Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!
Showing posts with label Kheri na Baraka. Show all posts
Showing posts with label Kheri na Baraka. Show all posts

Sunday 6 March 2016

Natumai JumaPili ilikuwa njema;Happy Mother's Day..Burudani-Miriam Paul-Nipe Macho,Mvua ya Baraka......



Wapendwa waungwana; Habari za siku nyingi,Natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na mwaka huu mpya..
Tunamshukuru Mungu kwa yote,Mungu yu mwema sana..nimeadimika kidogo mambo ni mengi familia imeongezeka
basi na majukumu yameongezeka,Lakini Mungu yu pamoja nasi na tupo pamoja tena..
Natumaini jumapili ilikuwa/inaendelea vyema
turudishe utukufu wa Mungu muumba wa yote...
"Happy Mother's Day" kwa wamama wote, Mungu atupe hekima,Busara katika Malezi ya Watoto wetu..
Mungu pia awaguse wenzetu wanaohitaji watoto ,akawape furaha hii nao wakafurahi pamoja na wengine..
Pia akawape sawasawa na mapenzi yake..
kuna ambao hawana kabisa ,Mungu yu pamoja nanyi,
Kuna walionao wa jinsia moja kike/kiume ,Mungu anamakusudi yake.
Kuna walionao lakini hawawajali/wameterekeza.Mungu awaguse mkumbuke majukumu yenu...

1Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:

2Nikuambie nini mwanangu?
Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?
Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?


 Neno La Leo;Methali 31:1-31

Mawaidha kwa mfalme
1Maneno ya mfalme Lemueli. Mawaidha aliyofundishwa na mama yake:
2Nikuambie nini mwanangu?
Nikuambie nini mwanangu niliyekuzaa?
Nikuambie nini wewe niliyekuomba kwa Mungu?
3Usimalize nguvu zako kwa wanawake,
usiwape mali yako hao wanaoangamiza wafalme.
4Haifai ee Lemueli, haifai wafalme kunywa divai,
wala wakuu kutamani vileo.
5Wakinywa watasahau maagizo ya sheria,
na kuwanyima haki wenye taabu.
6Mpe kileo mtu anayekufa,
wape divai wale wenye huzuni tele;
7wanywe na kusahau umaskini wao,
wasikumbuke tena taabu yao.
8Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu;
na kutetea haki za wote wasiojiweza.
9Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki,
linda haki za maskini na fukara.




Mke mwema
10Mke mwema kweli, apatikana wapi?
Huyo ana thamani kuliko johari!
11Mumewe humwamini kwa moyo,
kwake atapata faida daima.
12Kamwe hamtendei mumewe mabaya,
bali humtendea mema maisha yake yote.
13Hutafuta sufu na kitani,
na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.
14Yeye ni kama meli za biashara:
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15Huamka kabla ya mapambazuko,
akaitayarishia jamaa yake chakula,
na kuwagawia kazi watumishi wake.
16Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua,
na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake.
17Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
na kuiimarisha mikono yake.
18Hutambua kwamba shughuli zake zina faida;
hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa taa yake.
19Husokota nyuzi kwa mikono yake mwenyewe,
kwa vidole vyake mwenyewe husuka nguo zake.
20Huufungua mkono wake kuwapa maskini,
hunyosha mkono kuwasaidia fukara.
21Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe,
maana kila mmoja anazo nguo za kutosha.
22Hujitengenezea matandiko,
mavazi yake ni ya zambarau ya kitani safi.
23Mume wake ni mtu mashuhuri barazani,
anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi.
24Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza,
huwauzia wafanyabiashara mishipi.
25Nguvu na heshima ndizo sifa zake,
hucheka afikiriapo wakati ujao.
26Hufungua kinywa kunena kwa hekima,
huwashauri wengine kwa wema.
27Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake,
kamwe hakai bure hata kidogo.
28Watoto wake huamka na kumshukuru,
mumewe huimba sifa zake.
29Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu,
lakini wewe umewashinda wote.”
30Madaha huhadaa na uzuri haufai,
bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa.
31Jasho lake lastahili kulipwa,
shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.

                Bible Society of Tanzania
Jifunze zaidi









Mungu awabariki wote mliopita hapa,
muwe na wakati mwema.








"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Friday 25 December 2015

Nawatakia Christmas Njema;Burudani-Boney M. Christmas Album FULL 1981,Baba Gaston - Kakolele Viva Christmas

Nawatakia  Christmas Njema Iwe yenye Heri,Baraka,Furaha na Aamani.

"I wish everyone a  Merry Christmas" 
 







"Swahili Na Waswahili"Muwe na Wakati mwema.

Sunday 25 October 2015

Nawatakia Jumapili Njema na Uchaguzi mwema ;Tanzania Kwanza,Burudani-Kinondoni Revival Choir Twalilia Tanzania

Wapendwa/Waungwana natumai hamajambo na Jumapili hii ya Uchaguzi Tanzania ni njema..
Mungu azadi kuibariki Tanzania na Watanzania katika yote,Uchaguzi uwe wa haki,Amani,Utulivu.
Amani,Upendo,Umoja,Mshikamano,Undugu,Hekima,Busara vikatawale...
Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.


1Ndugu zangu, ninataka na kutazamia kwa moyo wangu wote hao wananchi wenzangu wakombolewe. Tena nawaombea kwa Mungu daima. 2Maana naweza kuthibitisha kwa niaba yao kwamba wanayo bidii ya kumtafuta Mungu; lakini bidii hiyo haikujengwa juu ya ujuzi wa kweli. 3Maana hawakufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu wawe waadilifu, na wamejaribu kuanzisha mtindo wao wenyewe na hivyo hawakuikubali njia hiyo ya Mungu ya kuwafanya wawe waadilifu. 4Maana kwa kuja kwake Kristo, sheria imefikia kikomo chake, ili wote wanaoamini wafanywe waadilifu.

Neno La Leo;Warumi 10:1-21
Ukombozi kwa wote
5Kuhusu kuwa mwadilifu kwa kuitii sheria, Mose aliandika hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya sheria ataishi.”6Lakini kuhusu kuwa mwadilifu kwa njia ya imani, yasemwa hivi: “Usiseme moyoni mwako: ‘Nani atapanda mpaka mbinguni?’ (yaani, kumleta Kristo chini); 7wala usiseme: ‘Nani atashuka mpaka kuzimu?’ (yaani, kumleta Kristo kutoka kwa wafu).” 8Maandiko Matakatifu yasema hivi: “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani tunayoihubiri.9Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. 10Maana mtu huamini kwa moyo akafanywa mwadilifu; na hukiri kwa kinywa akaokolewa.11Maandiko Matakatifu yasema: “Kila anayemwamini hataaibishwa.” 12Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao. 13Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.”



14Basi, watamwombaje yeye ambaye hawamwamini? Tena, watamwaminije kama hawajapata kusikia habari zake? Na watasikiaje habari zake kama hakuna mhubiri?15Na watu watahubirije kama hawakutumwa? Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Ni jambo la kupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiri Habari Njema!” 16Lakini wote hawakuipokea hiyo habari njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 17Hivyo basi, imani inatokana na kuusikia ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.
18 Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:
“Sauti yao imeenea duniani kote;
maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
19Tena nauliza: Je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni wa kwanza kujibu:
“Nitawafanyeni muwaonee wivu
watu ambao si taifa;
nitawafanyeni muwe na hasira
juu ya taifa la watu wapumbavu.”
20Tena Isaya anathubutu hata kusema:
“Wale ambao hawakunitafuta wamenipata;
nimejionesha kwao wasiouliza habari zangu.”
21Lakini kuhusu Israeli anasema:
“Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”
Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Sunday 4 October 2015

Muendelee vyema na Jumapili hii;Burudani-Mchanganyiko(African Praise&Worship)

Wapendwa/Waungwana;Muendelee vyema na Jumapili hii...
Baraka,Amani,Furaha,Upendo,Hekima,Busara vikatawale majumbani mwenu
Shukrani na Utukufu ni kwa MUNGU.


1Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Timotheo, tunawaandikia nyinyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho, na watu wote wa Mungu kila mahali katika Akaya. 2Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.


Neno La Leo:2Wakorintho 1:1-23
Shukrani kwa Mungu
3Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote. 4Yeye hutufariji sisi katika taabu zetu zote, ili nasi tupate kuwafariji wengine katika kila taabu kwa faraja hiyohiyo tunayopokea kutoka kwa Mungu. 5Naam, kadiri mateso ya Kristo yanavyozidi ndani yetu, ni kadiri hiyohiyo tunazidi kufarijiwa naye. 6Ikiwa tunapata taabu, basi ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu. Tukifarijika, ni kwa ajili ya kuwafariji nyinyi na kuwaunga mkono mpate nguvu ya kustahimili mateso yaleyale tunayoteseka sisi. 7Tena, matumaini tuliyo nayo kwa ajili yenu ni imara; tunajua kwamba mkishiriki mateso yetu, mtashiriki pia faraja yetu.
8Ndugu, tunataka kuwajulisheni taabu zilizotupata kule Asia; taabu hizo zilitulemea kupita kiasi, hata tukakata matumaini yote ya kuendelea kuishi. 9Naam, tulikuwa kama watu waliohukumiwa kuuawa, ili tufundishwe kumtegemea Mungu mwenye kuwafufua wafu, badala ya kutegemea nguvu zetu sisi wenyewe. 10Yeye alituokoa katika hatari kubwa ya kifo, na anaendelea kutuokoa; sisi tumemwekea tumaini letu kwamba atatuokoa tena, 11nyinyi mkiwa mnatuunga mkono kwa kutuombea. Hivyo neema tutakazokuwa tumepata kutokana na maombi ya watu wengi hivyo, ziwe sababu ya watu wengi zaidi kumshukuru Mungu kwa ajili yetu.
Badiliko katika safari ya Paulo
12Sisi tunajivunia kitu kimoja: Dhamiri yetu inatuhakikishia kwamba tumeishi ulimwenguni hapa, na hasa kati yenu, kwa unyenyekevu na unyofu tuliojaliwa na Mungu; hatukuongozwa na hekima ya kibinadamu bali na neema ya Mungu. 13Tunawaandikia nyinyi mambo mnayoweza kuyasoma na kuyaelewa. Ninatumaini kwamba mtaelewa vizuri kabisa, 14maana mpaka sasa mmenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwamba katika ile siku ya Bwana Yesu mtaweza kutuonea sisi fahari kama nasi tunavyowaonea nyinyi fahari.
15Nikiwa na matumaini hayo, nilikusudia kuja kwenu hapo awali ili mpate baraka maradufu. 16Nilikusudia kupita kwenu nikiwa safarini kwenda Makedonia na wakati wa kurudi pia, ili nipate msaada wenu kwa safari yangu kwenda Yudea. 17Je, mnadhani nilipopanga hivyo nimekuwa kama mtu asiye na msimamo? Je, mnadhani kwamba ninafanya uamuzi wangu kwa fikira za kibinadamu na kwamba nasema “Ndiyo” na “Siyo” papo hapo? 18Mungu ni ukweli tupu; basi, kile tulichowaambia nyinyi si jambo la “Ndiyo” na “Siyo”. 19Maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, ambaye mimi, Silwano na Timotheo, tulimhubiri kwenu, hakuwa mtu wa “Ndiyo” na “Siyo;” bali yeye daima ni “Ndiyo” ya Mungu.20Maana ndani yake ahadi zote za Mungu zimekuwa “Ndiyo”. Kwa sababu hiyo, “Amina” yetu husemwa kwa njia ya Kristo kwa ajili ya kumtukuza Mungu. 21Mungu mwenyewe ndiye mwenye kutuimarisha sisi na nyinyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu; 22ndiye aliyetutia mhuri wa kuwa mali yake yeye na kutujalia Roho mioyoni mwetu kama dhamana ya mambo yote ambayo ametuwekea.
23Mungu ndiye shahidi wangu; yeye anajua moyo wangu! Mimi sikuja tena Korintho kwa sababu tu ya kuwahurumieni. 24Hatutaki kutumia mabavu juu ya imani yenu; nyinyi mko imara katika imani yenu. Wajibu wetu ni kufanya kazi pamoja kwa ajili ya furaha yenu.
Bible Society of Tanzania

"Swahili na Waswahili" Mbarikiwe Sana.