Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Waswahili na maisha. Show all posts
Showing posts with label Waswahili na maisha. Show all posts

Tuesday 14 June 2011

Penye Wengi Pana Mengi!!!!!!

 Hapa kina Mama/Wanawake wapo Jikoni na Mazungumzo yao.
Hapa kina Baba/Wanaume wapo Nje na Mazungumzo yao.

Wapendwa, Wanapokutana watu wawili au watatu hapakosi neno/maneno ya kuongea.
Na katika pitapita zangu  Mswahili mimi, Kwenye  Mikusanyiko ya Wa Afrika/Waswahili wengi kama si wote,Utakuta Wanawake/Kinamama wanakaa pekeyao na Kina baba Wanakaa pekeyao,Hata kama hawakuambiwa Kina MAMA sehemu yenu hii na Kina BABA manaombwa kukaa hapa.

Wenyewe  tu mmoja baada ya mwingine utaona wanajitenga.
Jee wewe mpenzi msomaji Unamawazo gani katika hili? Ni Utii,Heshima,Kujinafasi,Malezi tuliyo lelewa Au....
Na unafikiri wakina Mama wakiwa huko zaidi wanaongelea nini?
Na kina Baba jee?.

Karibuni sana Wapendwa Tuzungumze Pamoja!!!!

Tuesday 3 May 2011

Waswahili wa Holland na Qeen Day!!!!!!!!


 Waswahili wa Holland wakisherekea Qeen day.Hii ni Siku muhimu kwa watu wa Holland,Waswahili wa huko nao wakaona vyema kujumuika na wenyeji wao.Tunawatakia Maisha mema na Ushirikiano mzuri.
Je wewe msomaji  huko unapoishi,  Unapenda kuungana na wenyeji wako katika siku zao muhimu?Karibuni sana  Waswahili wote popote mlipo,Mnaweza kutuma picha /matukio yenu.