Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 17 July 2012

How to make fresh coconut-milk (Tui la Nazi) - By Miriam Rose Kinunda!!!!!


Waungwana "JIKONI LEO"Si mwingine ni da'Miriam Rose  Kinunda wa "TASTE OF TANZANIA"
Leo anatuletea jinsi ya kuandaa Tui la Nazi.
Pia kaa Tayari kwa Video mpya zinakuja,Kitabu pia Kipo Njiani.
Kipende chako au........Kujua Zaidi Ingi http://tasteoftanzania.com/blog

Jamani eehh Nazi za Kopo,Box,Unga mzipumzishe haswa mliokuwa Nje ya Nyumbani.
Tena Mwezi wa Ramadhani unakuja kwa Wenzetu Wanaofunga Nazi ndiyo yenyewe au vipi?

Mimi hicho Kibao  cha Mbuzi hapa ninapoishi sijakiona,Lakini sina Hofu Jirani  yangu anaweza kuwa nacho si wanasema mpende Jirani yako? hahahhaa..
Na jee kwanini kiliitwa Kibao cha Mbuzi?

Jee wewe Unapenda Nazi? na Unapenda kuunga/kuweka kwenye Chakula Gani?

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaana!!!

Monday, 16 July 2012

Da'Sandra-Neema Atimiza Miaka14!!!!!!!


                      Duuhh miaka 14 si mchezo!!!!!

                     da' Sandra na Rafiki yake da'Frida[Swahili ya Tz na Swahili ya Kenya] wakiwa Drayton Manor ndipo alipofanyia sherehe ndogo na Wanafunzi wenzie.
Shukrani sana kwa Wanafunzi ,Walimu wa Blue Coat

Familia ya Isaac Tunamshukuru sana MUNGU kwa Mema yoote anayotutendea.Asante sana MUNGU kwa kutujalia na kututunzia Sandra.Tunamuweka Mikononi mwako kwa kila Jambo.Wewe watosha BABA.
Asante sana kwa Woote wanaojumuika nasi kwa namna moja au nyingine katika malezi yetu.

MUNGU Azidi kukubariki sana Sandra-Neema,Uwe Baraka kwetu na kwa Watu Wote.

MUNGU Awajalie pia wanaotafuta Watoto.

MUNGU NI MWEMA!!!!!!!!

Unakata Logo/ Wapi utatengenezewa?Fuatana nami!!!!!!!

 
within three days, using the very best professional logo tools designer.

 Logo nzuri ni moja ya njia muhimu na ya pekee kujitambulisha katika soko la bidhaa zako.
 Logo ndio kielelezo cha kampuni yako, na ndio kioo cha kutambulisha bidhaa zako.
 Logo ndio Alama pekee yenye nguvu, na ndio yenye kuzungumza na wateja wako kabla ya kuwasiliana au kukutana nao.
 Basi ili uweze kuwavutia wateja wa bidhaa zako, yakupasa uwe na kielelezo kitakachosema kabla ya wewe kuzungumza.
 Kitu icho si kingine ni ile alama ya utambulisho wa kipekee, aidha ni Logo au lebo za bidhaa zako. Ili uweze kufikia malengo yako ya kibiashara, unaweza kuwasiliana na 99graphix wabunifu wa aina mbali mbali za logo (Nembo).


 99Graphix Design Email: 99graphix@gmail.com http://99graphixdesign.blogspot.com/


Ndiyo waliotengeneza hiyo "Swahili Na Waswhili" hapo juu.
        Pamoja sana.

Jikoni Leo-Mapishi ya coated chicken with chutney - Recipe of (Swahili)!!!!

Waungwana "JIKONI LEO"Si wengine ni "TUPIKE PAMOJA"
Leo wametuletea Mapishi ya Coated Chicken With Chutney.Mmmmhhhh Tamu Sanaaa!!
Hii ni Video Mpya Waungwana Usikose kupitia www.tupikepamoja.com kwa vipimo na kujua zaidi.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja saaaana!!!

EXTRA BONGO NEXT LEVEL YAWAAGA WAPENZI NA WASHABIKI WAKE KWA SHOW KALI ILIYOSINDIKIZWA NA MATONYA, Q CHIF NA CHID BENZ NDANI YA UKUMBI WAO MPYA NEW WHITE HOUSE - KIMARA KOROGWE JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba mbele ya mamia ya washabiki wake jana usiku ndani ya Ukumbi wa New White House Kimara Korogwe

Msanii wa kizazi kipya Bongo Fleva Matonya akiwarusha mashabiki wa Extra bongo usiku wa kuamkia leo ndani ya New white house Kimara Korogwe.

Q chif akiimba kwa hisia kali usiku wa kuamkia leo ndani ya ukumbi wa New white house Kimara Korogwe katika show kali ya Extra bongo ya kuwaaga mashabiki wao, usiku wa leo wanaelekea Finland kwa mwaliko rasmi wa kwenda kufanya show kadhaa huko.

Chid Benz kama kawa akiwarusha mashabiki wake.

Matonya na Q Chif

Choki na Chid Benz

Ally Choki akimsikiliza kwa umakini mdhamini mkuu wa Bendi yake Chif Kiumbe, wakati wa show ya kuwaaga washabiki na wapenzi wao iliyofanyika ndani ya ukumbi wa New white house Kimara Korogwe

Sunday, 15 July 2012

Nawatakia J'Pili yenye Amani na Upendo;Burudani-Elisha Muliri!!!!!!!

Wapendwa nawatakia J'Pili njema.
Neno la Leo;Kitabu cha Pili cha Musa,Kiitwacho,KUTOKA;20:12-17.
Waheshimu baba yako na mama yako;Siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA,MUNGU wako.Endeleaa....

"Swahili NA Waswahili" MUNGU Atubariki Sote!!!!!

Saturday, 14 July 2012

Chaguo la Mswahili Leo-MATONYA feat LADY J.D - ANITA naNyingine Nyingii!!!!!

Waungwana Nimatumaini yangu woote Wazima.
Haya "Chaguo la Mswahili Leo" ni da'Judith[Lady Jayeed]
Vipi mwenzangu kuhusu dada huyu Amekipatia/Kujulia Kipaji chake?
Mimi huwa namkubali sana tuu kwa Muziki /Nyimbo zake.
Pia dada huyu anahusika na JIKONI, kwa hapo mimi siwezi semakitu kwani Sijawahi kufika"NYUMBANI  LOUNGE" Na sijawahi Kuonja Mkono wake[Mapishi yake].
Lakini nasikia ni Moto wa kuotea Mbali.

Jee unalolote unaweza kutuambia kuhusu kazi za dada huyu?
wewe anakubamba/unapenda kazi zake?.
Ngoja Tusikie kutoka kwako tusimalize Uhondo.

"Swahili NA Waswahili" Twende Sotee sasa... Natamanii kuwa Malaikaaa natamakuwa kuwa mtotoooo kohkohkoh Kibanda[Kipaji] hiki cha Kuimba mwenzangu mmhhh hahahha nimekumbuka Nyumbani nikiimba watu woote walala chini kwa kicheko haahahah Oiiiiiiiiiiiiiii 
ok nimekumbuka ngoja nilambe "chumvi" nitarudi tena