Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 8 March 2015

Nawatakia Jumapili njema Na Happy Women's Day;that's my king-.!!!Burudani-Your Name Brings Healing To Me - Planetshakers (Worship song with Lyrics)


Wapendwa;Natumaini Jumapili inaendelea Vyema..
Mungu andelee kuwa Bariki na Kuwalinda kila iitwapo Leo..

"Happy Women's Day"


That's My King..!!!!!!



"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe sana.

Saturday 7 March 2015

Stara T aachia wimbo wa Siku ya Wanawake Duniani



Msanii Stara T, ametoa wimbo mpya UWEZESHWAJI WA MWANAMKE ambao ni maalum kwa ajili ya siku ya kinamama dunia inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.


Wednesday 4 March 2015

Jikoni Leo;Kenyan Mukimo Recipe How to make Mukimo - Jikoni Magic

Waungwana;"Jikoni Leo"Tujifunze kupika "Mukimo" chakula hiki kinapikwa/kuliwa sana na Ndugu zetu waKenya...
Mimi ni mmoja wa wapenzi wa chakula hiki,lakini sijawahi kupika huwa napikiwa na Rafiki yangu.
Vipi wewe Mpendwa/Muungwana umeshawahi kula/kupika Mukimo?
Kama bado jaribu natumai utakipenda.....


Twende wote sasa..


Shukarani/Thanks;Jikonimagic

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Monday 2 March 2015

Mazungumzo na Mhe Samuel Sitta (Pt I).......KATIBA


Karibu katika sehemu hii ya kwanza kati ya mbili za mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.
Aliketi nasi kuzungumzia zaidi suala hili la Katiba hii pendekezwa, na mchakato mzima wa kuipata
Karibu

 

Thursday 26 February 2015

MAWAZIRI WA NCHI TANO AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON,DC NCHINI MAREKANI


Mkutano uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika leo siku ya Jumatano Februari 25, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo  uliohusiana na maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.

Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  Balozi   Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

Washiriki wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu  MEAC Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Washiriki kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi, 

Wawakilishi kutoka Kenya walikuwa ni James  Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA & IT Kenya, Balozi  Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi  MFA & IT Kenya, Bi.  Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir  PA to CS MEACT Kenya.

Wawakilishi kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred  Nwam na Stilson  Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.

Mkutano huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na Rais Barack Obama.


Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiliano saini huo utafanyika siku ya Alhamisi Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani, kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.


Ujumbe wa Tanzania


Ujumbe wa Burundi


Ujumbe wa Kenya


Ujumbe wa Uganda na Rwanda


Mkutano ukiendelea.
Balozi wa Tanzania nchini Martekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

Wednesday 25 February 2015

Maisha;Ndoa Na Wanandoa-Majuto ni Mjukuu.!!!!!


Kijana Joseph ambaye sasa ni
marehemu,enzi za uhai wake
alibahatika kuwa na kazi nzuri kabla
ya kuoa.
Baada ya kuoa miaka mitano ya
kwanza akabahatika kuwa na watoto
mapacha wa kike na wa kiume na
mke wake aliishi kwa furaha
akifurahia baraka ambazo Mungu
aliwapa familia ile.
Mke hakuwa na kazi na mme akaona
ni vyema amsaidie kwa kumsajilia
kampuni na mama yule akawa na
kampuni ya mitindo na ikafana sana
na kupata umaarufu katika eneo lile.
Miaka michache baadae baadae mme
akapatwa na matatizo kazini na
kusimamishwa kazi na kwa kuwa
alikuwa daktari basi na leseni yake
ya udaktari ikafungiwa na
hakutakiwa kufanya kazi yoyote.
Mpango huo ulisukwa na wenzake
pale kazini kwa kuwa alisifiwa sana
kwa utendaji wa kazi zake na
kupinga vitendo vya rushwa.
Maisha yakazidi kuwa mabaya pale
nyumbani kwani miaka ilivyosogea
hakupata tena wala kuliona lile
penzi la mkewe, kwani mke akawa ni
mtu wa kumchukia mmewe mara
mme akihitaji fedha apewe kwa
masimango na mbaya zaidi hata
watoto wakaanza kufundishwa na
mama yao kumchukia baba yao.
Hali ile ilimpa mzee yule wakati
mgumu na ikafikia kipindi akaanza
kudhohofika mwili kwa mawazo
ingawa akajitahidi sana
kutoyaonesha hayo machoni pa
watu na majirani.
Baada ya muda akapatwa na homa
na akawa akijiuguza lakini baada ya
muda akashauriwa aende akapimwe
na kugundulika kuwa alikuwa na
tatizo katika moyo wake
lililosababishwa na msongamano wa
mawazo.
Akamfuata mkewe ofisini kwake na
kumwambia anatatizo la moyo na
ilihitajika apate msaada wa fedha
kiasi cha laki tano (500,000) ili
afanyiwe upasuaji wa haraka na
kujiokoa katika hali hiyo hatarishi
kwa maisha yake.
Mke alimjibu, " Sidhani kama nina
hela ya kuchezea kwa kukupa
mwanaume usiye na faida kwa
familia yako... yaani mpaka chupi
nikununulie mimi?Wanaume
wenzako wanafanya kazi na sio kama
wewe ulivyo sasa"
Baba alinyanyuka na kuufuata
mlango bila ya kusema neno machozi
yakimtoka na akikumbuka jinsi
alivyoijenga familia yake kwa upendo
na amani akiwapa mahitaji yote na
jinsi alivyotumia mpaka tone lake la
mwisho la fedha, muda na hata
jasho kuinyanyua biashara ya mkewe
ambayo ni kwa ajili ya familia.
Akawasha gari na kuondoka kuelekea
nyumbani akiwa na mawazo huku
akiona jinsi mtu umpendaye
anayoweza kubadilika kiasi cha
kukuombea ufe kwa kuwa ni kero kisa
huna kazi na kumfananisha na wale
wote.
Huku nyuma mke akaingiwa na roho
ya ubinadamu na na kujilaumu kwa
kauli ile na kuanza kuumia kisha
akajaribu kumpigia simu mzee ikawa
haipokelewi na kumka kuliwasha gari
na kuanza kumfuata mzee
Kilomita chache mbele akaona kuna
mkusanyiko mkubwa wa watu akapaki
gari na kuuliza kuna nini?
wakamwambia kuna ajali ya gari
kuna mzee alikuwa anataka kuingia
upande wa kushoto bila kuona kama
kuna gari.
Kusogea pale hakuamini kuona mwili
wa mme wake ukiwa umefunikwa
alianza kutokwa na machozi kabla
ya kuingia kwenye gari na kuona
kuna kadi nzuri ikiwa kwenye
bahasha akaifungua na kuisoma.
Kilio kikubwa kilimtoka baada ya
kugundua kuwa siku hiyo ilikuwa ni
siku za kuzaliwa ya baba huyo na
hakuna aliyekumbuka zaidi ya yeye
mzee kununua kadi iliyoandkiwa "
NAKUSHUKURU MUNGU KWA
KUNIFIKISHA MWAKA HUU MPYA
PAMOJA NA CHANGAMOTO
NINAZOZIPITIA NAAMINI KUNA SOMO
WATAKA KUIPA JAMII KUPITIA MIMI.
UHIMIDIWE BWANA.. HAPPY BIRTH
DAY TO ME"
Mama yule aliomboleza na mpaka
sasa anazidi kuomboleza na hana
amani tena hata faida ya ile
biashara haioni tena na hajui nani
atamsamehe.
Je, unapitia mapito gani sasa katika
mahusiano yako?
Je, unayamudu vipi matatizo ya
mahusiano yako?
Je, unafikiria nini kama siku ukiamka
na kuona wewe ndio chanzo cha
kifo, kilema au chanzo msongamano
wa mawazo kwa mwenza wako
kutokana na tabia zako za ubinafsi?
Ndugu una kila sababu ya
kumshukuru Mungu kwa kukupa
mwenza huyo na kuamini kuwa
katika kila mnalolipitia ni jaribu la
kuwafanya muwe na sababu ya
kuonyeshana upendo vyema zaidi ya
ule wa mwanzo;
Nimeumia sana mpaka nimefikiria
sana mahusiano yangu na watu
wanaonizunguka,
kupitia stori hii nimepata somo la
upendo na uvumilivu na kuzishinda
stress za dunia.

"Nimetumiwa na Rafiki nami nikaona ni vyema tusome wote"
 "Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.