Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Msiba/Jamii. Show all posts
Showing posts with label Msiba/Jamii. Show all posts

Wednesday, 27 September 2017

Kifo cha Mtanzania Hispania - MwanasarakasiKIFO CHA MWANASARAKASI MOHAMMED IDI MOHAMMED (“MOHDY”)
Na Freddy Macha
Sarakasi ni kati ya sanaa hatari na za kusisimua sana.
Kwa sasa Ulaya wapo vijana na watu wa makamo mbalimbali waliohamia toka Afrika Mashariki (hasa Kenya na Tanzania) wakitumbuiza kadamnasi kwa sarakasi, Uingereza, Ureno, Ujerumani na Hispania.
Nchini Hispania kuna visiwa vya Grand Canary ambapo Watanzania wachache huruka ruka kuvutia maelfu ya watalii.
Moja yake ni Lanzarote. Hapa Mtanzania Mohammed Idi Mohamed aliyehamia baada ya kuishi Ujerumani kwa kipindi. Mohdy, Muddy au Modi (wanavyomjua wengi) aliwahi pia kufanya kazi Tanzania, Ureno na Uingereza.
Alifariki Jumatatu 18 Septemba, 2017, asubuhi. Sababu za kifo chake zimeelezwa na waganga ni kuvuja damu kutoka mfereji wa koo kwenda mapafu na kutokea tumboni. Alipasukwa mshipa huu wa damu ghafla na kuanguka bafuni akipiga mswaki. Bahati nzuri Muddy alijikatia bima ya maisha ambayo imeondoa tatizo la kusafirisha mwili wake nyumbani kuzikwa. Michango iiliyoombwa kutolewa itasaidia familia yake na gharama nyingine za mazishi. Tuma kupitia Western Union. Huwa bei nafuu zikitumwa zifike kesho yake badala ya siku hiyo hiyo... Marehemu ameacha watoto wawili na wajukuu. Mungu aiweke roho yake pema peponi.

Kwa walio Ujerumani, ni Malimbo Saidi Malimbo, simu (+49 ) 1522-4082848.

Uingereza, Saidi Kanda (+44) 4040-66607. Tanzania, Eddy Sengo, (+255) 656 210 725.

Picha ihsani ya Fab Moses, Lanzarote, Hispania


-London, 26 Septemba 2017

-Bpepe: gmacha52@gmail.com
-Tovuti: www.freddymacha.com

Tuesday, 19 January 2016

MSIBA NYUMBANI KWA MAREHEMU GEORGE SEBO BOWIE, MARYLAND NCHINI MAREKANI


Kushoto niAbdul Sebo  mtoto wa marehemu akipewa pole na moja ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwa marehemu Bowie kutoa pole na rambi rambi zao kwa wafiwa kutokana na kifo cha mpendwa wao Mzee George Sebo kilichotokea siku ya Jumatatu asubuhi January 18, 2016 katika Hospitali ya Prince George iliyopo Maryland nchini Marekani. Utaratibu na mipango tutajulishwa leo kwa sasa imetengenezwa GOFUNDME ambayo ni www.gofundme.com/8fjvpcns
Picha na Vijimambo/Kwanza Production
 Kati ni mke wa marehemu Aunty Grace akipewa pole na moja ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani kwa marehemu kujumika nao na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao mzee wetu George Sebo

 Mmoja ya wanaDMV wakijumuika pamoja na kwa kutoa pole na kuwafariji wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. Kushoto ni Salma Moshi.

 WanaDMV na wanafamilia wakijumuika na kuwafariji wafiwa nyumbani kwao Bowie, Maryland nchini Marekani na kutoa pole na rambi rambi zao . Kutoka kushoto ni Sharif, Tuma, Salma, Justa, Aunty Grace na Iska wakiwa na mke wa marehemu Aunty Grace kumpa pole kwenye msiba wa kuondokewa na kipenzi mume wake Mzee George Sebo.

WanaDMV wakijumuika na wanafamilia nyumbani kwa marehemu Bowie, Maryland.

Saturday, 26 October 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Msiba wa Martha Shani DC


Katika kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA wiki hii... Kutoka nchini Marekani, tuanze na habari za msiba ulioikumba jamii ya waTanzania waishio maeneo ya Washington DC.

Marehemu Martha Shani

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).a


Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 26, 2013 

*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"