Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Wanawake na Shughuli/Maendeleo. Show all posts
Showing posts with label Wanawake na Shughuli/Maendeleo. Show all posts

Monday 17 February 2014

Tano Ladies Na Maadhimisho ya Siku Ya Wanawake Duniani;Tarehe 8.03.2014!!!!!!

Wakiwa na Mhe.Balozi ;Liberata Mulamula
Wakiwa na Mhe.January Makamba
Wenyewe Wanawake wa Shoka Tano Ladies!!!!

"Swahili Na Swahili"Tukiwa na Nia Moja,Pamoja Tunaweza.

Wednesday 12 June 2013

Coventry Women Gala ya Tarehe-08/06/2013[Sehemu ya 2]Mgeni Alikuwa Mama Balozi JOYCE KALLAGE!!!


Waungwana;Tunaendelea na Matukio ya Coventry Women Gala...Mama Balozi Joyce Kallage na Da'Rose Kiondo..Wakifurahi Pamoja..ni Raha tuu..
Da'Agness akikaribisha Wageni na kujitambulisha.

Da'Halima akijitambulisha na kuwahakikishia watu Watashiba..

Hawa walisimamia Chakula na Kukaribisha Wageni.

Da'Stella akijitambulisha ..Yeye alikuwa msimamizi mkuu.

Da'Mija akijitambulisha..Yeye alisimamia Mitindo

Da'Rachel akijitambulisha..Yeye alisimamia Burudani, ndiye aliyepamba Ukumbi na Mc..
DJ Richie Dee..Yeye ndiyo aliyetuburudisha[Muziki]

Mama Balozi ;JOYCE KALLAGE;
Yeye alitupongeza na kutusisitiza kuendelea na masomo,Kusaidia watoto wengine wa kike Nyumbani wanaohitaji Kuendelea na Masomo lakini hawana uwezo.Kuungana  na kujitoa kwa Moyo na kufanya mambo mengi ya maendeleo.Pia alisisitiza sana tusijisahau Kufuata na kuendeleza mambo mema ya Kwetu..Hategemei mtoto wa mswahili asijue kiswahili ni aibu.Kama tumeshaliachia hili watoto wetu hawajui "KISWAHILI" Tufungue darasa la Kiswahili.
Aliongea Meengi.
Asante sana MAMA,Nasi tutafuata Ushauri wako.
[TEAM MAMA BALOZI]

Wanawake Oyeee!!!!Coventry Women Gala Oyeee!!!!!Waswahili Ughaibuni Juu!!!!!Wanawake na Maendeleo!!!!!
Amesema amefurahi kuona tumeweza kurudia tena!!

Hayo yote kwa furaha na unyenyekevu yalitoka kwa da'MARIAM KILUMANGA;Mwenyekiti wa;Tanzania Women's Association[TAWA UK.]
Alisisitiza Tusikate Tamaa na yupo pamoja nasi wakati wowote..Da'Mariam tulikuwa nae wakati uliopita.
Asante Saaaaana.
Dada/Mama;Hilda..Yeye ni Mfanyabiashara wa siku nyimgi,Amepitia changamoto nyingi sana.
Na sasa amesimama vilivyo..Ametufunza mambo mengi sana..alisema yeye si muongeaji sana..Mzuri sana kwenye Vitendo.

Asante Sana kwa Yote mama.


Dada;ROSE KIONDO,Kutoka Ubalozi wetu wa Tanzania hapa UK.

Da'ROSE KIONDO;Yeye alitusisitiza kujihusisha na Ubalozini kwani pale ni kwetu na tutambue hivyo..kwanini tunakuwa waoga na Nyumbani kwetu?Mtu hujivunia chake na kwako..kwa hapa tulipo Pale ndiyo Nyumbani,Wapo pale kwa sababu yetu pia.Aliongea Meengi yenye Faida kwetu.

Asante sana dada.

Alicheza kwanza..

Alitumia vilivyo uwanja...

Mc..mwenyewe hoii..usimchezee kabisa..Mada zake anazitunza vilivyo..

Ni-Aunty/Mama da'Fay..wewe utakavyo penda kumuita yeye hana shida..Yeye alitusisitiza zaidi,kutumia muda vizuri,kujiendeleza kielimu kwani haina mwisho..atakushangaa eti ukisema sina muda kwasababu nina watoto,mume,kazini,kazi za nyumbani..Ukiamua na kama wewe ni msomaji utasoma tuu..ni wewe utakavyojipanga..kila siku utasema muda huna mpaka lini?Tusipoteze muda kwenye mambo yasiyo na manufaa..hasa  tutumie hii MITANDAO vyema na si kutukanana na kuumizana..Tupendane..
Bila kusahau DIET..Na kutafuta mbinu ya kupunguza mwili..Aliongea meengi saana siwezi kumaliza yote hapa..


EPUKA UZEE USIOKUWA WAKO BIBI EEEEEHH.
.

Da'SUSAN

DA'SUSAN yeye aliongelea MADAWA YA KULEVYA..Utayajuaje,Watumiaji,kuepuka,uuzaji,Madhara yake na kuwalinda watoto wetu,Vijana,Jamii na nasisi wenyewe pia..Na mambo mengii yahusianayo na Madawa ya kulevya..

Asante sana.
Umeona hiyo beji niliyo jibandika hapo? Hawa wanatengeneza keki,beji na mengine meengi..ni wadada wanaojituma..ni AHLAM NA KOIYA..Wape Kazi watoto wa Nyumbani..
Hongereni Sana

Da'TINNA..Yeye ni mwimbaji  mzuri sana sauti MUNGU amemjaalia..usisite kumpa kazi. Dada/Mtoto wa Nyumbani.ni burudani tosha sauti yake.

Mama Balozi,Wageni walipata Nafasi  ya kuona/kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wanawake Wenzao...


Wewe unangoja nini?
Jitoe,Jitambulishe/Tambulisha kazi zako.Ujuzi wako..
Nategemea Kuwaona Wanawake wengi Shughuli ijayo..








Monday 10 June 2013

Coventry Women Gala ya Tar;08/06/2013-Mgeni;Mama Balozi Joyce Kallage;[Sehemu ya 1]!!!!

Waungwana;CoventryWomen Gala ya safarihii tulikuwa na Mama Balozi JOYCE KALLAGE.
Ameongelea nini Yeye pamoja na Wageni wengine?Usihofu nitakufahamisha..kwa leo Angalia Picha Kwanza. 
[TEAM MAMA BALOZI] 

Mama na Wanamitindo

Mama na Mbunifu wetu da'Mija na da'Halima[Maonyesho ya Mavazi yote ni kazi ya mikono ya Da'Mija!!]
  Mama Balozi Joyce Kallage hayuko nyuma kwenye MITINDO!!!!!




  Nasi tuliungana na wanamitindo kuonyesha Umoja....


  Wanamitindo wakipoziiii..




 

  Da'Rose Kiondo kutoka Ubalozini alikuwa na mengi ya kutuambia..nitakujulisha..


 Wamama wa Coventry na mama Balozi Joyce








  Asante sana mama yetu kwa Ukarimu na kuungana nasi....da'Stella alituwakilisha na kumkabidhi maua kama ishara ya Upendo wetu kwake..














   Mitindo ni kazi ya Mbinifu wetu hapa Coventry..Mwanamke wa Shoka...Da'Mija!!!

 Tulicheza saaaana..

   Itaendelea.....

    "Swahili Na Waswahili" Raha Tupu.