Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 4 August 2014

Ujumbe wa Leo; kutoka kwa kaka Boniface Ole Precious "Msakatonge"


MWANANGU MPENDWA, NAOMBA UNISIKILIZE KWA UZURII KABLA HUJAOA..


1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama mama kwako, mama kwa wanao na mama kwa familia, tafadhari mwanangu usimuache huyo!

2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi pamoja!

3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa familia!

4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa!

5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!

6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke na mume!

7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa sasa maisha yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa familia yako!

8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza kufanya nao ni kupeana mikono na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio vinginevyo!

9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.

10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au kutimiza wajibu wako.

11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanisha na mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.

12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako na mwambie atimize nusu iliyobaki.

13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.

14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga kama wazee wengi wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga huu, kwani kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume waonekane ni watu wa kawaida sana na sio muhimu kama enzi zetu. Ukijaliwa watoto wape elimu.

15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!

16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.

17. Mwanangu, nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako kama ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.

18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako kama baba wa familia kumbuka pia bado tunaishi na wewe ni mtoto wetu.

19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!

20. NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA MWANANGU. NAKUPENDA!

Ujumbe huu umeandaliwa na Boniface Ole Precious "Msakatonge" Ametoa ruhusa ya ku-share na marafiki.

Shukrani;https://www.facebook.com/SautiYaMwanamke/timeline

Sunday 3 August 2014

Nawatakia JumaPili Njema;Burudani-Living Water Worship Team Yesu U Mwema,Sifa ni kwako,Yehova Mwenye Nguvu Zote..!!!!!!!!


Wapendwa;Nawatakia Jumapili Njema Yenye Kusifu,Kuabudu,Kutukuza,Kushukuru,Kuwa na Matumaini na Kupendana......
5.Naam, na kwa sababu hiyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,6.Na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, 7. Na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.....


Neno La Leo;Waraka Wa Pili Wa Petro;1:1-21

19.Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vema, mpaka kutakapo pambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.20.Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu furani tu.21.Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa MUNGU,Wakiongozwa na roho mtakatifu.






"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima

Friday 1 August 2014

Siku Kama Ya Leo da'Rachelsiwa Alizaliwa;[Happy birthday]Namshukuru MUNGU kwa kila Jambo!!!!!!!

Wapendwa/Waungwana,Siku Kama Ya Leo mimi "Rachel siwa"Nilizaliwa.Namshukuru sana MUNGU wangu kwa yote aliyonitendea/anayonitendea...Yeye ni mwingi wa Rehema,Neema,Baraka,Upendo.Yeye ni kila kitu maishani mwangu..
Nawashukuru Sana Wazazi/Walezi wangu kwa malezi na yote mliyonitendea kulingana na uwezo wenu,Nathamini sana mchango wenu,Kwani malezi yenu hayana mwisho kwangu.
Namshukuru sana Mume wangu katika yote,Tangu pale tulipokutana/tulipotoka mpaka sasa tulipo na tunapoelekea ni kwa Uwezo wa MUNGU tutafika salama.
Niwashukuru sana Watoto wangu wote,wale wa kuwazaa na wakurithi , kwa Faraja,Heshima,Upendo na mengineyo..Najivunia kuwa MAMA.
Nawashukuru sana Dada,Kaka,Mawifi,Mashemeji,Ndugu,Jamaa,Marafiki na Watu wote wanaonifahamu kwa namnamoja au nyingine..Nawapenda Wote.MUNGU azidi kuwabariki na kuwaongezea kila lililo jema.
Asante sana kwa wote walioniletea zawadi,wanaoniombea,walionitumia ujumbe na mnaondelea kuniombea...MUNGUazidi kuwa Bariki na kuwatendea....



Asanteni Sana kwa kunisoma  na MUNGU awabariki Sana.

"Swahili Na Swahili" Pamoja Sana.

Tuesday 29 July 2014

Eid Mubarak Waungwana!!!!!

Nawatakia Eid Njema[Eid Mubarak]Ndugu,Jamaa,Marafiki na Wote .....
Muendelee/Muwe na Wakati Mwema,Amani,Upendo na Furaha.
"Swahili Na Waswahili"Pamoj Sana.

Sunday 27 July 2014

Muendelee na Jumapili Vyema;Burudani-Angela Chibalonza - Yahwe Uhimidiwe na Nyingine...Na Siku Kama Ya Leo Bibi na Bwana Isaac Walifunga Ndoa [Happy Anniversary]


Siku kama ya Leo, Bibi na Bwana Isaac,[Isaacrachel]Tuliungana na kuwa mwili mmoja[Tulifunga Ndoa].
Tuna Mshukuru sana MUNGU katika yote na   tunazidi kujiachilia mikononi mwake.Si kwa uwezo wetu  wala akili zetu.ni Mapenzi yake/Kwa Neema tuu
.


Wapendwa; Natumaini Jumapili inandelea/ilikuwa njema,MUNGU azidi kuwabariki,Kuwainua,Kuwalinda,Kuwaponya,Kuwatendea,Kuwafariji,Kuwapa amani,Kuwapa Furaha,kuwaunganisha na Kuwafunulia.......

Ndipo Samweli akatwaa jiwe,na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri,akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia.

Neno La Leo;1Swamweli:7:1-17
Hivyo wafilisti walishindwa,wasiingie tena  ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafiristi siku zote za Samweli..........








"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Wote.

Sunday 20 July 2014

Natumaini JumaPili inaendelea Vyema;Burudani-Swahilli Worship Songs!!!!!

Wapendwa;Natumaini Jumapili  inaendelea vyema,Iwe Yenye Imani,Tumaini,Baraka,Furaha na Amani....

Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani,wakamkuta yule mtumwa ni mzima.

Neno La Leo;Luka Mtakatifu:7:1-10

Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu,aliingia Kapernaumu.......



"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Tuesday 15 July 2014

Siku Kama Ya Leo da'Sandra-Neema Alizaliwa







 Wapendwa/Waungwana;Siku kama ya Leo ,1998.
 Familia ya Isaac,MUNGU alitubariki/Kutujaalia mtoto wa kike.
Sandra-Neema.Umekuwa na Endelea kuwa Baraka kwetu.

Tunamshukuru sana MUNGU kwa baraka hii na Tunazidi kumtukuza katika yote.
Tunayaweka Maisha ya Sandra-Neema mikononi mwake Mungu.

Azidi kukua Kiroho/Kiimani,Kimaadili,Kimo,Kimaarifa.
Azidi kuwa Baraka Kwetu sisi Wazazi naWalezi,Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani,Wakubwa Kwa Watoto na Jamii Nzima.
Shukrani sana Kwa wote tunaoshirikiana katika Malezi,Maombi/Sala/Dua na Katika yote yanayochangia Maisha ya binti yetu.
Mungu Baba azidi kuwabariki na Kuwaonngezea kila lililo jema.


Hongera sana da'Sandra-Neema katika siku yako hii  Muhimu.
Hongera kwa kumaliza vyema GCSE's Na tunakitakia kila la heri katika A-Levels[Sixth Form].
Ukawe kichwa na si Mkia.
Tunakupenda Sana na Tunakuunga mkono katika Safari yako njema ya Maisha.
MUNGU ndiyo kila kitu katika Maisha yako.Ubarikiwe Mno!!!!

Happy birthday Sandra[se-Ndondole].Wako;Mama,Baba,Mdogo wako-Tracey-Sarah.[Isaac Family]
MUNGU wetu ni Mwema Sana.



"Swahili Na Waswahili" Rachel siwa, ninawapenda Wote.