Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 11 May 2014

Nawatakia JumaPili Njema;Burudani-Umoja One SDA Church choir Volume 3 DVD



Wapendwa;Nawatakia JumaPili Njema,Amani,Baraka,Upendo,Utuwema,Kweli,Shukrani,Tumaini,Imani,Upole kiasi na Utukufu Turudishe kwa BWANA......


Sisi twatokana na MUNGU.Yeye amjuaye MUNGU atusikia;yeye asiyetokana na MUNGU hatusikii.Katika hili twamjua Roho wa kweli,na roho ya upotevu.........

Neno La Leo;Waraka wa Kwanza wa Yohana:4;1-21
Kuzipima Roho;1-6
MUNGU ni Pendo;7-21


Na amri hii tumepewa na yeye,ya kwamba yeye ampendaye MUNGU,Ampende na ndugu yake.


Mhhhhhh.......
 Asante/Shukrani;Umoja SDA

"Swahili Na Waswahili"MUNGU Atubariki Sote.

Sunday 4 May 2014

Nawatakia JumaPili Njema;Burudani,Kijitonyama-Twaokolewa kwa Neema Na Nyingine!!!!!!!!

Wapendwa nawatakia JumaPili Njema na Yenye Baraka,Amani,Upendo na Utukufu Turudishe kwake BWANA....

Mimi nitasimama katika zamu yangu,nitajiweka juu ya mnara,nitaangalia ili nione atakalo niambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwanngu.
Neno La Leo;Hababkuki;2:1-5.


BWANA akanijibu akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.





"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Monday 28 April 2014

Mhe Mwigulu Nchemba akizungumzia suala la uraia pacha Washington DC‏

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba akihojiana na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production Washington DC.

Photo Credits: Habari Kwanza blog
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa anajivunia kiasi cha UZALENDO walichonacho waTanzania hapa nchini, jambo linalompa moyo kuendeleza harakati zake za kusaidia kupatikana kwa uraia pacha, ombi lililo kuu kwa waTanzania waishio nje ya nchi katika mabadiliko ya katiba mpya.

Mhe Nchemba, ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika jijini Washington DC nchini Marekani, amesema kuwa ushiriki wa waTanzania na rafiki zao katika maadhimisho haya, umemdhihirishia nia na mapenzi yao kwa nchi yao, na hilo limemsukuma zaidi kusaidia kupitishwa kwa suala la uraia pacha kwenye katiba mpya.

Hii ni ripoti katika kipindi cha Morning Jam

Hotuba Ya Mhe. Mwigulu Nchemba katika sherehe za Muungano Washington DC‏


Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza katika moja ya hafla hapa Washington DC
Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog
Ifuatayo ni hotuba ya Mhe Mwigulu Nchemba.

Naibu Waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Tanzania Bara) aliyoitoa katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano hapa Washington DC.

Audio hii ni kwa hisani ya Vijimambo Blog


Sunday 27 April 2014

Muendelee Vyema na Jumapili Hii Iwe Yenye Maono Na Imani;Burudani-Upendo Group Kijitonyama - Mungu Anakupenda,Sifa na Zivume!!!!

Wapendwa,Natumaini J'Pili hii inaendelea vyema,Na iwe Yenye Imani,Maono/Ndoto,Shukrani na Hekima.
Mithali:29:18;Pasipo Maono,watu huacha kujizuia;Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.


Neno La Leo;Waebrania:11:1-40.[Maana Ya Imani]
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana.






"Swahili Na Waswahili"MUNGU Atubariki Sote.