Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 3 March 2013

Nawatakia J'Pili yenyeUshindi;burudani-Bahati Bukuku na Brown kyando - Unapojaribiwa na Nyingine..!!!!!!!

Wapendwa Muendelee kuwa na J'Pili yenye Baraka,Amani,Huruma  na "UTOAJI"Kwa MUNGU,Yatima, Wajane na kwa Wenyeshida na TABU.....

Na itakuwa,ukiisha kuingia katika nchi akupayo BWANA,MUNGU wako,iwe urithi, na  kuimiliki, na kukaa ndani yake;
Neno la Leo:Kumbukumbu La Torati:26:1-15;
[12]Utakapokwisha kutoa zaka,katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu,ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na  mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;.....................


"Swahili NA Waswahili"Amani na Upendo

Saturday, 2 March 2013

Chaguo La Mswahili Leo-Wenge Musica BCBG - Djodjo Ngonda na Nyingine Nyingii!!!!

Nani alikuambia Afrika si Wabunifu?




Waungwana maneno meengi sinaaa..Mmmhhhh...Kitambo kidogo..walikugusa/Kuwapenda?Jee Bado wapo Juu? Nini /Wapi unakumbuka ukisikiliza Nyimbo hizi?..

Mimi ninawakumbuka watu wengi saana wengine wapo Hai na wengine washatangulia[Kufa].Wengine ninamawasiliano nao Wengine hata sijui wako wapi...Yote ni Maisha.......
Twende Sote sasaaa.......


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Tuesday, 26 February 2013

Watanzania wa Ujerumani kusherekea miaka 49 ya Muungano ,jumamosi 27-04-2013 Mjini Koln ! Ujerumani.!!!!!



Umoja wa watanzania Ujerumani (U.T.U) Unapenda kuwajulisha kwamba  Sherehe za miaka ya Muungano Wa Tanzania Bara na Visiwani zitafanyika mjini Koloni, ujerumani siku ya jumamosi Tarehe 27.04.2013 Kuanzia saa 8 za Mchana
katika ukumbi wa Circus Fabric uliopo katika anuani hii::- 
Bergisch Gladbacher Strasse 1007a
51069 Kцln

Vikundi mbali mbali vinatarajiwa kutumbuiza
Ufunguzi saa 8 mchana
Maigizo ya watoto  
Sarakasi ya watoto
Sarakasi ya wakubwa
Ngoma za kiasili kutoka Tanzania 
Break Dance 
Live Bands
Maonyesho ya mavazi ya kisili ya kitanzania
Pia kutakuwa na chakula (a.k.a mnuso)

Kila mtanzania anaweza kushiriki kuuza bidhaa zake binafsi za sanaa kama Vinyago, picha,michoro, ususi NK. kuchukua nafasi katika ratiba ya maonyesho, wasanii wanaotaka kushiriki katika maonyesho wanatakiwa kujiandikisha moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa UTU kupitia barua pepei ifuatayo-:


Cell:   +491733 779720 
Cell    +491734297997
Umoja ni Nguvu! Utengano ni Udhaifu !


Sunday, 24 February 2013

Natumaini mmekuwa na J'Pili Njema;Burudani- kutoka Makanisa tofauti,Iringa Tanzania na Nje ya Nchi!!!!!!





Wapendwa;Natumaini J'Pili imekwenda vyema...Tumalize siku na Makanisa Mbalimbali waumini wakisifu na kuabudu....

Nawatakia kila lililojema na Baraka......
Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake  itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
Nneno la Leo:ISAYA:62:1-5;Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali,ndivyo wana wako watakavyo kuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi,  ndivyo MUNGU wako atakavyo kufurahia wewe.

"Swahili NA Waswahili"  Muwe na Wakati Mwema.


Wednesday, 20 February 2013

Jikoni Leo;Tupo Ghana- How to make Fu Fu!!!

w


Waungwana;"Jikoni Leo"..Tupo Ghana!!!!!!Unajua kupika FU FU wewee..kazi kwako..ukitaka Kujua Uhondo wa ngoma ......................

"Swahili Na Waswahili" Karibu Saaana.


Tuesday, 19 February 2013

Mapenzi na Wapenzi;Mr and Mrs - Nollywood Movie,Umefanikiwa kuiona hii?



Waungwana;Mliokuwa  na Ndoa na Mnaotarajia na Mnaofikiria na Mliofikia na.........

Kama hujabatika kuina hii..Naomba upatapo muda kidogo ichungulie.....
Na kama wewe ulibahatika kuiona..Jee umejifunza nini? nawe ukishaiona  Tunaomba utuambie nini umejifunza?.

Swali la Kizushi;Ndoa ni NINI?

Karibuni sana katika Yote!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaana.

Sunday, 17 February 2013

TAARIFA YA INSPEKTA JENERALI WA POLISI SAID A. MWEMA KWA UMMA KUHUSU TUKIO LA KUUWAWA KWA PADRE EVARISTI MUSHI ZANZIBAR TAREHE 17 FEBRUARI, 2013


Padre wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Marehemu Evarist Mushi.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema akitoa taarifa ya jeshi hilo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo leo mchana.
 
 
……………………………………………………….
Ndugu Wanahabari,
Nimelazimika nizungumze nanyi kuhusu tukio la kuuwawa kwa Padre Evaristi Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar lililotokea leo asubuhi tarehe 17 Februari, 2013 eneo la Mtoni mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo watu wasiofahamika walimpiga risasi Padre huyo alipokuwa anaenda kusalisha ibada katika kanisa la Betras. Baada ya tukio hilo kutokea alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo baadae alifariki dunia. Tukio hili ni baya na la kusikitisha.
2 Kufuatia kutokea kwa tukio hilo na kujirudiarudia kwa vitendo vya kuwashambulia na kuwadhuru viongozi wa dini na uchomaji wa nyumba za ibada, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumeanza uchunguzi wa kina wa kuwatafuta wanaohusika na matukio hayo.
3Hivyo, nimetuma timu ya wataalam waliobobea kwenye masuala ya upelelezi na oparesheni kutoka Makao Makuu ya Polisi, kwenda kushirikiana na timu ya wataalam iliyoko Zanzibar. Hadi sasa watu watatu wananshikiliwa kwa mahojiano.
Jeshi la Polisi limeimarisha doria maeneo yote hapa nchini na tunafuatilia mienendo na kuakamata watu wote wanaochochea, kufadhili, kuhamasisha na kushiriki katika vitendo vya uhalifu, vurugu na fujo.
Tukiwa katika kipindi hiki, nawaomba wananchi wote hapa nchini kuwa watulivu wakati suala hili linaposhughulikiwa kuhakikisha kwamba wahalifu hao wanakamatwa na sheria inachukua mkondo wake.
Naomba nitumie fursa hii pia, kuwasiliana na wananchi wenzangu wenye taarifa zitakazosaidia wahalifu hao kukamatwa kutupa ushirikiano kupitia namba zetu maalum za simu zifuatazo 0754785557 au 0782417247 na namba za makamanda wa mikoa na vikosi, ili kuhakikisha kwamba amani, usalama na utulivu vinadumishwa hapa nchini.
Nawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano.
AHSANTENI SANA.

Habari na;KapingaZ blog
Asante.