Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 25 March 2014

Monday 24 March 2014

[AUDIO]: Mdau Boniface Makulilo akijadili suala la Scholarship katika kipindi cha NJE-NDANI‏

Mdau Ernest Makulilo ambaye huandika kuhusu masuala ya Scolarship HAPA na pia kutoa video za suala hili HAPA
UNATAKA SCOLARSHIP?
Unajua pa kuzipata?
Unajua namna ya kuzipata?
Masharti yake je?
Makosa yanayofanywa na wengi?
Tofauti ya Scholarships za Undergraduate na Graduates wazijua?
Yapi ya kuchunga wakati wa kutafuta scholarships?
Boniface Makulilo ambaye amenufaika na scholarship hizi na kuandika kuzihusu kwa miaka ipatayo sita anaungana na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kujadili hili.
Kuna mengi mema ya kujifunza.
KARIBU

NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa waAfrika walio NJE na NDANI ya Afrika.

Sunday 23 March 2014

Nawatakia JumaPili yenye Furaha Na Shukrani;Burudani Kutoka- African Mega Praise....!!!!!!

GOD can do Anything, Anytime, Anywhere in His time!!!!!!
Nawatakia JumaPili Yenye,Furaha,Shukrani,Matumaini,Amani na Baraka....

Nitamhimidi BWANA kila wakati,Sifa zake zi kinywani mwangu daima...

Neno La Leo;Zaburi:34:1-12

Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima,Apendaye siku nyingi apate kuona mema?




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday 22 March 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90: Kupotea kwa Air Malaysia na takwimu za usalama wa anga duniani‏

Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011.
Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za
kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi
na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu
kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua
macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama
miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.


Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network
ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya
dunia.



Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea
tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana
wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.


Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90
ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es
Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30
AM).

Tuesday 18 March 2014

IskaJojo Studios; Ilimuhoji Miriam Kinunda Author of Taste of Tanzania Cookbook‏


IskaJojo Studios; Ilimuhoji "Miriam Kinunda" Mwandishi wa kitabu cha mapishi a Taste of Tanzania: Modern Swahili Recipes for the West.
Akieleza historia yake fupi ya kazi na mapishi na mengineo yanayoweza mnufaisha yoyote anayetaka kuandika kitabu na kufanikisha.



Miriam Kinunda - Taste of Tanzania  Na  IskaJoJo Studios 


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Monday 17 March 2014

Boniface Makulilo azungumzia maisha katika jeshi la Marekani kwenye kipindi cha NJE-NDANI‏

Boniface Makulilo alipokuwa katika Jeshi la Maji la Marekani (Navy)
Mtanzania Boniface Makulilo ametumikia Jeshi la Maji (NAVY) hapa
Marekani kwa miaka miwili na sasa ni mwanajeshi mstaafu (Veteran)

Amezungumza
na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kuhusu maisha yake ya jeshini na
namna ambavyo watu toka nje ya nchi wanaweza kunufaika na mafao yaliyopo
jeshini.

Ameeleza mengi ya manufaa ambayo wengi hatuyajui kuhusu maisha katika jeshi hilo.

Karibu uungane nasi

NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa waAfrika walio NJE na NDANI ya Afrika.

Sunday 16 March 2014

Nawatakia JumaPili Njema na Furaha;Burudani kutoka kwa Beatrice Kitauli-YESU Unipendaye[TENZI],Imbombo Inunu mwa JESU na Nyingine!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu Jumapili inaendelea vyema..

Heri kila mtu amchaye BWANA,Aendaye katika njia yake.


Neno La Leo;Zaburi:128:1-6

Tazama,atabarikiwa hivyo,yule amchaye BWANA......





"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.