Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 28 February 2014

[AUDIO]: Mjadala kuhusu Mitandao ya kijamii kutoka Jamii Production


Karibu katika kipindi hiki cha kwanza cha moja kwa moja (Live) kilichorushwa toka studio zetu za Washington DC

Katika kipindi hiki, mjadala ulikuwa juu ya MITANDAO YA KIJAMII.

Washiriki walikuwa Prof Nicholas Boaz. Mwalimu wa Mawasiliano kutoka Chuo kikuu cha Maryland.

Mzee
Emmanuel Muganda. Mtangazaji mkongwe aliyefanya kazi zaidi ya miaka 30
katika Idhaa za Sauti ya Amerika (VOA) na pia Denzel Musumba. Mmiliki wa
Border Media Group ambaye kwa miaka mingi amekuwa akitangaza kupitia
mitandao ya kiJamii

Kwa njia ya Skype tuliungana na Jeff Msangi. Mwandishi, Blogger na mwanaharakati aliyejiunga nasi kutoka Ontario Canada


Na kutoka nchini Tanzania tulimsikia mwakilishi wetu Ahmad James Nandonde aliyeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara na watu wengine.

Karibu sana



NB: Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa sauti katika baadhi ya sehemu za kipindi.

Wednesday 26 February 2014

[AUDIO]: Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...BAJETI KATIKA FAMILIA (Pt II)‏



Photo credits: moneymanagement.org

Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.

Katika kipindi hiki, tumeingia katika sehemu ya pili ya mjadala kuhusu BAJETI KATIKA FAMILIA ambapo mbali na historia ya bajeti, pia tumesisitizwa kuhusu umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.

Wachangiaji studio walikuwa ni Amos Cherehani ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha, Denzel Musumba na Mubelwa Bandio

KARIBU UUNGANE NASI

2014 Women's Day Promo - By TANO Ladies!!!!!!!!!





Monday 24 February 2014

Jikoni Leo;Jee Umeshawahi Kutumia Vitu Hivi?


Waungwana;"Jikoni Leo",Tukumbuke vifaa hivi vya kupikia na Kuhifadhia/Kuwekea Maji  ya Kunywa.
Mimi navijua kama Vyungu/Chungu na Mtungi.

Wewe unavijua kwa jina gani?
Jee Umewahi /Bado Unatumia?

Mtoto wangu Sandra Alipokuwa  mdogo alikuwa anaita Vyungu/Chungu.."KIMBONDO"

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Sunday 23 February 2014

Natumaini J'Pili Inaendelea Vyema;Burudani-Yesu Ni Bwana by E R Mwansasu Chidumule!!!




Natumaini J'Pili inaendelea vyema;Na asubuhi walipokuwa wakipita,waliuona ule mti umenyauka toka shinani.
Neno La Leo;Marko Mtakatifu:11:20-26.

Kwa sababu hiyo nawaambia,Yo yote myaombayo mkisali,aminini ya kwamba mnayapokea,nayo yatakuwa yenu.






"Swahili Na Waswahili"MUNGU  Atubariki Sote.

Saturday 22 February 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?‏


Photo: Mobile88.com

Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya
WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu
bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi
kifupi tu.

Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano
ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni
19 kununua WhatsApp.

Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Monday 17 February 2014

Tano Ladies Na Maadhimisho ya Siku Ya Wanawake Duniani;Tarehe 8.03.2014!!!!!!

Wakiwa na Mhe.Balozi ;Liberata Mulamula
Wakiwa na Mhe.January Makamba
Wenyewe Wanawake wa Shoka Tano Ladies!!!!

"Swahili Na Swahili"Tukiwa na Nia Moja,Pamoja Tunaweza.