Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Mahojiano/Diaspora. Show all posts
Showing posts with label Mahojiano/Diaspora. Show all posts

Wednesday, 20 September 2017

Wednesday, 28 June 2017

Mahojiano ya Mubelwa Bandio na Shose Kombe kuhusu Diaspora


Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Mkuu wa Mawasiliano wa Diaspora kutoka KCB Bank Shose Kombe.
Mahojiano haya yalifanyika ndani ya Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland nchini Marekani

http://www.kwanzaproduction.com/mubelwa-bandio/

Tuesday, 14 June 2016

Msemaji wa serikali azungumza na Diaspora.......Jukwaa Langu Juni 13 2016


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga
Photo Credits: Wavuti.com
Katika kipindi hiki, tumezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga ambaye ameeleza kuhusu nafasi na wajibu wa serikali kwa waTanzania waishio Diaspora.
Pia amegusia wajibu wa waTanzania hao kwa nchi yao na kujibu maswali mbalimbali
Karibu


Wednesday, 6 April 2016

[VIDEO] Mahojiano ya Mubelwa Bandio na mgombea uwakilishi nchini Marekani Will Jawando

Photo Credits: @wjawando
Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando
alihojiwa na Mubelwa Bandio katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland
nchini Marekani. Mbali na mambo mengine, alizungumzia kuhusu mikakati yake katika
kuisaidia diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla. Ikumbukwe kwamba 10% ya wazaliwa wa Afrika wanaoishi Marekani, wapo katika jiji la Washington DC

Karibu ufuatilie mahojiano haya


Saturday, 26 March 2016

Mgombea uwakilishi Marekani William Jawando ahojiwa Kilimanjaro Studio, azungumza na Diaspora


Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando, leo alihojiwa katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland nchini Marekani ambapo alizungumzia kuhusu mikakati yake katika kuisaidia diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla.

Will, ambaye akishinda atakuwa ni mtu wa pili aliyezaliwa na Baba aliyetoka Afrika kuingia bungeni humo (baada ya Rais Obama) ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ambavyo uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni muhimu Zaidi nchini Marekani, na hasa kwa wakazi wenye asili ya Afrika waishio vitongoji vya Washington DC.

Ikumbukwe kwamba, inakadiriwa kuwa mmoja kati ya wazaliwa kumi wa Afrika walipo nchini Marekani, anaishi eneo hili, na nusu yao, wameingia nchini baada ya mwaka 2000. Hivyo amefafanua namna ambavyo kuwa na mtu mwenye kuelewa na kuwakilisha vema jamii hiyo, ni muhimu kwa jamii hiyo.

Aligusia pia namna ambavyo asili yake na makuzi yake yamechangia yeye kuingia katika kazi za kuihudumia jamii, akaeleza vipaumbele vyake kwenye uongozi wake ujao na pia wito alionao kwa jamii ya waAfrika walioko Marekani.

Uchaguzi wa kuteuliwa kugombea kupitia chama cha Democrat utafanyika Aprili 26, lakini kura za mapema zitapigwa kati ya Aprili 14 na 21.

Kujua mengi kuhusu Will Jawando, maisha yake, kampeni na mipango yake, tembelea willjawando.com

Anagombea kiti kilichoachwa wazi na mwakilishi Chris Van Hollen ambaye ameamua kugombea kiti cha Seneti kinachoachwa wazi na Seneta Barbara Mikulski anayestaafu

Mahojiano kamili na Will Jawando yatakujia hivi karibuni

Baada ya mahojiano, Will alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wanaDiaspora wa Afrika waliokuwa ndani ya jengo ilipo studio.

Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akipata picha na Mubelwa Bandio baada ya mahojiano
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza na baadhi ya waAfrika waliohudhuria "Meet & Greet"Michelle Jawando, mke wa mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza machache kuhusu umuhimu wa uchaguzi wa mwaka huu

Mubelwa Bandio akiendelea na maandalizi ya mwisho ya mahojiano na Will Jawando
Mmoja wa wadau wa Kilimanjaro Studio Harieth Shangarai akimpatia maelezo machache Will Jawando
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akiuliza maswali kuhusu uendeshaji wa Kilimanjaro studio
Mubelwa Bandio akitoa maelekezo kwa Will Jawando
Mahojiano yanaendelea