Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mtanzania/Mswahili. Show all posts
Showing posts with label Mtanzania/Mswahili. Show all posts

Monday 4 June 2012

Orijino Komedi na -OK Msuruhishi wa Muungano-Msudani.avi

Hahahhhaahahhahah haya,Waungwana Mambo ya Tanganyika na Zanzibar!!!!!!
[Watoto wa mujini wanasema Kimenuka huko].


Sina la zaidi Mengi Mtasema Wenyewe!!PaMoja sana "Swahili na

 Waswahili"
Mungu ibariki Tanzania.

Friday 18 May 2012

MTANZANIA DR ENGINEER SHABAN KACHUA ATUNUKIWA RASMI SHAHADA YAKE YA UDAKTARI WA FALSAFA NCHINI CANADA.


Dr Engineer Shaban Kachua mwenye joho lenye rangi nyekundu na Bluu akiwa na waafrika wenzake wakati wa alipotunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa falsafa Nchini Canada.
Hapa Dr Kachua akiwa amekaa mstari wa mbele kabisa na wahitimu wenzake.
Mama Mzazi wa Dr Kachua (mwenye blauzi nyeusi), akiwa na Mama mkwe wake, wote kwa pamoja walishiriki katika tukio la kihistoria la kutunukiwa Shahada ya PHD kwa mtoto wao nchini Canada.
Mrs Dr Shaban Kachua (Jemima) akiwa na furaha pamoja na watoto wao walishiriki katika shughuli ya kutunukiwa Mume wake shahada ya udaktari wa Falsafa (PHD).

Kwa sasa Dr Shaban Kachua anaishi Nchini Canada pamoja na familia yake. Sisi kama watanzania wenzake tunapenda kumpongeza sana kwa kuweza kuipeperusha vema Bendera yetu, tunapenda kumshauri pia, elimu yake hiyo aweze kuitumia pia kulisaidia Taifa lake la Tanzania hasa katika nyanja hiyo ya Sayansi, kwa kutambua zaidi tuna upungufu mkubwa wa wanasayansi katika Taifa letu.

HONGERA SANA
Asanteni sana KapingaZ http://kapingaz.blogspot.co.uk/

Wednesday 16 May 2012

Mswahili;SAM MACHOZI - MY ANGEL.{OFFICIAL VIDEO}

Hii ni yenu.....!! ni video yangu ya kwanza kama sam machozi nigependa sana saport zenu wa TZ ili niweze kuipeleka bendera yetu mbele kimataifa zaidi tuamini kama tunaweza na tutaweza mungu yupo na sisi milele amine... ni sam machozi`TO ALL MY BEAUTIFUL PEOPLE...!
Hayo ni Maneno yake kaka Sam Machozi.

Pamoja sana Waungwana!!! Swahili na Waswahili.

Thursday 10 May 2012

Mchague Joseph Lukaza !!!!!!!


Mchague JOSEPH LUKAZA ili aweze kuibuka mshindi katika shindano la EXCEL WITH GRAND MALT katika chuo kikuu cha Dodoma katika  Category ya Innovation Nominee
Jinsi ya kushiriki kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa simu unaandika
"INV UDOM JOSEPH LUKAZA 3rd year" alafu unatuma kwenda namba 0653202000.
Na unaweza kupiga kura kwa kutumia tovuti
 
                             

Thursday 19 April 2012

MWAKILISHI MKAAZI WA UNOPS NDUGU OMARY MJENGA AKIBADILISHANA MIKATABA YA UJENZI WA HOSPITALI YA WATOTO NCHINI SIERA LEONE
Ndugu Mjenga wakijadiliana jambo na Naibu Mwakilishi wa UNICEF Bw Gopal Sharma wa nchini Siera Leone

Kutoka kulia ni Bwana Omar Mjenga, Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, akibadilisha mikataba ya ujenzi wa hospitali tatu za kisasa za watoto na Naibu Mwakilishi wa UNICEF Bw Gopal Sharma aliyemwakilisha Bw Mahimbo Mdoe ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Nchini Sierra Leone na Kushoto, ni mwakilishi wa Waziri wa Afya wa Siera Leone.


Bw Mahimbo ni Mtanzania mwingine mwenye cheo cha uwakilishi. Mtanzania mwingine mwenye cheo cha uwakilishi ni Bw Gabriel Rugalema, ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa FAO Nchini Sierra Leone. Tanzania inazidi kutamba katika nyanja za kimataifa


Habari hii nimetumiwa na KapingaZ Blog. http://kapingaz.blogspot.co.uk
Ahsanteni sana.