Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 2 July 2013

Mswahili wetu Leo; Da'Tolly Ben..Alianzia wapi na yeye ni Nani?


039
Naitwa Akii Tolly Chawachi,najulikana kama Tolly Ben.Mtoto wa sita wa Mchungaji Benjamin Chawachi na Mama mchungaji Hezeline Chawachi.Nimezaliwa kwenye familia iliyosimama katika nguzo ya kumcha Mungu,Upendo,Umoja ,amani na furaha.Nguzo hizi husimamisha maisha yangu.
Tangu nikiwa mtoto, ni mtu wa kufurahi na kucheka wakati wote.Nilijisika vibaya na kuumia nilipoona mtu akiwa na sura ya huzuni.Niliamini kila mtu anapaswa kuwa na furaha,na nilipata shida kuelewa kwanini watu wengine hawawi na furaha.
Muda wa chakula ulikua muda maalum sana kwa familia yetu.kila mtu alikaa mezani kwaajili ya chakula.Tulikula na kufuraia chakula , Baba na Mama siku zote walikuwa na mambo mengi ya kutusimulia na kutuambia ambayo yalifanya tucheke sana na kufurahi.Kila mtu aliupenda muda wa kula na kuungoja kwa hamu.
Ilijengeka kichwani kwangu kwamba wakati wa kula ni wakati wa kufurahi na kucheka.Jambo ambalo lilinijengea mapenzi na chakula na kunifanya nipende kupika na kula chakula kizuri.Sikupenda kula chakula ambacho hakinifurahishi.
Ingawa nilipenda kupika,  sikujua kwamba nilikua na uwezo mkubwa kwenye sanaa ya chakula hadi pale nilipofika kidato cha tatu na kuchagua kusoma somo la chakula na virutubisho kama somo la ziada. Ujuzi wa awali nilioutoa jikoni kwa mama yangu,na uwezo wangu mkubwa jikoni uliongezeka na kukua kwa kasi ndani ya miaka niliyosoma somo hilo. Nilifanya vizuri sana katika somo hilo na kupata alama “A”katika mtihani wa Taifa.
Nilipokua mtu mzima na kuanza kutembea na kula katika nyumba na familia za ndugu, jamaa na marafiki Niligundua ambavyo watu wengi hupungukiwa na ujuzi wa sanaa ya chakula na ufahamu wa virutubisho vya vyakula.Jambo ambalo linachangia familia zao kutokufurahia chakula.
Ili kukuza furaha ya chakula Katika familia za kitanzania,nilianzisha blog rasmi “TOLLYZKITCHEN’’kwa ajili ya kufundisha sanaa ya chakula ,lengo kuu likiwa ni kuwasaidia watanzania kuboresha mapishi yao nyumbani na kuwaelimisha juu ya virutubisho na lishe ili kuleta furaha na vicheko katika familia kila waketipo kula na kuboresha afya zao
Leo,Kupitia “TOLLYZKITCHEN” nawafikia,nawafundisha na kuwaelimisha maelfu ya Watanzania na watu wengine wazungumzao lugha ya Kiswahili kote duniani.


MALENGO
Moja:Kuboresha mapishi nyumbani
Ingawa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kwa vyakula vingi, Ufahamu na ujuzi wa kuandaa chakula Bora chenye ladha nzuri,muonekano wakuvutia na wingi wa virutubisho ni mdogo miongoni mwa watanzania.Jiko hili liko hapa kutatua tatizo hilo
Mbili:Kuielimisha jamii juu ya virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili.
Elimu ndogo juu virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili huwafanya watanzania wengi wale mlo usio kamili,hivyo kusababisha ukosefu wa virutubisho muhim mwilini na kua chanzo cha magonjwa mbalimbali katika jamii.jiko hili hutoa elimu juu ya virutubisho vya chakula na umuhim wake katika mwili.
Tatu:Kukuza matumizi ya bidhaa za chakula zilizosindikwa na kuzalishwa hapa nchini.
Tanzania ni nchi inayozalisha bidhaa nyingi za chakula,bidhaa hizo ni nyingi sana sokoni,lakini Watanzania wengi hupenda kununua na kutumia bidhaa za chakula zitokazo nje ya nchi.Jiko hili linawahimiza watanzania kutumia bidhaa za chakula za hapa nchini kwani bidhaa hozo ni bora na fresh kuliko zile zitokazo nje.
DIRA
Dira ya Tollyzkitchen ni kua jiko linalotoa elimu na mafunzo bora ya upishi,chakula na virutubisho,na kuboresha upishi na ulaji wa virutubisho sahihi vya chakula kwa watanzania na watu watumiao lugha ya Kiswahili.Kuona watanzania wakitumia bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini.
DHIMA
  • Kutoa Elimu na mafunzo ya upishi,chakula na lishe bora kwa kupitia,tovuti ,simu,redio ,runinga ,vitabu na mafunzo kwa vitendo.
  • Kutoa ushauri na maelekezo juu ya chakula na lishe kwa makundi maalum
  • Kutoa Elimu juu ya chakula na virutubisho kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ,kwa kushirikiana na taasisi za elimu
  • Kufundisha na kuelimisha jamii juu ya upishi,vyakula na lishe bora kwa kutumia michezo,mashindano,muziki na sanaa mbalimbali.
  • Kukuza na kuboresha matumizi ya bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini kwa kutoa elimu ya uelewa na utambuzi wa bidhaa bora za chakula.
kumjua/kujua kazi zake ingia;

     "Swahili NA Waswahili" Wanawake Na Maendeleo/Kujituma.

Monday 1 July 2013

Waswahili na Vituko;Teacher Wanjiku: Mwalimu wa Kiswahili





Waungwana;Waswahili wa Kenya na Vituko/Ucheshi...
Si kunausemi kucheka kunaongeza Uhai?..Tucheke Pamoja!!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Tufurahi Pamoja.

Jikoni Leo;Kuku wa kuokwa na Da'Cecy!!!!!



Waungwana;"Jikoni Leo"ni Mapishi ya KUKU wa Kuokwa..
Mengimsina Fuata na Da'Cecy...

Unaweza kupata meengi hapa;Cecy Lyengi


"Swahili NA Waswahili! Pamoja Sana.


Sunday 23 June 2013

NawatakiaJ'Pili Njema Yenye Amani;Burudani-Bahati Bukuku



Wapendwa ;Muwe na J'Pili yenye Baraka,Amani,Upendo na Shukrani....
Maandalio ya moyo ni ya mwanandamu;Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huzipima roho za watu......

Neno La Leo;Mithali:16:1-20;[3]Mkabidhi BWANA kazi zako,Na mawazo yako yatathibitika....

"Swahili NA Waswahili" Nawapenda Wote.

Saturday 22 June 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Oliver Mutukudzi!!!!




Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo ni Oliver  "TUKU" Mutukudzi;
 Maneno mengi sina Burudika tuu..jee anakubamba/kupenda kazi zake?
Twende Soote sasa....

   "Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima.

Sunday 16 June 2013

Nimatumaini yangu J'Pili imekwenda/Inakwenda vyema;Honngereni Wa BABA wote mnaojua Majukumu Yenu!!!!



Natumaini mmekuwa/Mnaendelea   na J'Pili Yenye Baraka,Upendo,Amani,Furaha na Tumaini..
MUNGU akamwambia Ibrahimu,Sarai mkeo,hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jijna lake litakuwa SARA.

Neno La Leo;Mwanzo:17:15-22.Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka,ambaye  Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao...

Hongereni Kina BABA Wote...Nawe usiyekuwa na mtoto na unapenda/hitaji kuitwa/kuwa na Watoto MUNGU Hajakuacha/kukusahau..Usikate Tamaa Soma hili Neno Uone Abrahamu MUNGU alimtendea....


Wakati wa Home work..hapa hakijaeleweka..

Hapa kuna matumaini....


Hapa urafiki..
Kutembea tembea baada ya yote!!!!!



"Swahili NA Waswahili" MUNGU Awabariki 

Friday 14 June 2013

Kuelekea Siku Ya Mtoto Wa Afrika;Da'Tolly Tolly Anauliza;UNALEA WATOTO AU MAYAI?KESHO YAO ITAKUAJE?




Imeandikwa na da'Tolly .....wa TOLLYZKITCHEN

Kama  Unalolote linalohusu Siku Ya Mtoto wa Afrika na unapenda kushiriki nasi usisite kututumia Email;rasca@hotmail.co.uk

kwa Habari na Mambo Meengi  ya Watoto,Wazazi/Walezi.nifuate huku;http://www.watotonajamii.blogspot.co.uk/

   Pia Usisahau kuungana nasi katika kucheza pamoja na watoto wetu..hapa UK siku hiyo tarehe 16 ni Siku  ya BABA..[FATHER'S DAY] Watoto na Wazazi watakuwa na Mambo meengi..
Basi Tukutane wiki inayofuata  J'Mosi ya tarehe 22/06/2013.


Unalea Watoto au Mayai? si Maneno yangu msome da'Tolly.



043
Katika maisha si kila unalolifanya unafanya kwasababu unapenda au unafurahia, wakati mwingine maisha yanatulazimu kufanya mambo Fulani au kujua jambo Fulani kwasababu ni muhimu kwetu au kwasababu jamii inatutaka tujue na kuweza.
Kupika ni moja ya hayo. si kila mtu anapenda kupika, lakini ualisia wa maisha unawalazimu  watu kujua kupika.Kwa maisha yetu ya kiafrika kujua kupika ni jambo la lazima kwa mwanamke,hata ivyo ualisia wa mabadiliko ya maisha karne hii ya 21 yanawalazimu hata wanaume kujua kupika.
Kupika ni jambo la kujifunza kwa wazazi na ndugu wanaokuzunguka katika kukua kwake,ni kitu unachojifunza kila siku ya maisha yako na kwakufanya mazoezi ya kupika mara kwa mara kama sehem ya ushiriki wa kazi za nyumbani.
Wazazi wa siku hizi wanawanyima watoto  nafasi ya kujifunza kupika kwa kushiriki kazi za nyumbani.Familia nyingi zina dada au kaka anaefanya kazi zote za ndani na matokeo yake watoto wengi hufanya kazi ya kuangalia Tv siku nzima na kukaa kwenye viti kama mayai  kwenye trei.
Kuwalea watoto wako kama mayai,kutowashirikisha katika kazi za nyumbani na shughuli zako za biashara na mambo mengine ni kosa kubwa sana.Ni kumnyima mtoto nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali yampasayo kujua kwenye maisha.
Huku jikoni mtoto anatakiwa kushiki kazi ndugo ndogo tangu anapokua mdogo,aanze kwa kutoan vyombo mezani,kufuta meza,kupanga meza,kufagia jiko,kutwanga vitunguu swaumu na mambo madogo madogo kama hayo kutokana na umri wake.
Hapo nyumbani wapangie watoto zamu na taratibu za kufanya kazi za nyumbani.si kupika tu,bali kazi za nyumbani kwa ujumla.
Tulipokuwa wadogo,mama yetu alitupangia zamu na ratiba ya kazi zote,kutofanya kazi katika wakati husika kuliambatana na adhabu ya kufanya kazi hiyo kwa siku tatu  mfululizo kama kazi ya nyongeza,uku wengine wakipumzika.Ratiba ya kazi hizi ilibandikwa nyuma ya mlango wa kabati  jikoni na ilizingatia umri.Ratiba yetu likua na mambo haya:
1.Ratiba ya kuamka kuandaa chai asubuhi
2.Ratiba ya kupika  mchana na usiku
3.Ratiba ya kuosha vyombo,wadogo wanaosha vyombo vya chai asubuhi
4.Ratiba ya kupanga meza(wadogo)
5.Ratiba ya kufuta meza(wadogo)
6.Ratiba ya kusafisha Sebule na jiko
7.Ratiba ya kusafisha vyumba
8.Ratiba ya kusafisha choo na bafu
9.Ratiba ya kufagia nje
10.Ratiba ya kumwagilizia mauwa
11.Ratiba ya kumsaidia mama kwenye biashara
12.Zamu ya kusali na kuongoza ibada ya jioni
042
Zaidi ya ratiba kulikua na kanuni au sharia ambazo zilikua lazima kufuata na kila moja ilikua na adhabu yake pale unapoivunja.
1.Lazima kuoga kabla ya kwenda mezani kupata kifungua kinywa na kabla ya kwenda kupata chakula cha jioni.Usipooga basi hakuna kwenda mezani,ikimaanisha hautakula.
2.Lazima kufua nguo na kupanga kabati kila jumamosi.Usipofanya hivyo jumapili wengine wakipelekwa kutembea,wewe unabaki nyumbani .
3.Home work zote lazima zifanywe kabla ya saa moja jioni,na umpe mama,baba,mtu mkubwa yoyote akague .Usipofanya hivyo mara nyingi adhabu ilikua kufanya maswali mengine kumi kama hayo au anamwambia mwalimu wako akushugulikie shuleni.
4.Kwenda kanisani ni lazima,hili halikua na mjadala na hakukua na namna ya kulikwepa.
5.Hakuna kuangalia Tv wala sinema kabla ya saa nane mchana.Asubuhi ni walkati wa kazi,mapumziko ni Baada ya  Lunch.Adhabu ya kuvunja hili ilikua ni kupewa kazi za kufanya,kwani kukaa unaangalia Tv maana yake huna kazi.Unaambiwa kashone vifungo vilivyotoka kwenye nguo zako,au kafute na kubrashi viatu vyako.
  • Hizi ni baadhi ya ratiba na sharia au kanuni zilizonilea,na kunifanya niwe hivi nilivyo leo.ratiba hizi zilihusisha watoto wote,wakiume na wakike.Kwa ratiba kama hizi mtoto anajifunza kila kitu  na anajifunza kujitegemea kwa kila kitu.
Ifike mahala muone aibu na mjiulize watoto wenu watakua kina baba au kina mama wanamna gani wakikua.Waswahili husema  Samaki mkunje  angali mbichi.Wewe unaengoja Samaki wako aive ndipo umkunje,utatia aibu na utaumbuka.
Pia ni vyema kujua kuwa,ni katika ufanyaji wa kazi hizi unaanza kuona na kutambua uwezo na vipaji vya watoto.Mpishi mzuri utaanza kumuona mapema,wale wanaopenda kusimamia wenzao ndio vipaji vya uongozi hivyo,kuna wale wa maneno mengi ila hawafanyi kazi nao utawajua na uanze kuwasaidia kubadili tabia hizo zisizofaa.
Hapa jikoni watoto wakija lazima niwape kazi yakufanya,kama hakuna kazi basi nampa kiti akae mlangoni(kukwepa ajali) tuongee mawili matatu wakati napika.Kwani najua anapoangalia niachofanya kula jambo anajifunza,na mara nyingi wanakua na maswali mengi juuu ya lile ninalolifanya.
Yangu ni haya tu kwa leo,yaliyobaki kazi kwako.Ukiamua kulea watoto kama mayai  basi endelea ukijua unamuharibia mtoto maisha.
kwa mambo ya mapishi na malezi ingia hapa;http://tollyzkitchen.wordpress.com/