Thursday 1 November 2012
Wednesday 31 October 2012
Tuesday 30 October 2012
Wanawake Waswahili Wa Coventry,U.K.[WWWCU]Wamtakia Kheri na Baraka da'Maggie!!!!!!!
Watu wa Mapambo[Zay&Rachel] |
Kina kaka/Baba wa Covenrty na da'Esther wakiweka sawa mambo ya Burudani. |
Kina mama wa Coventry wakiandaa chakula |
Wapiga picha wakiongozwa na Mwanamke wa shoka da'Mija [Mrs Manju]kutoka MI-RA COMPANY |
Maombi yaliongozwa na da'Elina[Mrs Ademisoye]
Neno lilitolewa na da'Rachel-siwa [ muke ya Mubena]
kupambwa na kuhakikisha da'Maggie amefika na kuondoka yalisimamiwa na da'Lina[Wifi la Wabongo] |
Mpendwa wetu da'Maggie.
yeye ndiye aliyetukutanisha hapo.Ndugu yangu Maggie watu wote hawa wametoa Muda,Hali na Mali kwa sababu yaMshikamano, Umoja,Utuwema, Fadhili na Upendo wa Kweli............
MUNGU na Azidi kutuongoza.
Picha Zitaendelea usicheze mbaaali.
"Swahili na Waswhili" na "Wanawake wa Shoka"[MI-RA]
Pamoja Daima.....
Sunday 28 October 2012
Siku kama ya Leo da'Jestina George Alizaliwa!!!!!!
Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita Mpendwa wetu Da'Jestina[mamake na Imani] Alizaliwa.
Da'Jestina Tunakutakia kila lililo Jema,Baraka,Amani,Fadhili na Uishi Miaka Mingi na Utimize Malengo Yako.
MUNGU azidi kukutendea na kukulinda kila iitwapo Leo.
Ukitaka kujua mengi kuhusu dada huyu ingiahttp://www.jestina-george.com/
Tumalize J'Pili kwa Amani na Upendo;Burudani-Atta Boafo - Double Double na Nyingine Nyingii!!!!
Wapendwa; Tumalize J'Pili hii Vyema,Tuwe na Amani,Upendo,Umoja,Msamaha,Uvumilivu na Shukrani.
Neno la Leo.Mithali;29:7-9 Mambo haya mawili nimekuomba;Usininyime[matatu]kabla sijafa.Uniondelee ubatili na Uongo;Usinipe umasikini wala Utajiri;Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.............
"Swahili NA Waswahili" MUNGU Atubariki Soooote
Thursday 25 October 2012
TANZIA!!!!!
FAMILIA
YA MAREHEMU MCHUNGAJI MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA
WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MZEE NSUBISI SAMUEL MWAKIPUNDA (MKURUGENZI WA
ZAMANI WA IDARA YA MAELEZO) KILICHOTOKEA SIKU YA JUMATANO TAREHE
24/10/2012.
MIPANGO
YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU PUGU KINYEMWEZI DAR ES SALAAM.
HABARI
ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.
KWA
MAWASILIANO ZAIDI
+255655994499
“BWANA AMETOA BWANA, AMETWAA
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”
AMEN
Tuesday 23 October 2012
Mswahili Wetu Leo; Arba Manillah wa Kukaye Motooooooo!!!!!!!
Waungwana;MSwahili Wetu Leo ni Kaka ARBA MANILLAH.
Ni mwanamuziki anayeishi na kufanya kazi zake Nchini Ujerumani[Chemnitz, Germany].
Arba Alizaliwa na kukulia IRINGA,TANZANIA.
Bendi yake inaitwa "KUKAYE MOTO"
Kujua zaidi kuhusu kaka huyu ingiaKukaye Moto na www.kukayemoto.de Twende sote sasa....
"WANYALUKOLO"......Kihesa,Mkimbizi,Semtema,Ruaha,Ipogolo,Kigonzile,Ilala,Lugalo.....................Dar-es-salaam,Ilala,Mabibo....
"Swahili NA Waswahili" IRINGA TO GERMANY.
Sunday 21 October 2012
Saturday 20 October 2012
Chaguo La Mswahili Leo,Mdumange,Chiwoda,Sindimba,Wamasai na Wagogo.Kiasili Zaidi!!!!!
Waungwana;"Chaguo La Mswahili "Leo kinyumbani/Kiasili Zaidi.
Haya twende sote sasa,Lakini wewe unajua kucheza Ngoma za Asili au Unajua Ndombolo tuu?
Unafikiri ipi Ngoma Nzuri zaidi ya Zote Tanzania?
Ngoma ya kwenu Inaitwaje?
Utamaduni Tanzania unaendelea au Unakufa?...
Mtu Kwao Ungana Nami........"Swahili NA Waswahili" Mkataa Kwao Mtumwa!!!!!!
Thursday 18 October 2012
Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, Nd Omary Mjenga akutana na Balozi wa Marekani Nchini Siera Leone leo.!!!
Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, Nd Omary Mjenga, akipiga picha ya kumbukumbu Pamoja na Balozi wa Marekani Nchini Sierra Leone Bw Michael Owen, alipomtembelea leo na kufanya mazungumzo naye.
Bwana Omary Mjenga akiagana na Mh. Balozi wa Marekani Nchini Siera Leone baada ya kumaliza mazungumzo.
Balozi Michael Owen, aliwahi kuwa Naibu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania mnamo mwaka 2001 hadi 2004.
Wednesday 17 October 2012
Wanaume na Mitindo ya Nywele!!!!!!!!
Waungwana "Wanaume na Mitindo" Leo tuangalie Mitindo ya Nywele, ki-Leo/kisasa..haya Wewe unaionaje? Inakubamba/kuipenda au...
Jee Wanawake mnasemaje baba watoto, Mchumba,Kaka,Mwanao na Mitindio hii, upi umeupenda zaidi?...
Wenyewe Jee kina Kaka,Baba,Mojomba mnatuambiaje?
Mengi sina Nawasikilizawenzangu....
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima...
Kuona picha zaidi, ingia kwenye Kibaraza chetu kipya;http://mitindoafrica.blogspot.co.uk/
Subscribe to:
Posts (Atom)