Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 5 May 2013

Tumalizie J'Pili Kwa Kuombeana/Kutiana Moyo;Burudani-MWAMBA WENYE IMARAA na Nyingine!!!!!

Wapendwa;Tumalizie J'Pili hii kwa kuwaombea, Wagonjwa,Wafiwa, Wenzetu  wa Arusha, Wenye shida na Tabu, TANZANIA,AFRIKA,DUNIA.
MUNGU apate kuwalinda,Kuwaponya,kutatua shida zao, Amani iwe juu yao.
Nanyi mkiwa katika kusali,msi payuke-payuke,kama watu wa mataifa;maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

Neno La leo;Mathayo Mtakatifu:6:1-21.

"Swahili Na Waswahili" MUNGU atubari Sana.


Saturday 4 May 2013

Poleni Sana Familia Ya Costa Shirima!!!!!


Ulale kwa Amani Mpendwa wetu COSTA SHIRIMA.Pole  Sana Mke,Watoto,Wazazi,Ndugu,Jamaa na Mrafiki kwa Msiba huu wa Mpendwa wetu  COSTA SHIRIMA.Daima Tutakukumbuka na Kuenzi Mema yote uliyoyatenda.Familia ya ISAAC,Swahili NA Waswahili Blog Tupo Pamoja katika wakati huu Mgumu Kwenu.

Habari kamili,shukrani;http://mrokim.blogspot.co.uk/
MFANYA BIASHARA COSTA SHIRIMA ALIYEDONDOKA  GOROFANI KARIAKOO...



TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.

Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.

Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.


Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.

Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.

Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.

Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika. Timu nzima ya Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo.

Tuesday 30 April 2013

Unazikumbuka hizi?,Mtoto wetu[Everyone's Child],Neria na Nyingine-[kwa Kiswahili]!!!!





Waungwana;Filamu/Hadithi hizi na Nyingine ni zamuda.lakini mimi bado nazipenda na nipatapo muda huwa nazirudia...
Yaani zina mafundisho na Mifano/Yaliyotokea/Yanayoendelea Kutokea katika   Maisha ya kweli katika Jamii.

  Kuna lolote unakumbuka,kukugusa,kukutokea wewe au mtu wa karibu,Kusikia Jee?
       
   
kuona Zaidi ingia;swahiliwood

             "Swahili na Waswahili" Pamoja Daima.

Monday 29 April 2013

Jikoni Leo;Mchele Mmoja mapishi Tofauti!!!


Waungwana;"Jikoni Leo"Mchele mmoja Mapishi Tofauti...Kazi kwako wewe Mpishi.
   "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Sunday 28 April 2013

Muwe Na J'Pili yenye Neema na Imani;Burudani-Rebecca Malope!!!!!!!!









 Wapendwa;Natumaini J'Pili inaendelea vyema...
Muwe na Amani,Baraka,Furaha na Tumaini...

 Upendano wa ndugu na udumu.[2]Msisahau kuwafadhili wageni;maana kwa njia hii wengine wamekaribisha malaika pasipo kujua.
Neno La Leo:Waraka kwa Waebrania:13:1-6..Hata twathubutu kusema BWANA ndiye anisaidiaye,sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?

           "Swahili NA Waswahili" Neema na iwe nanyi Wote.





Saturday 27 April 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Boyz II Men - On Bended Knee,I Swear,Mama na Nyingine!!!!!!!


Waungwana; Chaguo La Mswahili Leo..Mambo ya.. Boyz 2 Men.... Thank you in Advance, On Bended Knee, A song for MAMA ..................... na Nyinginee....
Mhhh palikuwa hapatoshi...Vipi wewe kuna lolote unakumbuka ukisikia/kuangalia nyimbo hizi...Wapi na Nini?

  "Swahili Na Waswahili"  Zilipendwa/Zinapendwa...J'Mosi Njema.

Thursday 25 April 2013

Mitindo Nga'mbo;Fashion Sense TV!!!!!!!







Waungwana, Walioko/Wanaoishi Nga'mbo  Baadhi ya Maeneo Jua limeanzaa..watu watapungua uzito kwa Makoti..hahahhaha.. ...
Vipi wewe hapo ulipo? 
haya niwakati wa kuzunguka zunguka Mjini , Nyama Choma, Kupeleka/Kucheza na Watoto Park na Mengine meengi..Raha tupu!!!


 Na Mitindo ndiyo hiyo Madukani...................



"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima