Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 24 May 2015

TAMASHA LA GOSPEL CONCERT & CONFERENCE MEMORIAL WEEKEND, COLUMBUS, OH.‏




Mwimbaji mahili wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Upendo Nkone
akiimba moja ya nyimbo zilizowainua watu vitin kwenye tamasha la
Gospel linaloendelea mjini Columbus tangia siku ya Ijumaa May 22 na
kuhitimishwa leo siku ya Jumapili May 24. Tamasha lilihudhuriwa na
watu kutoka mataifa mbalimbali wengine wakiwa wamesafiri kutoka
majimbo ya mbali na Ohio.


Mwimbaji kutoka Jamhuri ya Congo akienda sambamba na mwimbaji
mahili wa nyimbo za injili Upendo Nkone kwenye tamasha la Gospel
lililofanyika siku ya Jumamosi May 23, 2015 6230 Busch Blvd suit 260,
Columbus, OH 43229.


 Nnunu Nkone akitoa neno la Mungu na kuimba kwenye Tamasha la
Gospel lililofanyika
Mchungaji Donis Nkone ambaye ni kaka ya mwimbaji Upendo Nkone
akitoa ukifanya utambulisho kwa bendi iliyokuwa ikitumbuiza nyimbo za
injili kwenye tamasha la Gospel lililofanyika siku ya Jumamosi May 23,
2015 mjini Columbus.


Mchungaji Donis Nkone na mkewe Nnunu Nkone wakifuatilia tamasha la
Gospel


Bendi ikienelea kupiga moja ya nyiimbo za mwimbaji wa nyimbo za
injili kutoka Tanzania Upendo Nkone.


Bendi ikitumbuiza.


Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.








Friday 22 May 2015

Siku Kama Ya Leo da'Tracey-Sarah Alizaliwa..!!!!!!!

Siku Kama ya Leo Familia Ya Isaac ilipata Mtoto wa Kike..
Mtoto huyu ni "Da'Tracey-Sarah.."
Hatuna kiasi cha kutosha cha kumshukuru MUNGU wetu kwa jambo hili jema Maishani mwetu.
Tumeuona/Tunaendelea kuuona Utukufu wa MUNGU juu ya Maisha ya Mtoto huyu.
Tunazidi kumuweka Tracey-Sarah mikononi mwako..
Katika Safari yake ya Ujana,Elimu na Maisha yote yawe mikononi mwako.
Azidi kuwa Faraja,Furaha,Shuhuda,Shangwe,Baraka na Amani..Kwetu kama wazazi,Walezi,Ndugu,Jamaa na Marafiki pia.
MUNGU BABA azidi kukutendea katika yote mama Tracey-Sarah
Akupe sawasawa na Matakwa yake, akupe umri mrefu na ufanikishe kazi aliyokutuma hapa Duniani.

Shurani sana kwa Wote tunaoshirikiana katika Malezi,Sala/Dua.
MUNGU azidi kumbariki kila mmoja na amzidishie mara 100 ya pale alipojitoa kwa ajili ya
Maisha ya watoto wetu na sisi pia.

Nina mengi ya kusema lakini kwa leo inatosha.
MUNGU wetu ni mwema sana na Utukufu tumrudishie yeye..!!

Happy Birthday da'Tracey-Sarah[Sendondole].









"Rachel/Isaac/Sandra-Neema/Tracey-Sarah"Tunawapenda tunawapenda wote.

Monday 18 May 2015

Ana kwa Ana na Nape Nnauye Pt I


Karibu kwenye sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano yetu na Katibu Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania.
Ameeleza mengi akianza na Hali ya chama hivi sasa.
KARIBU

Sunday 17 May 2015

Natumaini Jumapili Inaendelea Vyema;Iwe yenye Baraka Na Fanaka,Burudani- Jamaican Gospel Mix....


Natumaini Jumapili inaendelea Vyema,Iwe yenye Hekima,Busara,Heri,Fanaka,Utii,Uaminifu,
Imani na Matumaini...Utukufu tumrudishie Mungu...!!!



1Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu,
bali kwa moyo wako uzishike amri zangu.
2Maana yatakupa wingi wa siku,
maisha marefu na fanaka kwa wingi.
3Utii na uaminifu visitengane nawe.
Vifunge shingoni mwako;
viandike moyoni mwako.


Neno La Leo;Methali 3:1-35

Mawaidha kwa vijana

4 Hivyo utakubalika na kusifika,
mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.
5Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote,
wala usitegemee akili zako mwenyewe.
6Umtambue Mungu katika kila ufanyalo,
naye atazinyosha njia zako.
7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima;
mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.
8Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako,
na kiburudisho mifupani mwako.
9Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako,
na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10Hapo ghala zako zitajaa nafaka,
na mapipa yako yatafurika divai mpya.
11 Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu,
wala usiudhike kwa maonyo yake;
12 maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye,
kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi.
13Heri mtu anayegundua hekima,
mtu yule anayepata ufahamu.
14Hekima ni bora kuliko fedha,
ina faida kuliko dhahabu.
15Hekima ina thamani kuliko johari,
hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.
16Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu;
kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima.
17Njia zake ni za kupendeza,
zote zaelekea kwenye amani.
18Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao;
wana heri wote wanaoshikamana naye.
19Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia,
kwa akili aliziimarisha mbingu.
20Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,
na mawingu yakadondosha umande.

21Mwanangu, zingatia hekima safi na busara;
usiviache vitoweke machoni pako,
22navyo vitakuwa uhai nafsini mwako,
na pambo zuri shingoni mwako.
23Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama,
wala mguu wako hautajikwaa.



24Ukiketi hutakuwa na hofu;
ukilala utapata usingizi mtamu.
25Usiogope juu ya tishio la ghafla,
wala shambulio kutoka kwa waovu,
26Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza;
atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.
27Usimnyime mtu anayehitaji msaada,
ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.
28Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho,
hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo.
29Usipange maovu dhidi ya jirani yako,
anayeishi karibu nawe bila wasiwasi.
30Usigombane na mtu bila sababu
ikiwa hajakudhuru kwa lolote.
31Usimwonee wivu mtu mkatili,
wala usiige mwenendo wake.
32Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu;
lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
33Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu,
lakini huyabariki makao ya waadilifu.
34 Yeye huwadharau wenye dharau,
lakini huwafadhili wanyenyekevu.
35Wenye hekima watavuna heshima,
lakini wapumbavu watapata fedheha.
Bible Society of Tanzania




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.