(Lifestyle)Jamii,Tamaduni ,Matukio,Maisha ya Waswahili. Wapendao Kiswahili/Waswahili,Marafiki wa Swahili na Waswahili, Na Mengineyo ya Karibu, Yahitajikayo Kujuzwa Waswahili.Karibuni sana!!!!!!!
Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Waungwana; "Jikoni Leo" ni Puréed vegetables (a special meal for children from 18 months to 4 years old) Mpishi si Wengine ni da'Sophi wa "Tupike Pamoja". Mmmhhh Tamu Saaaana!!!!! Kwa kujua zaidi ingia;Tupike Pamoja au www.tupikepamoja.com
Waungwana;"Jikoni leo" si wengine ni "TupikePamoja," Walipotea kidogo lakini waswahili wanasema kinya kingi kina.............basi wamerudi tena kwa kishindo. Nisiwachoshe kwa maneno meeengi.Fuatana nasi katika Pishi la Leo ni "Country Salad" ... Haya mambo hayo...ukitaka kujua zaidi usisite ingiaTupike Pamoja au
www.tupikepamoja.com
Waungwana; "Jikoni Leo" lilikuwa Mtaani, haya jiko hilo moto ukiwa mwingi unapandisha juu kama bembeaaaa.. Vipi Jiko hili kwa Kuchomea Mahindi,Mihogo,Mishikaki/Nyama Choma na ............ Mambo ya Hot Dog hayooo mitaani...Vipi wewe kilaji hiki kinapanda/unakipenda? Ahh Wadhungu kwa mikate wanaibadili Jina tuu na kuweka vitu tofauti lakini ni Mkate tuu. Hahhaha tena Nyumbani wanywaji Bia kwenye Bar wanakula Nyama choma au Michemsho..Wao Ngano kwa Ngano, Bia kwa Mkate..... Jee Wanywaji mliokuwa Nje ya Bongo/Tanzania Nanyi mnaweza kunywa Bia kwa Mkate?.... Tunasubiri Maoni,Ushauri na Kuelimisha kwa Upendo..!! "Swahili na Waswahili" Pamoja Daima.
Huu ulikuwa Mchanganyiko[Msetoo], Mchele,spaghetti,Karoti naaaNjegere yaani kama Biliyani,Pilau. haa hhaaaaaa [Mchanyatooo]
Huyu alipika Nyama iliyochanganywa na Majani siyajui, Ndizi na vingine vingi kama Tulavyo Waswahili lakini Michanganyo yake tofauti kidogo.[Jamaica]
Hawa waliandaa OLIVE Kwa radha Tofauti, hii mimi nilitaka kurudisha Chenji[sikuweza kumeza]
Hii ni Nazi, hiyo Nyeupe kabla haija Okwa, hii ya chini imeOkwa nilipenda sana.
Hawa walitengeneza/kupika kutumia Tambi[Noodles]Ngano na Viungo vya kwao....
Hawa walitumia Ngano zaidi.Mmmhhh Ngano ina mambo meeengi sana!!
Waungwana;"JIKONI LEO"Lilikuwa Mitaani kuona,kujifunza,kuonja tusivyovijua/Mapishi ya watu wa Nchi Mbalimbali. Kulikuwa na mambo meengi, Leo tuanze na Jikoni.Kuonja ilikuwa Bureeeee ,Duhh nilionja mpaka nilichoka Mmmmhh vingine havionjeki. Nafikiri ni Mazoea ya Vyakula. Nazi ilitengenezwa kivingine,Ngano ambayo mimi nimezoea kwa Maandazi,Chapati na vitu vichache vya Kiswahili, nayo ilipikwa kivingine. Duuhh sijui nianzie wapi niishie wapi,wewe kula kwa picha tuu.MCHELE MMOJAMapishi Mbali mbali.......... Yote tisa Chakula cha Waswahili Hakikuwepo,Sikujua kwa nini labda hawakuwa na Taarifa au Mwezi Mtukufu waliona walaji Wachacheeeee!! Katika Kutembea watoto wakaniita Mama tumeona Banda la ZANZIBAR!!!!!!Lakini Tumemsalimia kwa KISWAHILI Amecheka tuu,Tukamsalimia kwa Kiinglishi[ENGLISH] Ametujibu.Nilipofika hapo nikakutana na Muhindi Amezaliwa KENYA naye anamuuliza kama ametokea TANZANIA?Kwa KISWAHILI,Duhhh kaka Muuzaji alichekaaaaa.Akasema hajui hiyo Lugha yeye anajua hiyo kitu ZANZIBAR na MASAI Tuu.Baada ya kuongea Nae Akasema yeye ni MJAMAIKA[JAMAICAN] Hupenda kujifunza Mapishi na Mambo ya Nchi Tofauti. Mimi nikamsalimia MUHINDI Tuka chapa SWAHILI YETU na TUKAFURAHI. Jee Unalolote la Kuongezea kuhusu kwanini WASWAHILI Kutokuwepo/Kutokuwa na Banda hapo? Uoga,Kutojiamini,Hatupendi kujitangaza,Hatuna Muda/Nafasi ,Mwezi Mtukufu,Hatufuatilii nini kinaendelea Sehemu Tunayo Ishi ...AU? Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo. Hii ilikuwa; COVENTRY.U.K. "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
MAHITAJI yogurt vijiko 2vya chakula sukari 1/4 mug hamira kijiko kimoja cha chai iliki kijiko kimoja cha chai samli kijiko kimoja cha chakula unaweza tumia,maji/maziwa/nazi yapime katika mug uliyopimia sukari ponda hadi unga wako uwe mlaini kiasi,katakata matonge,sukuma kata maandazi yako yaache yaumuke yachome. unaweza kutumia maharage,mchuzi wa nyama,maini,samaki kama kitoeo.
Waungwana Mapishi yapo Mengi haya "JIKONI LEO" ni Maandazi ya Yogurt ,Siyo Nazi kaazi kwako kama wewe Mpishi au Muonjaji!!!!
Mpishi si Mwingine ni da'MAIDANA na "JIKO LANGU" [LAKE]. kwa Maelezo Zaidi ingiahttp://jiko-langu.blogspot.co.uk/
"Swahili NA Waswahili" inawatakia Ramadhani Njema Waislam woote Dunia.
Waungwana "JIKONI LEO"Si wengine ni "TUPIKEPAMOJA" Leo wametuletea Mapishi ya Coated Chicken With Chutney.Mmmmhhhh Tamu Sanaaa!! Hii ni Video Mpya Waungwana Usikose kupitia www.tupikepamoja.com kwa vipimo na kujua zaidi.
Waungwana "JIKONI LEO" Pata video mpya kutoka "TUPIKE PAMOJA" Wanakuletea mambo ya Supu!! Supu si Nyama tuu, Ungana nao kupitia www.tupikepamoja.com pia unaweza kuungana nao You tube. Mhhh Tamu sana!!!!!!!! Unaswali au Maoni? Usisite kuongea nao ,Usife nalo....hahahaaha "Pamoja sana Swahili NA Waswahili"
Waungwana "JIKONI LEO" Ni "TUPIKE PAMOJA" Wametoa Video mpya Jinsi ya Kupika Donuts.kama una Swali,Ushauri Usisite kuwasiliana nao kupitia.www.tupikepamoja.com.
Waungwana; "JIKONI LEO;"Ni Tupike Pamoja wametoa Mapishi mapya ya Russian Salad,kwa njia ya Video.Lugha ni Kiswahili. Usikose kujifunza kupitia "TUPIKE PAMOJA" Mmmmmhh Tamu Saaaana. Kuona mengi zaidi ingia;www.tupikepamoja.com au hapo pembeni kuna nembo yao bonyeza tuu.
Visheti,Kashata,Keki, hivyo vyenye kidoti mie naviitaga vibata, sijui vyaitwaje?Hapa bado Ufuta jamani duuhh
Mikate,sijui wewe utaitaje kwani hapa kwangu kila mtu anajina lake!
Ipo kwa umbo tofauti
Waungwana karibuni tena "JIKONI LEO".Leo Mpishi wetu si Mwingine ni da'Maidana,Ni blogger Mwenza,Pia ni MjasiriaMali,Ukitaka kujua zaidi. Anapatikana.http://tmark-turn.blogspot.co.uk
Nimegundua Waswahili Wengi Wanapenda kupika na kujifunza Mapishi Mbalimbali. Vipi wewe mwenzangu unapenda kupika?jee mbali na kupika Unapenda/Unaweza Kufanya nini kwa Mikono yako?
Karibuni sana Waungwana katika yoote!!!!!! "Swahili na Waswahili" pamoja sana!!!!
Habari utakazo zipata katika tovuti hii ni picha za video na
maelezo ya kina kuhusu namna ya kupika mapishi na vyakula vizuri vya
kimataifa muhimu zaidi ni rahisi kupika. Tovuti hii ni kwa ajili
ya watu wanaopenda kupika, kujaribu vyakula vipya na ladha mpya ili
kuwashangaza rafiki na familia zao kwa ladha hizo. Maelekezo ya mapishi
utakayopata hapa ni kwa ajili ya meza kuu ingawa wakati mwingine
tunashirikiana nawe katika vinywaji na viburudisho (deserts &
sweets). kwa kuanzia ni matumaini yetu utafurahia kupika kama sisi. Pia usisahau kututumia maoni yako, maswali na ujumbe tuweze kuboresha na kutimiza mahitaji yako, Asante kwa ushirikiano wako Furahia chakula chako!
Kujua zaidi Mtembelee.www.tupikepamoja.com
Haya Waungwana Mambo hayo kazi kwenu na "Tupike Pamoja"
Muonekano wa kitabu cha mapishi cha"A Taste of Tanzania".
Cover ame-Design Mwenyewe na Picha amepiga mwenye.Kitabu kitatoka hivi karibuni.
Utakipataje;Ataweka wazi jinsi gani unaweza kupata Kitabu.Ukiingia pale kwake kunasehemu ya mawasiliano,Unaweza kuwasiliana nae Zaidi kupitia http://www.tasteoftanzania.com
Jee da'Miriam anajua KISWAHILI?JIBU;Ndiyo,anakichapa haswa, kama ulivyoona kwenye ile post iliyopita niliandika ni Mswahili.
Nafikiri nimewajibu nijuavyo Waungwana mlionitumia Email na mlionitumia Messages kwenye sim.Na nimeweka hapa kama kuna wengine waliokuwa na maswali kama haya nao Wamepata Jibu.
Haya Waungwana pata mapishi ya UJI na FUTARI kutoka kwa da'Miriam Rose.Hapo juu.
Hapo chini;Mapishi ya "VITUMBUA"Kutoka kwa da'Cecy anapatikana http://mapishinacecy.blogspot.co.uk.
Mswahili mimi kupika vikorombwezo saaaana siweziiiiii,Najua kupika kiasi cha Kula MUBENA yangu na Watoto yangu na Wageni kidogo tuu,Si kila mtu anaweza kila kitu jamani, Watu na VIPAJI Vyao.MIMI nitakuwa nakurushia Matukio tuu hapa.Na nikipata Muda nitaweza Kuwatembelea Wapishi Nyumbani kwao na Kuwawekea MAZUNGUMZO na MAPISHI HAPA!!AU VIPI WAUNGWANA.SWAHILI NA WASWAHILI!!!PAMOJA SANA TUU.
imi huwa navutiwa mnoo na kazi zake dada huyu.Huwa sisiti kumuuliza pale nitakapo kujua zaidi.Sijapata nafasi ya k HayaWaungwana leo nimewaletea da'Mriam Rose wa Kinunda.
Mukutana nae,Lakini kwa mawasiliano tuu kwangu ni mtu asiye na Majivuno,dharau,Umimi/Ubinafsi.Ni dada Mcheshi na mwenye Upendo, na meeengi.
Hongera sana na Ahsante sana da'Miriam Rose kwa yooote,Mungu azidi kukubariki.
Kufahamu zaidi kazi zake na yeye ni nani ingia "Taste of Tanzania" http://www.tasteoftanzania.com
Kwangu mimi ni Mwanamke wa Shoka huyu dada,Kichwa,mama Vipaji.
Ni Mwanamke wa Kwanza Blogger Mswahili mimi kumfahamu.blog yake http://damija.blogspot.co.uk
Da'Mija na Wanawake wa Shoka.
Swali;wewe Unafikiri Wanawake wa Shoka Wakoje?.
Haya tukiachana na hayo, Shuka Chini uone Swali lake analotaka KuJibiwa,Linatokana na Mada ya Jikoni leo ni Kakazz.
Mama MM[Jina lake linaanzia na M,Mume wake M, watoto wao M.M]
Kidada zaidi au vipi!!Una mbwembwe wewe dadake.
Nanukuu.. "Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia
kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au
Kuto OA Kabisa?."
Nami ngoja niulize kulingana na swali.."Kwani
nafasi ya mwanamke ni ipi katika ndoa..Je ni kupika na kufanya kazi za
ndani? au kwa maana nyingine ni kwa nini hasa mwanaume huamua kuoa?
Mimi nafikiri mboga za leo mwenzake Nguna/Ugali,Jee mwenzangu?
Mboga ya Majani. Jee ukishiba utashushia na nini?
Waungwana Wanaume Leo ndiyo waliotuandalia Chakula, Kumbe wakiamua wanaweza,Huko nyuma tulijadili kuhusu ''WANAUME NA JIKO'',Kaka S. [Sam mwana wa Mbogo]Alielezea vyema sana, Hasa yeye anavyohusika Jikoni.Pia akasema Wanawake wengi wakisaidiwa huwa Wanatabia ya Kujisahau.
Kaka zangu hawa nao wanasema wao hupenda kujipikia zaidi kuliko kupikiwa.
Swali;Eti Wanaume wengi wanaopenda Kupika na Kujifanyia kazi za ndani wenyewe Huchagua sana Wanawake wa Ku OA,Huchelewa KUOA au Kuto OA Kabisa?.
Jee wewe Mwenzangu una Maoni,Ushauri Gani? Pamoja sana!!!
Mboga za Majani Mchanganyiko,Majani ya Kunde na Majani ya Maboga
Mchuzi wa Samaki Umeungwa/wekwa Nazi na nyanyachungu
Maandaziiiiii na hapo chini ni Mahindi ya Kuchemsha.
Haya Waungwa,vipi wewe unapenda kupika?au Unapika kwasababu ni lazima upike na ule?Kwenye kazi zaNyumbani kila mmoja kuna kazi anapenda kuifanya, Na kuna baadhi ya Kazi hatuzipendi,Lakini tunafanya kwa sababu ni lazima zifanywe,Na utasikia duuh yule kaka/dada au Mama/Baba anajua Kupika sana,Hivi kujua kupika ni Chakula kiive au? Kwani Utamu/Radha ya chakula wewe unaweza kupendezwa nacho na mwingine asipendezwe nacho. Jee Kazi/Ujuzi wa Kupika ni kwa Wanawake tuu?Kwani mara nyingi utasikia Mwanamke jiko na si Mwanaume Jiko,Hasa kwa Maisha ya Leo, kwa Maisha ya Zamani wengi wao Mama/Dada kazi yao kubwa ni Upishi na Baba wengi ndiyo walikuwa wanafanya Kazi hasa Mijini, Kwa Vijijini Woote BABA na MAMA Wanaenda shambani lakini Kupika ni MAMA.Jee Leo Tunaweza Thubutu kusema MWANAUME JIKO? AU TUTAKUA TUMEWADHALILISHA?Kwani wapo Wanakarangiza haswaaaa kutushinda au Hamjakutana nao?.
Karibuni Waumgwana kwa Mawazo na Kuelimisha na Kwa upendo.