Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 13 May 2012

Nawatakia J'Pili Njema na Hongera kina MAMA!!Burudani; mwaitege-mama ni mama.Bahati-Mapito!!!

Da'Rehema na Mwanawe Chance
Wifi'Rehema na Mwanawe Farid.


Nawatakia J'Pili na Hongera kina MAMA Woote popote Mlipo!!
 Kila lenye Kheri,Baraka,Upendo,Uvumilivu,Utuwema,Umoja,Huruma na REHEMA!!!

Wengine tulisha Sheherekea, lakini si Mbaya tukiungana Nanyi tena.

Leo da'REHEMA na wifi REHEMA ndiyo wanaotuwakilisha SWAHILI na WASWAHILI.katika Siku ya MAMA.

3;REHEMA na kweli zisifarakane nawe.6;Katika njia zako zote mkiri yeye,Naye atakuonyesha MAPITO yako.
Neno la Leo;Mithali:3;1-7

Saturday, 12 May 2012

Chaguo la Mswahili Leo;Kutoka kwa Familia ya Penza.Burudani;Diamond - Moyo wangu,Mbagala,Mawazo!!!!!



Diamond na Chance
Diamond na da'Phoibe[Mwana Penza]
Waungwana Leo sipo mbaali sana,yaani si za Kale,Kijana anabamba/anafanya vyema katika Kazi yake, au vipi.
Jee wewe Muungwana Kijana Almasi anakubamba/unapenda kazi yake?Zaidi ni Sauti,Maneno,Muonekano,Uchezaji, Manjonjooo kama si Vionjooo?

Twende Sootee sasaaa, Moyo Wanguuu ooh Moyo wanguuu oooohhh.....Makuti na Mkoleeeeee duuhh mpaka Mkoleeeee!!

Pamoja sana na muwe na J'Mosi njema!!!!!!

Friday, 11 May 2012

Wanawake na Shughuli;Burudani-Bembeleza,Pii pii!!!!


mwanamke akifanya vitu vyake.Picha kwa hisani ya da'Jane Siame wa http://j2wisdom.blogspot.co.uk


Waungwana  natumai wote Hamjambo.

"Wanake na Shughuli " Kumekuwa na Shughuli nyiingi sana zinazohusishwa wanawake tuu.Jee Wanaume Hampendi/Hawapendi Shughuli/kujichanganya peke yenu/Yao?


Au sisi Wanawake ndiyo haswaa tunatakiwa kujichanganya,kufurahi,kukutana wenyewe?


Na jee kwanini tunapoalikana hizo shughuli tunaambiana kuwa ni ya "WANAWAKE TUU" Sasa basi ukienda huko unakuta Dj,Mchukua matukio, Mara kaka,Mjomba kaja na mengine meeengi yanafanywa na "WANAUME".Jee kweli wanawake wa leo hakuna wakutosha kufanya hizo kazi?
Je na hawa MASHOGA  Tumeshawaweka kwenye kundi Letu?

Vipi unapoaga Nyumbani kwa baba Ngina[mume] unaenda kwenye Shughuli za Wanawake tuu, nae anakupeleka na kuishia mlangoni anarudi Nyumbani.
 Akikufuata anakutana na Wanaume kibao wanatoka humo kwa Shughuli jee hii imekaaje?


Mpenzi Msomaji wewe una Mawazo,Maoni,Ushauri Gani katika hili?


Karibuni sana Tuelimishane  Kwa Upendo!!!!

Thursday, 10 May 2012

Mchague Joseph Lukaza !!!!!!!


Mchague JOSEPH LUKAZA ili aweze kuibuka mshindi katika shindano la EXCEL WITH GRAND MALT katika chuo kikuu cha Dodoma katika  Category ya Innovation Nominee
Jinsi ya kushiriki kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa simu unaandika
"INV UDOM JOSEPH LUKAZA 3rd year" alafu unatuma kwenda namba 0653202000.
Na unaweza kupiga kura kwa kutumia tovuti
 
                             

Wednesday, 9 May 2012

Jikoni Leo;Kitabu cha Mapishi cha da'Miriam Rose.Mapishi ya vitumbua kutoka kwa da'Cecy!!!

Cookbook Sneak Peek – Kitabu cha mapishi

Muonekano wa kitabu cha mapishi cha"A Taste of Tanzania".

Cover ame-Design Mwenyewe na Picha amepiga mwenye.Kitabu kitatoka hivi karibuni.

Utakipataje;Ataweka wazi jinsi gani unaweza kupata Kitabu.Ukiingia pale kwake kunasehemu ya mawasiliano,Unaweza kuwasiliana nae Zaidi kupitia http://www.tasteoftanzania.com

Jee da'Miriam anajua KISWAHILI?JIBU;Ndiyo,anakichapa haswa, kama ulivyoona kwenye ile post iliyopita niliandika ni Mswahili.

Nafikiri nimewajibu nijuavyo Waungwana mlionitumia Email na mlionitumia Messages kwenye sim.Na nimeweka hapa kama kuna wengine waliokuwa na maswali kama haya nao Wamepata Jibu.

Haya Waungwana pata mapishi ya UJI na FUTARI kutoka kwa da'Miriam Rose.Hapo juu.

Hapo chini;Mapishi ya "VITUMBUA"Kutoka kwa da'Cecy anapatikana http://mapishinacecy.blogspot.co.uk.

Mswahili mimi kupika vikorombwezo saaaana siweziiiiii,Najua kupika kiasi cha Kula  MUBENA yangu na Watoto yangu na Wageni kidogo tuu,Si kila mtu anaweza kila kitu jamani, Watu na VIPAJI Vyao.MIMI nitakuwa nakurushia Matukio tuu hapa.Na nikipata Muda nitaweza Kuwatembelea Wapishi Nyumbani kwao na Kuwawekea MAZUNGUMZO na MAPISHI HAPA!!AU VIPI WAUNGWANA.SWAHILI NA WASWAHILI!!!PAMOJA SANA TUU.

Monday, 7 May 2012

Jikoni Leo;Mswahili,da'Miriam Rose Kinunda,Pishi-Green Bananas na Mengine meengi ya kujifunza!!!


Da'Miriam Rose
imi huwa navutiwa mnoo na kazi zake dada huyu.Huwa sisiti kumuuliza pale nitakapo kujua zaidi.Sijapata nafasi ya k
HayaWaungwana leo nimewaletea da'Mriam Rose wa Kinunda.


Mukutana nae,Lakini kwa mawasiliano tuu kwangu ni mtu asiye na Majivuno,dharau,Umimi/Ubinafsi.Ni dada Mcheshi na mwenye Upendo, na meeengi.


Hongera sana na Ahsante sana da'Miriam Rose kwa yooote,Mungu azidi kukubariki.


Kufahamu zaidi kazi zake na yeye ni nani ingia "Taste of Tanzania"   http://www.tasteoftanzania.com

Sunday, 6 May 2012

Nawatakia J'Pili Njema,Burudani- Pote Atawala,Unibariki,Umechoka!!!!!!

9:Nami nawaambia,Ombeni nanyi mtapewa;Tafuteni,nanyi mtaona;Bisheni,nanyi Matafunguliwa.

13:Basi,ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,Je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao Wambombao?


Neno la Leo:Luka Mtakatifu;11:1-13.
Mbarikiwe sana na muwe na wakati mwema.