za injili huku akiwashirikisha Mike Kalambay aliyekuja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Upendo Nkone aliyekuja toka Tanzania maalum kunogesha tamasha la Gospel lililofanyika siku Jumapili May 24, 2015 na kuhitimisha tamasha hilo lililokua la siku 3 mjini humo lililoanzia siku ya Ijumaa May 22, 2015.
Mike Kalambay akiimba huku akitoa neno la Mungu kwa Kifaransa kilichochanganyika na lingala huku mchungaji Fayes (kulia) akitafsiri kwa kiingereza na Kiswahili.
Mike Kalambay akiimba moja ya nyimbo za injili kwenye tamasha la gospel lililofanyika siku ya Jumapili May 24, 2015 mjini Columbus, Ohio.
Mike Kalambay toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akishambulia jukwaa na nyimbo za injili.
Mwimbaji mahili wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akiimba moja ya nyimbo zake kwenye tamasha hilo.
Upendo Nkone na mchungaji Donis Nkone wakifuatilia tamasha Mike Kalambay (hayupo pichani).
Mchungaji Donis Nkone na mke wake Nnunu Nkone wakiwa wamepiga magoti wakati Mike Kalambay akiwashukuru kwa kufanikisha ujio wake ikiwa ndio mara ya kwanza kwa yeye kufika mjini humo.
Mike Kalambay(kati) akipata picha ya pamoja na mchungaji Donis Nkone na mkewe Nnunu Nkone mara tu baada ya kumalizika kwa tamasha hilo lililovuta watu mbalimbali wa mataifa tofauti mjini Columbus, Ohio.





Mahojiano na Nape Nnauye Pt II


Karibu katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya mahojiano yetu na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Kazungumzia mambo mbalimbali, hasa suala la uchaguzi

Karibu

Sunday 24 May 2015

Nimatumaini Yangu Jumapili Inaendelea Vyema;Burudani-Turudi miaka ya Nyuma kidogo,[Mchanganyiko]LULU,Mimi yesu,Samson na Delila,Mapambazuko,Nishike Mkono,Kwa Viumbe Vyote.........

Wapendwa Natumaini Jumapili Ilikuwa Njema na inaendelea vyema..
Muendelee na Baraka,Neema,Furaha,Amani itawale nyumbani mwenu...

1Basi, wewe mwanangu, uwe na nguvu katika neema tunayopata katika kuungana na Kristo Yesu. 2Chukua yale mafundisho uliyonisikia nikitangaza mbele ya mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu wanaoaminika, ambao wataweza kuwafundisha wengine pia. 3Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu.4Mwanajeshi vitani hujiepusha na shughuli za maisha ya kawaida, ili aweze kumpendeza mkuu wa jeshi.5Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo. 6Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya kwanza ya mavuno. 7Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uelewe kila kitu.
Neno La Leo;2 Timotheo 2:1-26.
Askari mwaminifu wa Yesu Kristo
8Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri, 9na ambayo kwa sababu yake mimi nateseka na nimefungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa minyororo. 10Kwa hiyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele. 11Usemi huu ni wa kweli:
“Ikiwa tulikufa pamoja naye,
tutaishi pia pamoja naye.
12Tukiendelea kuvumilia,
tutatawala pia pamoja naye.
Tukimkana,
naye pia atatukana.
13Tukikosa kuwa waaminifu,
yeye hubaki mwaminifu daima,
maana yeye hawezi kujikana mwenyewe.”
Mfanyakazi aliyekubaliwa na Mungu
14Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia. 15Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli.16Jiepushe na majadiliano yasiyofaa na ya kipumbavu; kwani hayo huzidi kuwatenga watu mbali na Mungu.17Mafundisho ya aina hiyo ni kama donda linalokula mwili. Miongoni mwa hao waliofundisha hayo ni Humenayo na Fileto. 18Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika. 19Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: “Bwana anawafahamu wale walio wake,” na “Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu.”
20Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: Vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine vya matumizi ya heshima na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida. 21Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema. 22Jiepushe na tamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo, amani, pamoja na watu wote ambao wanamwomba Bwana kwa moyo safi. 23Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi. 24Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu, 25ambaye ni mpole anapowaonya wapinzani wake, kwani huenda Mungu akawajalia nafasi ya kutubu, wakapata kuujua ukweli. 26Hapo fahamu zao zitawarudia tena, wakaponyoka katika mtego wa Ibilisi aliyewanasa na kuwafanya wayatii matakwa yake.
Bible Society of Tanzania














"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

TAMASHA LA GOSPEL CONCERT & CONFERENCE MEMORIAL WEEKEND, COLUMBUS, OH.‏




Mwimbaji mahili wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Upendo Nkone
akiimba moja ya nyimbo zilizowainua watu vitin kwenye tamasha la
Gospel linaloendelea mjini Columbus tangia siku ya Ijumaa May 22 na
kuhitimishwa leo siku ya Jumapili May 24. Tamasha lilihudhuriwa na
watu kutoka mataifa mbalimbali wengine wakiwa wamesafiri kutoka
majimbo ya mbali na Ohio.


Mwimbaji kutoka Jamhuri ya Congo akienda sambamba na mwimbaji
mahili wa nyimbo za injili Upendo Nkone kwenye tamasha la Gospel
lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 6230 Busch Blvd suit 260,
Columbus, OH 43229.


 Nnunu Nkone akitoa neno la Mungu na kuimba kwenye Tamasha la
Gospel lililofanyika
Mchungaji Donis Nkone ambaye ni kaka ya mwimbaji Upendo Nkone
akitoa ukifanya utambulisho kwa bendi iliyokuwa ikitumbuiza nyimbo za
injili kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23,
2015 mjini Columbus.


Mchungaji Donis Nkone na mkewe Nnunu Nkone wakifuatilia tamasha la
Gospel


Bendi ikienelea kupiga moja ya nyiimbo za mwimbaji wa nyimbo za
injili kutoka Tanzania Upendo Nkone.


Bendi ikitumbuiza.


Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.