Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 28 May 2012

Da'Tracey-Sarah,Atimiza Miaka 11!!!!!!!

Da'Tracey-Sarah
Da'Sandra akiandaa Keki
Tumtangulize Mungu kwanza katika Yote!!!

Leo umezima 11,mungu akulinde uzime 100!!!
Anaitwa Mkama; kwakuzima Mishumaa hayuko nyuma,Kama mtoto wako anasuasua kuzima,Tuwasiliane!!
da'Tracey akikata keki na da'Mija akihakikisha mambo yako sawa!!!

da'Elizabeth na da'Mija wakiandaa keki,watu tule!!kweli watoto wa Shoka,Mungu awabariki sana!!
Mama akimlisha Mwana!!
Da'Mija akilishwa na Rafiki yake kipenzi,Mungu azidi kuwaunganisha daima!!
Da'Tracey akilishwa na dada yake!!
Da'Sandra akilishwa na Mdogo wake, duuh kuna haja ya kuongeza sijui!!
Da'Anita akilishwa,Chezea yeye!!!
Da'Asiimwe akilishwa,huwa hana haraka wala maneno mengi,jicho tuu linaongea!!
Da'Manjula aliamua kupanda juu ya kiti,Ale kwa raha,nani anapenda Ufupi?
Kamanda Mkama a.k.a.Mzee wa Next,Akipata kipande chake!!!
Dada Mkubwa,Eliza naye akijipatia keki!!
Pamoja daima!!!!
Katuni/Vibonzo lazima tuangalie!!!
Mapoziiiiiii
Unahitaji wanamitindo? Tuwasiliane.....hahahahaha
Na muziki tulisakata, sikunyingine nitaweka Video!!!Lakini Zilipendwa waligomaaa!!!
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi,da'Mija[Mia] akipozi baada ya kazi kubwa!!
Da'Tracey[Sarah]Akipozi  na Kuwashukuru Wazazi,Ndugu,Jamaa na Marafiki kwa yooote!!!Familia ya Isaac,Tunamshukuru sana Mungu kwa Mema Mengi aliyotutendea,Asante kwa kumtunza na kumlinda Mtoto wetu Tracey-Sarah na Familia pia.
Asante kwa Kumaliza SAT'S,Salama,wewe ulimlinda akiwa Shule ya Msingi pia Tunamuweka Mikononi mwako Aendapo Secondary.

Shukrani Nyingi Ziwaendee,Familia ya Nyotu[Kamau].Familia ya Manju[Da'Mija Mwanamke wa Shoka].Kaka Don,baba Eliza na Familia yako. Da'Maggie[dadake]Asante sana.

Mungu awabariki sana kwa Moyo wenu wa Upendo na Kutumia Muda wenu kuwa nasi.

Pamoja sana Wapendwa,MUNGU NI PENDO APENDA WATU.Nasi TUNAWAPENDA WOOOOOTE.

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

hongera sana!!

Mija Shija Sayi said...

Rachel umedata dadake!! Yaani nimecheka leo duh! Hayo mapozi ya picha, kweli una haja ya kuonwa na wanaohitaji wanamitindo.

Mungu azidi kumbariki Da' Trecy aka mama wa kujiachia.. azidi kumpa kila lenye baraka aje a-rule the world.

Shukrani kwa yote, I salute you!!

God bless..

emuthree said...

Familia ina raha yake na raha ya familia ni watoto, lakini watoto wanahitaji malezi bora,wana haki zao, wanahitaji furaha na upendo, ili baadaye na wao wawe hivyo hivyo kwa watoto wao.
Kazi nzuri ndugu wa mimi tupo pamoja

Simon Kitururu said...

Hongera sana Da Tracey!

EDNA said...

Hongera saaaaaana Da tracey Mungu na akupe miaka mingi duniani,kanifurahisha huyo anayezima mishumaa kwenye birthday isiyo yake hahahaaa.

Rachel Siwa said...

Ahsante sana Wapendwa woote na Amina kwa Dua/Maombi yenu!!!!

@da'Mija Ameeeeen!hahahaaha watu na viapaji vyao Ma'Mkubwa,Pamoja sana.

@Asante sana Ndugu wa mimi,Pamoja daima.

@Mwanakwetu hahahaah huyo anaitwa Kamanda Mkama bingwa wakuzima Mishumaa,Ukimuhitaji tuwasiliane tuu.

mumyhery said...

Happy birthday Tracy

Rachel Siwa said...

Asane sana da'Mumyhery....