Sunday, 3 February 2013
Saturday, 2 February 2013
Chaguo La Mswahili Leo;Mchanganyiko-BOZI BOZIANA,Franco&Sam Mangwana,Madilu...Mmmhh..Mooto!!!!!
Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo..Mhhhhh...motoo.mambo mchanganyiko.ya Kitambo kidogo....
Vipi hizi zinakukumbusha nini/wapi?.Zina kubamba/kuzipenda? Au hukupata kuzisikia?...
Twende sote sasaa.....Balobakiee..na Imalobato lembiyeeeh........kusemasema walisema tumechokaaa..Muongo na mulozi ni watu wa kuchomaaaah.......
Kujulikana kumbetabu mwana mbokaaa... Ukiwa shantii kama Mushedo wanashangaaaa....ukitembea peke yako wanasema wewe ndiyo mbayaaaa....Kujulikana kuna mamboooo....Lwambo wetu Franco wandugu eeehhhh.......
Rafiki yake ananiaeeehh...wewe Mangwana ee...usiwafuate endelea jamani eehh...Ukipata Tabu omba kwa MUNGU eeeehhh Alafu MUNGU pekee yeye Milele na Milele eeehhh........
Wewe na mimi kisa gani ayaahh Ndugu nimekosea nini Angalia Makambooo eee....kama kuna mambo unielezee Taratibuuu eeehh kukorofisha mbele ya watu sitakieeeeehh sikia eeeeehhh.........
"Swahili NA Waswahili"Pamoja sana.
Thursday, 31 January 2013
Jikoni Leo,Shaba,Soda Mtungini na.....!!!!!!
Soda za kwenye Mtungi...nimezipata hukooo Ruhuwiko....
Kitu Chipsi na Nyama Choma/kuku..... hapa Diet hakuna...
Waungwana;Jikoni Leo..Mambo kama hayo....
mimi sina meengi..zaidi nasubiri kutoka kwako ..
Umeshawahi Kula shaba/Pilau.Chakula cha Shughulini?...Nini ubaya wake na Nini Uzuri wake?
Karibuni sana kwa Maoni/Ushauli na Kuelimishana kwa upendo.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaana.
Wednesday, 30 January 2013
Watoto Na Mitindo;Pata na Video Hairstyle Slideshow!!!!
Aliye msuka huyu ndiyo aliyekuwa akiwasuka watoto wangu..Nimefurahi kusikia bado yupo na anaendelea vyema na kazi zake kwa watoto...tena anawezana nao haswa...
Waungwana; Mimi naamini watoto wana Mitindo yao..pia wakipendeza wao wenyewe na wazazi tunakuwa na furaha sana..
Si Lazima au si wote wanapenda watoto wasukwe..basi hata kama ana Nywele fupi..kuna Vibanio vyao pia wanapendeza sana......
Nao Watoto kuna Umri wewe mzazi utamchagulia Mitindo ya Nywele lakini kuna Umri mwingine Mmmhh !!...inakuwa kazi ya ziada, Yeye/Wao hutaka hivi nawe unataka hivi..basi ni mabishano tuu..kama wapo wawili huwa wanaangaliana wao na kucheka au kuguna....hahahhaahhah imeshakukuta hii?
Karibuni sana kwa Maoni/Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.....
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
Sunday, 27 January 2013
Natumai mlikuwa na J'Pili yenye Kupendeza;Burudani-Bahati Bukuku-Dunia,Samehe!!!!!!!!!
Wapendwa natumaini mlikuwa na J'Pili yenye kupendeza.....
Tumalize J'Pili hii kwa.....Neno La Leo;Wakolosai;3:18-25;
[18]Ninyi wake,watiini waume zenu,kama ipendezavyo katika BWANA.
[19]Ninyi waume,wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
[20]Ninyi watoto,watiini wazazi wenu katika mambo yote;Maana jambo hili lapendeza katika BWANA
[21]Ninyi akina baba msiwachokoze watoto wenu,wasije wakakata tamaa......Endelea....
"Swahili NA Waswahili" MUNGU awabariki Saana.
Monday, 21 January 2013
Jikoni Leo;Ugandan foods & Cuisines!!!!!!!
Waungwana;Jikoni Leo Tupo Uganda...Pata kujua Mapishi yao na Maandalizi yoote.
Mengi sina ukitaka kujua Uhondo wa Ngomaaa..Ingia Ucheze..
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.
Sunday, 20 January 2013
Wapendwa Nawatakia J'Pili Yenye Ushindi;Burudani-Geraldine Oduor - Wewe ni Mungu na Nyingine Nyingii!!!
Wapendwa Poleni na Snow natumaini hamjambo na kufurahia majira aliyoyaweka MUNGU na kushangilia. Ikiwa snow kama Greenland Mchanga na Joto kama Sahara Baridi kama Himaya Mvua na Radi za Ikweta.Tusilalamike Nawatakia Kila la Kheri.....
Ujumbe huu Wa kutia Moyo Nilitumiwa na Kaka yangu ALEX LUKUNDO Wa hapa COVENTRY .
Nami nimependa kushiriki nanyi NA Kuongezea....Hasa mliokuwa kwenye Hali ya hewa kama hii isiwe sababau ya kukosa Kushiriki IBADA.
Neno La Leo:Mathayo Mtakatifu:6:19-21;Kwakuwa hazina yako ilipo,ndipo utakapokuwapo na Moyo wako.
"Swahili NA Waswahili" MUNGU Awabariki Sana.
Subscribe to:
Comments (Atom)











