Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Friday 7 March 2014

International Women's Day 2014 - UDSM female staff.

Wanawake tunaweza.. Mamaaa GerryHans nawatakia wanawake woote kila la kheri ktk kusherehekea siku ya wanawake duniani. Kina Mama oyeeeee...

Picha na Mpiga picha Wetu;Phoibe Penza- Mshana[Mwanapenza]


Kama unapicha,Ujumbe wowote,Usisite kututumia kwa Email;rasca@hotmail.co.uk

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.




Tuesday 15 October 2013

AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA@ CAPITAL RADIO. Kutekwa kwa Waziri Mkuu wa Libya na kukamatwa kwa Al-Libi‏



Kutoka Tripoli nchini Libya....Watu wenye silaha mapema Alhamis walimteka na baadae kumuachia huru Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan juu ya kile ambacho waasi wamesema ni kuonyeshwa kukerwa na matatizo ya RUSHWA NA USALAMA katika nchi hiyo.

Hili linaonekana kutekelezwa kufuatia kukamatwa kwa mshukiwa wa kundi la kigaidi la AlQaeda Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, ambaye pia anafahamika kama Abu Anas al-Libi aliyekamatwa jumamosi iliyopita nchini Libya na makomandoo wa Marekani

Huu ni muendelezo wa taarifa tofauti na za kuchanganya tangu kukamatwa kwa Al-Libi

Ifuatayo ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es
Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 12, 2013


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

www.jamiiproduction.blogspot.com
http://www.youtube.com/user/mutwiba/videos
https://soundcloud.com/jamii-production