Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 13 January 2012

Wanawake na Urembo!!!!!!!!






Nimatumaini yangu woote wazima,
Haya Waungwana Wanawake na Urembo! Kuna mengi kwenye hizi picha na kwa Wanawake kwa Ujumla,
Mimi leo si msemaji saana,Kazi kwenu nyie na Mitazamo yenu,kipi wewe umependa hapo/Kukuvutia na kipi hujapenda hapo,yaani kama ingekuwa wewe hapo ungeongezea nini au ungepunguza nini,Pia wewe Mwanaume kama ni Mkeo,dada,shangazi na...Ungependa nini aongeze au  apunguze nini?Na jee labda unapenda lakini hujui ufanyeje uwe/awe kama hivyo,au kunakingine unapenda hapo hakipo,Basi usisite kusema/Kutoa Mawazo,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

Karibuni sana.


Tuesday 10 January 2012

Wazazi /Walezi wa sasa na Malezi!!!!!!




                        watoto kutusaidia jikoni.

kusafisha vyumba vyao.

kusaidia kusafisha na sehemu nyinngine
Wabaki na Furaha/Amani.
Ni matumaini yangu wote wazima,
Haya wapendwa,Wazazi/walezi wenzangu,vipi watoto kufanya/kusaidia kazi za nyumbani,
Hii imekaaje/wewe unaonaje?kazi kama kusafisha vyumba,kuosha vyombo,kuaanda vyakula na kazi nyingine nyingi,Jee wewe unafikiri ni Umri gani uliosahihi kwa mtoto kuanza  kumfundisha kazi ndogondogo?naje huu ni Unyanyasaji au ni malezi ya kawaida? naje Kuna kazi za watoto wa kiume na wakike?kama ndiyo jee sisi wenye watoto wa jinsia moja je?Unafikiri watoto wote wanapenda kazi? je kama hataki?.
Mimi binafsi kazi nyingine sikuwa nazipenda kufanya nilipokuwa mtoto,lakini mama alikuwa ananilazimisha, jee alikuwa ananikosea au ndiyo malezi?Jee wewe unapenda/ulipenda kazi zote ufanyazo/ulizokuwa unafanya?.
Mwana Umleavyo ndivyo akuavyo au.......

Karibuni sana Waungwana katika kusaidiana Kimawazo,Kujadili na Kuelekezana kwa Upendo!!












Thursday 5 January 2012

Waswahili na Maisha yao-Coventry Swahili Party/Mwaka Mpya[shukrani]!!!



                             Asanteni sana  Swahili dadazzzz.
                                   dada Esther Asante.
                                      Wapendwa Mungu awabariki sana.
                                       Mbarikiwe Malongazzzzz.
                                    Ahsante sana mamaKisa.
                                       Ahsante sana Dj Rik/blogger wa the network.





                   Chakula; Nyama choma na vyote,Vimepikwa kwa  da'Batuli.
Ahsanteni sana wote kwa Upendo na kutoa Muda wenu kwa kujumuika nasi ,  Mungu awabariki sana,Tunawatakia kila lililo jema.Kwaniaba ya da'Maggie ,da'Vick na Familia yangu,TUNAWAPENDA SANA.