Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday 11 February 2012

Chaguo la Mswahili Leo-Gere,Warumba Mpoo?kutoka kwa Wana Njenje!!

OMARY MJENGA AKIWA NA FAMILIA YA BALOZI MDOGO WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA MH. CHABAKA KILUMANGA




Kutoka kulia ni Mtoto wa Balozi Mdogo nchini Uingereza anaitwa Maya, anaefuata ni Mwakilishi wa UNOPS Siera Leone Ndugu Omary Mjenga, anaefuata ni Mke wa Balozi Mdogo Uingereza, anaefuata ni Balozi mdogo wa Tanzania Nchini Uingereza Mh. Chabaka Kilumanga, na wa mwisho ni Aziz Msuya mtoto wa Balozi wetu Pretoria Afrika ya kusini.
Mjenga yuko Nchini Uingereza kuhudhuria moja Kikao ambacho kiko ndani ya majukumu yake ya kikazi.

Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog.
Ahsante sana.

Friday 10 February 2012

Harambee ya Msiba wa Mtanzania Mwenzetu,Washington DC.Kutoa ni Moyo!!!

Marehemu Christavina Kusaga Cryor
Familia ya Kusaga inawaomba watanzania wote walioko Marekani na hasa eneo la Washington DC na vitongoji vyake kushirikiana nao katika harambee (fundraising) ili kupata pesa ya mazishi ya mtanzania mwenzetu Christavina Kusaga Cryor aliyefariki February 7, 2012 kwa sarakani ya utumbo.

Marehemu alikuwa akiishi Landover, MD. Ameacha mume na watoto wawili- mvulana wa miaka 4 na msichana wa miaka 2. Alikuwa akisumbuliwa na cancer ya utumbo.

Tafadhali fika tushirikiane kusaidia mume wake na watoto na familia wamzike mpendwa wao. Jumla ya gharama za mazishi ni $11,000, na mpaka sasa tuna $3,000. Tunashukuru kwa waliokwisha saidia.

Harambee itakuwa Jumapili February 12, 2012, kuanzia saa 8.30 mchana (2.30pm).

Anuani ni: 3621 Campus Drive, College Park, MD 20740.

Kwa wale wa mbali au wasioweza kuhudhuria tafadhali tusaidie mchango wako kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing # 255071981. Jina la Account ni Lavorn Cryor. Tafadhali eneza habari hii kwa ndugu na marafiki wote. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu katika wakati huu mgumu.

Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile (240.938.3177); Teddy (301.254.4169); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au Rebecca (202.580.4648).

M/Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen