Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 5 February 2012

Nawatakia J'Pili Njema na Burudani-YUMWEMA ANGEL CHOIR

Hali ya Hewa baadhi ya Sehemu iko hivi,Isiwe sababu ya kutokwenda  kwenye Nyumba za ibada Wapendwa,Mungu awabariki sana, na Muwe na J'Pili njema yenye Baraka,Amani na Upendo. Mungu yu Mwema Maishani mwetu,wenyekuamini hivyo na Tuseme AMINA!!

Friday, 3 February 2012

Dada huyu Auwawa Kikatili na Rafiki yake wa Kiume!!!!

Da'Rudo Mawere Enzi ya Uhai wake.


Dada huyu ameuwawa na aliyekuwa Rafiki yake wa Kiume/Mpenzi wake, Jason Dube,Naye mwanaume huyo baada ya kufanya mauaji  hayo  huko Ireland,akarudi U.K. naye amekutwa amejiua.Kaka Jason alikuwa akiishi hapa Coventry,Poleni sana Familia ya Dube na Mawere.Habari kamili unaweza kuipata hapa;http://www.nyasatimes.com/malawi/2012/01 au htt://www.independent,pia ukiingia face book andika Rudo Mawere pia unaweza kupata maelezo vizuri.Habari hii imetuhuzunisha sana kwani huyu mwanaume tulikuwa tunamfahamu.



   


Friday, 27 January 2012

Watoto wa Kiume na Wakike Wanamajukumu Sawa?


Nimatumaini yangu woote Muwazima!!!na Kama kunamgonjwa Pole sana na Mungu akuponye.
Waungwana Eti watoto wa kijijini wa Kiume na Wakike wanamajukumu sawa?Yaani si lazima wote waende kuchota maji pamoja,basi kama huyu anafagia mwingine aoshe vyombo,na ikifika saa ya kujisomea wote wanasoma,ikifika saa ya kucheza wote wanacheza.Najua kila familia inamalezi yake,Jee vipi kwa malezi ya kileo huko kijijini yameweza kubadili muonekano/Majukumu ya watoto? kama si kijiji kizima basi kuna nafuu?na kama hakuna jee tunaweza kuwasaidiaje?Sawa Mwanamke ni mwanamke, Mwanaume ni Mwanaume hilo naliheshimu pia.Jee Vipi na Watoto hawa wa Mjini?

Karibuni sana Wapendwa, kwa Mawazo,Ushauri,Kuelimishana  kwa Upendo.

Wednesday, 25 January 2012

Wanawake na Urembo,Unapenda Shanga?

                                Wengine wanavaa Kiunoni.
                                     Wengine wanavaa Shingoni
                            Wengine Kichwani,Mikononi...........
Nimatumaini yangu wote muwazima!!!
Haya wapendwa leo tuangalie Urembo huu wa Shanga,Jee wewe Mama,Dada wapenda Shanga?
Nawe Baba,kaka Unapenda Mkeo,Mchumba wako ajipambe kwa Shanga?
Kuna wanaopenda kuvaa Miguuni,kuna Mikanda, Bangili,Hereni naa........,Jee wewe Unapenda/Ungependa Uvae/Avae wapi?Wengine wanapenda za Bendera ya Taifa na......Vyovyote vile ilimradi SHANGAAA!.
Kitamaduni zaidi au Vipi?

Karibuni sana Waungwa!!!!!