Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 22 May 2016

Natumaini Jumapili ilikuwa njema/inaendelea vyema;Burudani-Natembea kidogo kidogo nikinyatanyata......Happy Birthday da'Tracey-Sarah

Wapendwa natumai Jumapili ilikuwa/inaendelea vyema..
Mungu azidi kuwabariki katika yote..


Hapa kwetu Jumapili ni njema kabisaa
Leo tunaungana na binti yetu mpendwa kwa kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa
Siku kama ya leo Mungu alitubariki na kutujaalia mtoto wa kike da'Trace-Sarah
Mungu anaendelea kumtunza vyema katika yote..
Mungu yu mwema sana tunamrudishia sifa na utukufu kwakwe
Tunamwachilia binti huyu mikononi mwake Baba wa Mbinguni katika yote
Aendelee kuwa Baraka kwetu kama wazazi,walezi, Ndugu,Jammaa,Marafiki na Jamii yote
Mungu yu Mwema mnoooo
Happy Birthday da'Tracey-Sarah.

 8Mungu asema: “Nitakufunza
na kukuonesha njia unayopaswa kufuata.
Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.

Neno La Leo;Zaburi:32:8-11

9Usiwe mpumbavu kama farasi au nyumbu,
ambao lazima wafungwe lijamu na hatamu,
la sivyo hawatakukaribia.”
10Watu waovu watapata mateso mengi,
bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.
11Furahini na kushangilia kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu;
pigeni vigelegele vya shangwe enyi wanyofu wa moyo.

Bible Society of Tanzania


"Swahili Na Waswahili"Muwe na wakati mwema.

Wednesday 18 May 2016

Chaguo La Mswahili Leo:Yemi Alade - Na Gode (Swahili Version Official Video)

Chaguo La Mswahili Leo...
dada Yemi Alade ..

Sema Asanteehh hata ukikosa eehh sema Asante kweli wewe ni Mungu..........
.


"Swahili Na Waswahili"Burudika.

Tuesday 17 May 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu May 16 2016. Ziara ya Waziri mkuu UK. Uraia pacha


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London


Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kikiongozwa na Mubelwa Bandio toka Beltsville Maryland, USA, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.

Ni Tanzania kutoka jicho la DIASPORA

Na katika kipindi cha juma hili, tulizungumza na Chris Lukosi, ambaye
alitupa muhtasari wa ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa huko nchini Uingereza.

Muhtasari huo ulizua na mjadala mkali juu ya ahadi za serikali kuhusu vibali maalum kwa waTanzania waishio nje ya nchi.

Karibu

Sunday 15 May 2016

Nawatakia Jumapili njema:Burudani/Mahubiri na Mwl.Christopher Mwakasege...


wapendwa nimatumaini yangu jumapili ni njema na inaendelea vyema
Nawatakia Amani kutoka Moyoni,Imani,Baraka na Mkono wa Mungu ukawaguse
wote wenye kukata tamaa,wagonjwa,misiba,woga,kuonewa,kukataliwa/kutengwa
wagonjwa na wenye shida/tabu..
Amini Mungu yupo na ukimuita ataitika,Mungu wetu si kiziwi,kipofu...Anaweza na alitenda anatenda anaendelea kutenda....














"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Thursday 12 May 2016

Jikoni Leo na Tupike Pamoja; Recipe of Lemon chicken

Wapendwa waungwa natumai muwazima..
hapa kwetu tupo tupo vyema kabisa na hali ya hewa ni nzuri...kijua kimetoka..
vipi huko uliko wewe?

Ni Jikoni Leo sambamba na Tupike Pamoja wametuletea toleo jipya...

nisikuchoshe na maneno meengi Karibuni..


.....twende pamoja...


zaidiingia;Tupike Pamoja



"Swahili na Waswahili"Pamoja Daima

Sunday 8 May 2016

Jumapili iendelee kuwa Njema;Burudani-Christopher Mwahangila-Mungu Ni Mungu Tu na Edson Mwasabwite - Ni Kwa Neema Na Rehema





Natuini Jumapili ilikuwa/inaendelea vyema..
Mungu azidi kuwabariki kwa kila jambo..
wanaopitia magumu..Mungu akawaguse..
Mungu yu mwema sana...
Nawapenda wote na muwe na wakati mwema...


Umuhimu wa methali
1  Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi.2Methali hizi zawapatia watu hekima na nidhamu; zawafanya waelewe maneno ya busara, 3zawafanya kuwa na nidhamu, utaratibu, uadilifu, haki na kutenda kwa usawa. 4Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. 5Mwenye hekima azisikie na kuongeza elimu yake, naye mwenye busara apate mwongozo. 6Mtu aelewe methali na mifano, maneno ya wenye hekima na vitendawili vyao.
7  Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa,
lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Bible Society of Tanzania





"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Wednesday 27 April 2016

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete na Mama Salma Kikwete wakaribishwa nyumbani kwa Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi


Wiki iliyopita Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC, alimkaribisha Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete nyumbani kwake kwa chakula cha jioni na kujumuika pamoja na ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao walikuwa nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mikutano ya Benki ya Dunia (World Bank Group) na International Monetary Fund (IMF) tarehe 12 - 17 Aprili 2016. Kwenye ziara yake jijini Washington, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete alishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Afya (World Health Congress) na Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani (International Commission on Financing Global Education Opportunity).


DSC_0447.JPG
Mhe. Rais  Mstaafu Dkt. Jakaya M. Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na wenyeji wao, Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Mama Marystella Masilingi


Mhe. Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya M. Kikwete akibadiliashana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Servacius Likwelile (kushoto), Mhe. Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu nyumbani kwa Mhe. Balozi , Tanzania House Bethesda, MD.