Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday 31 May 2016

Kama umeguswa msaidie huyu bibi..


"Nimetumiwa na Rafiki"
~
Haya wapendwa  nataka ku share hii video na nyinyi na yoyote atakae pata imani please inbox Facebook[Nana O Al Wakuvuruga ]msaada wako. Miezi kadhaa nyuma niliwaho share hii video na baadhi ya groups ili atakae weza amsaidie huyu bibi kuna ambao wamejitolea alhamdulillah lakini kwa ufupi pesa itamtosha kwa miezi miwili mitatu kununulia kula yake halafu baada ya hapo atarudi to square one. Inawezekana mnajiuliza huyu bibi ni nani? Huyu bibi sihusiani nae na wala sijawahi kutana nae ila inshaAllah mwaka huu nitamtafuta nimjue kwa ukaribu. Mimi nilipewa video hii na mwenzangu ambae nae pia alipata kumjua mwaka jana alipoenda matembezi Tanzania. Akapewa habari ya bibi huyu ili kama anaweza amsaidie chochote. Kubwa alienipa hii taarifa kajua hawezi lifanya hili jambo peke yake ndio akanijulisha na mimi. Sasa kwa ufupi huyu bibi hakujaaliwa mtoto, amefadhiliwa na watu hicho chumba mnacho kiona kwenye video na picha nitawatumia mpate kuona vizuri mazingira anayo ishi. Hajui kula yake ataitolea wapi wala tiba, kabaki anapita akiomba ndio siku inaenda. Hicho chumba mnacho kiona kukinyesha mvua ya nguvu maji yanajaa huko chumbani kwake anashinda juu ya kitanda mpaka maji yakauke. Nahitaji watu wajitolee kwa hali na mali apate kukarabatiwa chumba chake na at least japo ajijue anapata japo mlo mmoja kwa siku. Wazee wetu kweli wana shida lakini naamini hawajafikia hali hii, kumbuka bibi huyu hakujaaliwa kuzaa kwahiyo hana matumaini zaid ya kuomba vijumbani. Please find it in your heart and inshaAllah donate whatever you can. I joke a lot this is not one of those jokes; its real for this elderly lady and ahe doesn't even know I'm doing this
"Swahili Na Waswahili"Kutoa ni Moyo.

1 comment:

Anonymous said...

Hana ndugu wa karibu masikini?
Tanzania ingeanzisha Sehemu YA kuwalea kuliko kuishi peke yake
Inshaaallah tutaku inbox