Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 12 April 2012

Siku kama ya leo da'Victoria-Ruth Alizaliwa!!!!!!

Siku kama ya leo Bibi na Bwana Malonga wa Tanga,Walipata mtoto wa kike na wakamwita Victoria-Ruth.
Hongereni sana wazazi/Walezi na Mungu awabariki sana.


Hongera sana da'Vick-Ruth kwa kuongezeka,Mungu azidi kukubariki na kukulinda siku zote za maisha yako.
Uwe baraka kwa wazazi/walezi ndugu,jamaa ,marafiki  na watu wote wadogo kwa wakubwa.
Uwe na Wakati mzuri leo na siku zote.MUNGU NI PENDO.


Swali la Kizushi:Wapendwa eti watu wenye kutumia the,thatha badala se au sasa,Athante,ASante,walipokuwa watoto walinyonya vidole sana,walideka,walichelewa kuongea au.......


Karibuni Waungwana!!!!!!

Tuesday, 10 April 2012

Maelfu ya watanzania wajitokeza kumzika Kanumba Jijini Dar !!..pata na [Video]


Safari ya Mwisho ya Mpendwa wetu Kanumba.Sisi Tulikupenda Lakini Mungu amekupenda zaidi.Ulale kwa Amani.
Picha kwa Masaada wa kaka LUKAZA wa http://josephatlukaza.blogspot.co.uk,Ubarikiwe.
Video kwa msaada wa[ Michuzi blog]http://issamichuzi.blogspot.co.uk.Ahsanteni Sana na   Tulie kwa Amani yeye Amekwenda..

Steven Kanumba (kauli yake ya mwisho) [HD]

Monday, 9 April 2012

MAMA KANUMBA KAFIKA DAR NA RATIBA YA MAZISHI KAMA IFUATAVYO!!

 


WAKATI MAOMBOLEZO YA MSIBA YAKIENDELEA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIFIKA KUTOA MKONO WAPOLE  AMBAPO LEO MHESHIMIWA PREZIDAR J.K ALIFIKA NYUMBANI KWA KANUMBA KUTOA MKONO WA POLE, NA KESHO ASUBUHU WAZIRI MKUU MHESHIMIWA PINDA ANATARAJIWA KUFIKA  KUTOA MKONO WA POLE KABLA YA KUELEKEA MKOANI DODOMA KWA AJILI YA BUNGE LINALOANZA JUMANNE
 RATIBA YA MAZISHI IMETOLEWA RASMI AMBAPO MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE KAMA ILIVYOKUWA IMEPANGWA, MAREHEMU ATAAGWA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB AMBAPO KUANZIA SAA 4 SHUGHULI ZA MISA NA KUAGA MWILI ZITAANZA NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI.
R.I.P KANUMBA
Habari hii kutoka http://8020fashions.blogspot.co.uk.

Ahsanteni sana.

Saturday, 7 April 2012

MAMA KANUMBA AONGEA;Mmmmmhh Pole sana Mama!!!!!!

Mama Mzazi wa Kanumba.
Mmmmhh,Pole sana Mama,Mungu akutie nguvu.
Picha na Video,kutoka ;http://bukobawadau.blogspot.co.uk   Ingia hapo kujua zaidi.Ahsanteni sana.

Ulale kwa Amani Kaka Steven Kanumba!!!!!

Steven Kanumba Enzi za Uhai Wake.
Poleni sana Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani,WaTanzani na Wapenzi Woote Wa KANUMBA!!
Sisi tulimpenda sana Lakini Mungu amempenda zaidi,Tulie na Kumshukuru Mungu kwa Kila jambo,Sote ni Wapitaji katika hii Dunia,Mwenzetu Ametangulia,Inauma sana lakini hatuna Jinsi,Tukumbuke na Kuenzi Mema yote aliyoyatenda.Tuwe tayari wakati wote kwani hatujui Siku wala Muda,Tupendane na Tusameheane.Mungu awatie Nguvu Wafiwa katika Wakati huu Mgumu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE NA LIHIMIDIWE MILELE;
AMINA.

Thursday, 5 April 2012

Watoto na Mitindo,Kutoboa/Kutoga Masikio!!!!

Haya Waungwana;Wazazi/Walezi Unaonaje watoto kutoboa/kutoga masikio wakiwa Wadogo?jee Tunawafurahisha au Tunajifurahisha?ni vyema atoboe/kutoga yeye mwenyewe akikua au bora tuwafanyie labda wakikua watatulaum?
Karibuni Sana kwa Maoni na Ushauri.Pamoja!!!!!!